Mabadiliko huanza ndani yako mwenyewe.
Mabadiliko hayaanzii nje yako ewe
Miss Natafuta.
Ukibadilisha mazingira ya nje yako wakati ya ndani hujayabadili basi kumbuka utakuwa unatwanga maji kwenye kinu tu.
Fikiria mtu ambae alikuwa anataka aache punyeto alipaka mpaka pilipili mikononi ili aache,lakini ilipofika muda akaenda mwenyewe kunawa mikono na akapiga punyeto yake alipomaliza akajilaumu.
Hapo ni kuwa usitegemee sababu za nje kutaka kubadilika.sababu za nje hazipo na sisi mda wote.
Wewe upo na wewe kila unapoenda na wala haupo na simu yako wala tv.kwa hiyo kama kuepuka kwako kuangalia picha za ngono unategemea kuiacha simu yako na kuuza basi jua sababu ya nje umeiepuka ila je unaweza kuiepuka nafis yako ambayo upo nayo kila unapokwenda?basi kama huwezi kuiepuka basi vizuri ukaanza na mszoezi ya kuibadilisha nafsi.
Ukiibadilisha nafsi yako basi utaenjoy maisha utajikuta unamiliki simu,TV na wala hupati tabu ya kutumia nokia ya tochi kwa sababu ya kuepuka kuangalia porn movie.haya yanatokea endapo umeamua kuibadilisha nafsi yako kwanzaa kabla ya chochote.
Na hiyo nafsi ndo sababu ya ndani kabisa ya wewe kuangalia hizo porn.
Sasa njia za kubadilisha nafsi yako ili iwe na uwezo wa kujizuia ni njia rahisi sana na zina mafanikio makubwa lakini kabla haujaanza kuibadilisha kamatia huu msingi hapa chini usemao..
"katika kila lengo lako unalotaka ufikie basi kuna maumivu na tamaa unatakiwa uishinde na uikimbie"
Na msingi wa pili pia uelewe kuwa..
"hakuna nafsi yeyote isiyotamani mambo yenye kufurahisha lakini nafsi imepewa akili na iuwezo wa kuyakwepa mambo hayo"
Hivyo basi usione watu wamekaa ukajua hawatamani kabisa kuangalia porn hapana,nafsi wakati mwingine zinawaambia "angaliaa" lakini wana uwezo wa kudhibiti nafsi zao na kupotezea ushawishi kama huo.
Lakini pia kumbuka katika ile fomula ya kwanza kuwa hautokaa kabisa ukaja kuona umechukiaaa tuu hiyo hali,bali unatakiwa upitie hatua kadhaa ili usiitamani na kuifanya hata kama fikra inakujiaa.
Picha za ngono ni hatari sana kwa afya ya ubongo.
Kuna bwana mmoja alisema kwamba " ana miaka 13 toka ameacha kuangalia lakini mpaka mwaka huo wa 13 bado zile picha za ngono zinamjia kichwani licha ya kuwa ana miaka 13 tokea kuacha kwake,vipi wewe unaendelea mpaka leooooo je itakuwaje?
Chukua hatua.