Umeshakaa ukawaza kuwa muda wowote unaweza itwa na ukajikuta mbele ya Muumba wako? Ulishaandaa majibu ya kumpa utakapoulizwa juu ya matendo yako likiwemo hilo la kuzini moyoni na kujichua?
Kaa tafakari. Jua kuwa kama wanavyoanguka wengine sasa, kuna siku, na inaweza isiwe mbali, zamu yako itafika. Hakikisha unafanya amani na Mungu mapema kabla ya siku hiyo, ambayo inaweza kuwa miaka 50 mbele au ikawa leo hii hii.
Mathayo 5
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Waebrania 9:27
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;