Ahhhh!
Kama lengo lako kubwa ni hilo nimekuelewa vizuri Sana. Ukichunguza comments zangu kuhusu maamuzi mbalimbali ya marefa likiwemo goli Kona dhidi ya Yanga, penati zisizokuwa penati, Kadi za njano zilizostahili nyekundu dhahiri nk huwa nasisitiza "uwezo wa marefa ni mdogo" halafu ndo lije suala la kuhongwa. Siwezi kulaumu rushwa au upendeleo bila uthibitisho lakini kilicho dhahiri ni kwamba marefa wa kitanzania hawana uwezo kabisa wa kufikia maamuzi sahihi katika matukio mengi, na hili linathibitishwa na jinsi Kamati ya Waamuzi ya CAF inavyowachukilia wa kiwango cha chini na hivyo kutowapanga kuchezesha mashindano Makubwa ya CAF/FIFA. Kama tatizo lingekuwa ni rushwa hapa ndani huko CAF wangefanya vizuri lakini wanaonekana ule msemo maarufu wa "MADHAIFU YA KIBINADAMU" umedhihirika zaidi kwao kuliko nchi nyingine.