Naomba ushauri jinsi ya kumuapproach aliyenitafutia kazi, nataka kuacha kazi

Kijana jitahidi Kazi usiache.

Cha msingi Uombe Internal Recategorization uzur ushakuwa na Connection hapo ni easy.

Usiache Kazi

Sie wengine tulifanya Mambo ya hatar na ya kuumiza ili kulinda Heshima na CV kwa wale waliotupachika/kutuamini/kutushika Mkono.

Nilifika stage mtu nikimuomba Msaada wa Kazi / Mishe akininyima au akiwa mzito kunisaidia silaumu kwasababu najua kuna Watu itakuwa aliwasaidia na wao wakamuangusha na always ipo hivyo.

Watu kama nyinyi ndio mnafanya watu kuwa WANYAMA wasitoe msaada wowote tena.
 
Nashukuru sana Kwa ushauri wako. Ila kabla ya kuomba Kazi nilikuwa Nina harakati ambazo nafanya ndio hizohizo nataka kuziendelezea pale zilipoishia.
Girl go for on na hizo harakati kama zipo proper utafika mbali
 
Nashukuru mkuu Kwa ushauri wako. Nilichokuja kuomba hapa ni approach za kumwambia aliyenitafutia kazi Kuwa naacha kazi. Ulichoandika kina mantiki ila ni irrelevant na nilichoandika Mimi
 
Acha hio kazi kimya kimya mkuu, km nafsi yako inakataa na inakusuta aaaacha mara moja na huyo mzee huna hata haja ya kumwambia chochote, endelea na harakati zako zingine tu
 
Mkuu nashukuru sana Kwa mchango wako. Mtaani ni pagumu everyone know that hata Mimi najua ila kikubwa ni kuwa nimejifanyia tathmini I don't fit na nipo more motivated kufanya harakati zangu
 
Hakuna kitu kibaya unachotaka kufanya,ni bora huyo mzee angekutafuta kuhusu kukupa hiyo nafasi lkn ww ndio uliomba msaada wake,sasa ndani ya muda mfupi unataka kuacha...kifupi utajiharibia sana sio kwenye kazi tu,lkn utakua huaminiki tena,...huwezi jua huyo mzee ana network kiasi gani,inaweza tokea nafasi akae recommend kua huaminiki...ushauri ungefanya hiyo kazi hata mwaka mmoja,kwanza hakuna kazi nyepesi,changamoto kazin ni kawaida.
 
Wakuu nashukuru sana. Siwapangii Cha kunishauri ila kimsingi nafsi yangu ishafanya maamuzi ya kuacha ila nachohitaji ni jinsi ya kumpa taarifa aliyenitafutia kazi
 
Umenikumbusha machungu, nilipambana kumtafutia post nduguyangu wadamu kabisa My really brother.

Akaiacha baada ya mwezi mmoja, yeye alinitumia mseji akanishukuru sana akasema nashukuru sana mdogoangu kwa kunipigania lakini nimeamua kuacha kazi nimepata sehemu nyingine.

Daaaah ilikuwa siku mbaya sana kwangu sababu kazi ilikuwa nzuri, mbakaleo sijawahi kumuuliza kwanini aliamua kuacha kazi sikuile.

Ajabu nikwamba Mimi na browangu tunapendana kama mapacha lakini sijawahi kumuuliza mbaka Leo.
This time anapambana nje ya mipakahuko.

Bro K, kama upo humu take note ulinihuzunisha sana mwakaule nduguyangu, hahahàaa.
 
Fanya kazi kwanza ndani ya miezi mitatu alafu tafuta sababu ya kuacha now bado mapema sana hawezi kukuelewa hata km unatakuwa una points kutoka duniani hadi mwezin
 
Umeshaamua kuacha kazi, na umeweka bayana...

Sababu utazomwambia huyo aliyekutafutia kazi ishazitaja mwenyewe hapa, basi naye mwambie hivyo hivyo...

Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
 
Wakuu nashukuru sana. Siwapangii Cha kunishauri ila kimsingi nafsi yangu ishafanya maamuzi ya kuacha ila nachohitaji ni jinsi ya kumpa taarifa aliyenitafutia kazi
Kafanye utakavyo. Acha kusumbua watu.

Maamuzi ushafanya unangoja nini. Nenda mwambie. Easy go.

Just text him
 
Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
We ni mpuuzi....
 
Usiache kazi kabla hujapata kazi, resign endapo umepata kazi nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…