Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

ONTARIO bado haujaanza kupiga biashara USA?? I mean kuhusisha vitu vyovyote kutokea nchi hiyo?
Nimeona unamshkaji Washington, sasa nataka nijue kama umeshaanza kuwatumia watu unaojuana nao ili kukuletea faida( mi naamini kila kitu katika hii dunia kinaleta pesa, ila inategemea unakitumiaje)
 
Hakuna mtu duniani atakupa feed formula hata ufanyaje boss, hapa nisikufiche. Sawa na Cocacola kutoa formula ya vinywaji vyake.

Kuku 500 hawatakiwi kula zaidi ya mifuko 26 ya kilo 50
Sawa
Nadhani lengo lako ni zuriii kabisa
Kusaidia jamii kutoka hapa tulipo kupga hatua mbele zaida...fine

Nifanyeje sasa ili nami niweze kufuga kwa faida?
 
Shukrani mkuu kwa kurudi tena!
Kwenye ule Uzi wako ulipita ulinitia moyo sana Na umenipa ari mpya!
Ila nikawa nafikiria unatokea familia Fulani mboga saba!
Ila huu Uzi umemaliza dauti zangu zote kama umepigana sana!
Hongera sana mkuu kwa Mara nyingine
 
Mid sized companies kwa Bongo unabidi uwe na turn over ya bil 1 - 20 kwa mwaka.
Mkuu uko vizuri sana upstairs, salute!!! Umejibu vizuri sana kwa kuelezea midium size company. Hii ina maana small ni below that range na large ni above that range. I am not concerned whether the range for mid sized is OK or not, but the way you put it, is marvelous!!!
 
ONTARIO bado haujaanza kupiga biashara USA?? I mean kuhusisha vitu vyovyote kutokea nchi hiyo?
Nimeona unamshkaji Washington, sasa nataka nijue kama umeshaanza kuwatumia watu unaojuana nao ili kukuletea faida( mi naamini kila kitu katika hii dunia kinaleta pesa, ila inategemea unakitumiaje)
Boss sijui hasa swali lako ulikua unamaanisha nini. Sijawahi kufanya biashara yoyote na USA, na kwasasa sitegemei any soon. Lakini nimewahi kuagiza vitu kadhaa kutoka USA lkn kutumia eBay.

Kuhusu kujuana na mUSA na kunisaidia kibiashara... iko hivi nilikutana na Prof. Thom Jayne huyu ni Foundation professor kutoka Michigan State university na Director wa Alliance for African Partnership.

Alinipa mchongo m1 wa kuniunganisha na prof Sianga wa Eldoret university, tukaingia mkataba wa wao kufanya research kwenye kuku wangu kwenye kudevelop Probiotics an alternative to antibiotics. So nakula faida mara 2, kulipwa na hawa watu wa research na kuuza products zng.

Hp nikiwa na Prof Jane
2017-05-22+18.20.jpg
 
Boss mwezi wa 10 ndio muda muafaka wa kilimo cha mihogo, kwenye zile vuli. Japo mimi nilichelewa lkn kiukweli mvua hizi zimeniboost sana.

Nunua mbegu ya Monsanto inaitwa VIRCA, hii kitu ni mkombozi, haishikwi ma magonjwa ya kipuuzi puuzi. Ukifata principles na ukiwa na soko la uhakika utapiga pesa nzuri, 1.5-2 mil faida kwa hekari... na si unajua hiki kilimo ni cha kimaskini, gharama za uzalishaji ni reasonable sana hasa mvua zikikubali. So ukianza zako na heka 10, unaeza ukapata pata tufaida twa kulimia heka 50.
Mkuu nina ardhi mkoani ruvuma nataka nilime Mohogo ila sijui process zake na hasa Soko lake ni wap
 
mkuu naomba kujua aina gan ya kuku kwa hizo aina ni bora na garama za matunzo kidogo ziko chini?
Boss swali gumu kidogo, lkn mimi kumshauri mtu anayeanza ningemwambia aanze na Broilers. Kwanini? hawa ukiwa makini nao wanakupa pesa kila mwisho wa mwezi I mean siku 35. So ni rahisi wewe kujichanga. Gharama yao haipaswi kuzidi 500,000 (kwa kuku 100) nawe ukiuza kwa bei ya kienyeji ya laki 6, then faida yako ni laki 1 kwa kuku 100.

Kama una mtaji mzito na hauna haraka ya pesa gonga layers (kuku wa mayai). Kamwe hutotafuta mteja ukiweza kuzalisha trei 200 kwa siku. Yani wakianza kutaga wewe ni kukusanya milioni kila siku kwa miezi 18 mfululizo.
92a39400b50035d834adef0eceecf1b0.jpg
 
Shukrani mkuu kwa kurudi tena!
Kwenye ule Uzi wako ulipita ulinitia moyo sana Na umenipa ari mpya!
Ila nikawa nafikiria unatokea familia Fulani mboga saba!
Ila huu Uzi umemaliza dauti zangu zote kama umepigana sana!
Hongera sana mkuu kwa Mara nyingine
Ningekua mboga 7 sahivi ningekua nipo na kina Gigy mane napima oil. Hahahaa
 
Boss swali gumu kidogo, lkn mimi kumshauri mtu anayeanza ningemwambia aanze na Broilers. Kwanini? hawa ukiwa makini nao wanakupa pesa kila mwisho wa mwezi I mean siku 35. So ni rahisi wewe kujichanga. Gharama yao haipaswi kuzidi 500,000 (kwa kuku 100) nawe ukiuza kwa bei ya kienyeji ya laki 6, then faida yako ni laki 1 kwa kuku 100.

Kama una mtaji mzito na hauna haraka ya pesa gonga layers (kuku wa mayai). Kamwe hutotafuta mteja ukiweza kuzalisha trei 200 kwa siku. Yani wakianza kutaga wewe ni kukusanya milioni kila siku kwa miezi 18 mfululizo.
92a39400b50035d834adef0eceecf1b0.jpg
Dah nashukuru sana mkuu sikutegemea kama utanijibu kwa uwazi namna hii..Ubarikiwe kiongozi
 
Mkuu nina ardhi mkoani ruvuma nataka nilime Mohogo ila sijui process zake na hasa Soko lake ni wap
Ruvuma mbali boss wng.

Watu wengi wanalima mihogo pwani ambapo ni karibu na Dar. Ukiweza kujaza canter na kuleta Buguruni, Dar, wala huiti wateja. But mimi hua nauzia shamba - tunamalizana porini, bugudha za mjini sitaki.
 
Ila kwa mahindi Ruvuma ni sawa?Ndipo nina uhakika wa kaeneo mkuu
 
Back
Top Bottom