Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Kama anataka easy life na kazi za majungu aende huko serikali. Kama anataka challenge na kukua kikazi aende good neighbours. Mimi nilichaguaga kwenye NGOs sababu nilikiwa nataka kukua kiajira na kufanya kazi na watu tofauti tofauti. Nikatoka hapo nikaenda UN Agency, sasa niko ubalozini. Nikitoka hapa labda niende kwenye development banks eg. WB, AFDB etc.
 
Kama Halmashauri ni Mkataba wa muda mrefu aende Halmashauri kwasababu Good Neighbours wa kawaida sana...ingekua Mashirika makubwa angeacha hiyo ya Halmashauri...Halafu huyo Jamaa yako anasali kwa Mungu yupi anaempa kazi mbili mbili wakati watu wameoga na mafuta ya manabii hawapati hata Kibarua ??
Mungu ni wetu sote huyu huyu aliyempa dogo nafasi 2. Tuendelee kumuamini na kumuomba hata wakati utakapofika.

Ila halmashauri nako changamoto, diwani tu kaishia darasa la ine 😀 anakuazimia unaweza poteza kazi kirahisi tu.
 
Ni kitinda mimba wangu. Amepata kazi Serikalini kwenye Halmashauri moja Mkoani Shinyanga na pia kwenye Shirika linaitwa Good Neighbors Tanzania. Mishahara ni kama inalingana, aende wapi?

Naomba ushauri wapendwa.

Kwani ndoto zake kimaisha ni zipi?

Hizi mambo za kulazimisha kufanya kazi fulani mwisho wake matokeo kuwa na kundi la watu waliopata kazi, lakini si kazi kupata watu...
 
kimsingi hili hali kuhusu, ila kama unahisi kuwa concerned usi influence maamuzi yake bali jaribu kutambua kwanza malengo yake ki-career, ndio itakusaidia wewe kujua anachohitaji kwasasa,,. na kwasababu umeomba ushauri public naweza kusema kijana ana nafasi nzuri ya kukua akiwa Good neighbors, regardless na aina ya placement ila future yake itakuwa poa akipita njia hizo kwahiyo mwache atumie muda huu kukua na kujifunza na kutafuta connection zaidi halmashauri won't serve her/him any good sana sana atakuwa janja janja tu
 
Kama anataka easy life na kazi za majungu aende huko serikali. Kama anataka challenge na kukua kikazi aende good neighbours. Mimi nilichaguaga kwenye NGOs sababu nilikiwa nataka kukua kiajira na kufanya kazi na watu tofauti tofauti. Nikatoka hapo nikaenda UN Agency, sasa niko ubalozini. Nikitoka hapa labda niende kwenye development banks eg. WB, AFDB etc.
Big up mkuu, Kuna wajumbe wanasema Tanzania hakuna the so called carrier growth lakini naamini ipo sana kama mtu anataka kua hivo na akilini kwake akaweka malengo kwamba baada ya muda fulani nataka nifikie level fulani.
 
Aende Halmashauri kuna uhakika wa ajira na maendeleo ya kazi yake.Anaweza kupata fursa za kujiendeleza zaidi kitu ambacho Good neighbours hawatotaka !
 
Mwambie atazame long run benefits Faida za muda mrefu.

Akiwa Serikalini -Atakuwa amepata kazi ya kudumu Ila Serikalini huwa hakuna changamoto za kukua kifikra, kitaaluma wala kiakili Ila faida inabaki hiyo moja kuwa ni ajira ya kudumu ambayo anaweza kuifanya hadi mwisho.

Kuhusu kwenye hilo shirika- faida yake kuna ukuaji wa kitaaluma, exposure, kukua kiakili na kupata uzoefu ambao utamfanya awe marketable na kuwa na potential.

Hasara - anaweza kuwa redundancy, mkataba kuisha, ajira sio ya kudumu n.k

Ushauri.

Utamtazama kijana wako ikiwa sio hard worker - hana roho ya upambanaji hustler, basi muache aende Serikalini.

Ila ikiwa anajiamini na ni MTU mpambanaji mwenye spirit ya Kutaka mafanikio basi muache aende kwenye mashirika atakutana na watu wenye exposure kubwa watamjenga na baada ya mda atakuwa valuable.

Nadhani huu ushauri nimeelezea utapata A,B,C all the best.
Ushauri murua kabisa
 
Ni kitinda mimba wangu. Amepata kazi Serikalini kwenye Halmashauri moja Mkoani Shinyanga na pia kwenye Shirika linaitwa Good Neighbors Tanzania. Mishahara ni kama inalingana, aende wapi?

Naomba ushauri wapendwa.
Uchaguzi ni wake, ila Halmashauri itapendeza zaidi.
 
Kama anataka easy life na kazi za majungu aende huko serikali. Kama anataka challenge na kukua kikazi aende good neighbours. Mimi nilichaguaga kwenye NGOs sababu nilikiwa nataka kukua kiajira na kufanya kazi na watu tofauti tofauti. Nikatoka hapo nikaenda UN Agency, sasa niko ubalozini. Nikitoka hapa labda niende kwenye development banks eg. WB, AFDB etc.
Hata halmashauri kuna
1.Career growth
2.Kukutana na watu wengine(expanding network)
3.Kuna maisha
Lakini yoote hayo yanamsaidia ki local,kibongo na kwa std za tanzania ni kutusua vizuri tu.
Wewe ulichoshinda ni kuwa elements zote hizo unazo hivyo internationally pengine umetusua.
Hivyo inqtegemea tu;anataka aendelee kuwa local/ kibongo zaidi au ki international.Bongo sihamii
 
Kukua ki local. Yaani huko kukua ni kuiba kwa sana. Lakini kwa mshahara hutoboi mzee.
 
UMESOMA KWELI WEWE??? sasa hilo ni swali la kuuliza??? shirika vimkataba uchwaroo hivyoo kesho huna chako ila kama utakomaa ukue zaidi usirudi kuomba ajira tena huku chini haya...ila mkataba ukiisha huna plan bhasi unga halmashauri
 
Back
Top Bottom