Ni kitinda mimba wangu. Amepata kazi Serikalini kwenye Halmashauri moja Mkoani Shinyanga na pia kwenye Shirika linaitwa Good Neighbors Tanzania. Mishahara ni kama inalingana,aende wapi?naomba ushauri wapendwa
Mwambie atazame long run benefits Faida za muda mrefu.
Akiwa Serikalini -Atakuwa amepata kazi ya kudumu Ila Serikalini huwa hakuna changamoto za kukua kifikra, kitaaluma wala kiakili Ila faida inabaki hiyo moja kuwa ni ajira ya kudumu ambayo anaweza kuifanya hadi mwisho.
Kuhusu kwenye hilo shirika- faida yake kuna ukuaji wa kitaaluma, exposure, kukua kiakili na kupata uzoefu ambao utamfanya awe marketable na kuwa na potential.
Hasara - anaweza kuwa redundancy, mkataba kuisha, ajira sio ya kudumu n.k
Ushauri.
Utamtazama kijana wako ikiwa sio hard worker - hana roho ya upambanaji hustler, basi muache aende Serikalini.
Ila ikiwa anajiamini na ni MTU mpambanaji mwenye spirit ya Kutaka mafanikio basi muache aende kwenye mashirika atakutana na watu wenye exposure kubwa watamjenga na baada ya mda atakuwa valuable.
Nadhani huu ushauri nimeelezea utapata A,B,C all the best.