Nawashukuru wote mlioshauri,Jana Jumatano nilifanikiwa kumpata Ofisa mmoja anayefanya Kazi kwa sasa katika hilo Shirika la Good Neighbors tukakaa na kuongea kwa kirefu. Kimsingi yeye mwenyewe anahangaika kutafuta kazi sehemu nyingine akidai kwamba hilo Shirika ni la hovyo sana na lenye manyayaso ya kila aina kutoka kwa wenye Shirika ambao ni Wakorea. Kwa kweli amenisimulia mambo mengi sana ya ndani ya hilo Shirika mpaka nikaogopa inakuwaje hayo yote yanatokea na Serikali ipo. Anasema ilifikia kipindi Serikali ilimfukuza nchini PA Mkuu wao kutokana na ufedhuli wake kwa Wazawa na akaletwa Mkuu mwingine Mkorea mwanamke aliyepo mpaka sasa. Suala la manyanyaso kwa wWafanyakazi na kuhamasisha ushoga ni moja ya ajenda kuu za hilo Shirika lakini kwa kivuli cha dini.Kwa kifupi nae anapambana kuondoka hivyo kanishauri mwanangu hata kama ni Halmashauri ya kijijini kusiko na umeme aende na sio kwenye hilo Shirika la Good Neighbors.
Nawashukuru wote mliochangia,kijana ataenda Halmashauri kuripoti,mbarikiwe sana