Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Ni kitinda mimba wangu. Amepata kazi Serikalini kwenye Halmashauri moja Mkoani Shinyanga na pia kwenye Shirika linaitwa Good Neighbors Tanzania. Mishahara ni kama inalingana, aende wapi?

Naomba ushauri wapendwa.
Good neighbours kwa mshahara gani, wana mishahara ya kijinga. Mwache mtoto aende halmashauri kwenye ajira ya kudumu
 
Kama Halmashauri ni Mkataba wa muda mrefu aende Halmashauri kwasababu Good Neighbours wa kawaida sana...ingekua Mashirika makubwa angeacha hiyo ya Halmashauri...Halafu huyo Jamaa yako anasali kwa Mungu yupi anaempa kazi mbili mbili wakati watu wameoga na mafuta ya manabii hawapati hata Kibarua ??
MUNGU wetu sote
 
Nawashukuru wote mlioshauri,Jana Jumatano nilifanikiwa kumpata Ofisa mmoja anayefanya Kazi kwa sasa katika hilo Shirika la Good Neighbors tukakaa na kuongea kwa kirefu. Kimsingi yeye mwenyewe anahangaika kutafuta kazi sehemu nyingine akidai kwamba hilo Shirika ni la hovyo sana na lenye manyayaso ya kila aina kutoka kwa wenye Shirika ambao ni Wakorea. Kwa kweli amenisimulia mambo mengi sana ya ndani ya hilo Shirika mpaka nikaogopa inakuwaje hayo yote yanatokea na Serikali ipo. Anasema ilifikia kipindi Serikali ilimfukuza nchini PA Mkuu wao kutokana na ufedhuli wake kwa Wazawa na akaletwa Mkuu mwingine Mkorea mwanamke aliyepo mpaka sasa. Suala la manyanyaso kwa wWafanyakazi na kuhamasisha ushoga ni moja ya ajenda kuu za hilo Shirika lakini kwa kivuli cha dini.Kwa kifupi nae anapambana kuondoka hivyo kanishauri mwanangu hata kama ni Halmashauri ya kijijini kusiko na umeme aende na sio kwenye hilo Shirika la Good Neighbors.
Nawashukuru wote mliochangia,kijana ataenda Halmashauri kuripoti,mbarikiwe sana
 
Kuna watu hadi mna pata option za kuchagua kazi [emoji81][emoji81][emoji81] jobless hii feelings mna ionaje
 
Kuna mdau juu kule alipost kwamba hili shirika lina vimelea vya upinde watu wakamcrush sana ila jamaa anathibitisha Hilo.
 
Back
Top Bottom