Naomba ushauri: Kila tukikosana ananiambia mimi nina experience ya ndoa, niitumie kuishi nae

Naomba ushauri: Kila tukikosana ananiambia mimi nina experience ya ndoa, niitumie kuishi nae

KusiniKuchele

Senior Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
168
Reaction score
303
Habari za majukumu ndugu zangu? Straight to the mada.
Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Mzaliwa wa Manyara Mwiraqw.

Niliolewa kwa ndoa takatifu ya kanisani mwaka 2020 lakini bahati mbaya mume wangu alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2023. Since then sijawa sawa kihisia namkumbuka sana naishia kulia tu na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Sasa kilichonileta hapa ni kuwaomba ushauri. Kuna kijana mmoja nilisomaga nae chuo kikuu na wote tulikua tunaimba kwaya. But hatukuwahi kuwa kwenye mahusiano. Kuanzia mwaka 2017 akanitongoza kwa lengo la kuanzisha familia but sikua nampenda so sikua tayari kabisa. Ni Msukuma wa Geita.

Baada ya Mr kufariki akarejesha upya majeshi,but bado moyo wangu haukua kwake. Mwaka jana November akapambana mpaka kunihamishia DSM na kunitafutia kazi kampuni X lengo likiwa tuwe karibu. Akaniambia nikaishi kwake na mimi nikasema anyway labda ntajifunza kumpenda na kumsahau marehemu mume wangu.

But kiuhalisia bado moyo wangu umegoma kabisa kumuelewa. Kila tukigombana ananiambia eti kwasababu anajua yeye sio chaguo langu. Sasa hapa niko in dilemma natamani kuondoka niendelee na maisha yangu maana naona sasa hata ule urafiki tu tuliokua nao zamani kama siutaki tena.

Naombeni mnishauri. Wale wenye midomo michafu this isn't the right place ya kutukana. Kiukweli nataka kuwasikia mawazo yenu nifanyaje?
Bado ana kaushamba ka kisukuma,ana hasira na mkono wa kupiga alishanipiga mara moja.

Akinywa pombe ndo kabisa anakua mkali balaa. I am stucked kwakweli mahari naenda this Year December na ndugu zake washapanga but nawaza nisitishe hata hiyo mipango yake.

Kila mkikosana ananiambia mimi nina experience ya ndoa so nitumie hiyo experience kuishi nae 🙆‍♀️
 
WEWE NDIO MWENYE SHIDA, WALA USISINGIZIE HUYO MSUKUMA, UNAISHI NAE MGUU NJE-NDANI HUKU UKIAMBATANISHA NA KUMBU KUMBU YA MAREHEMU MMEO

Anyway:

SIKU ZOTE MTU AKIJA KUOMBA USHAURI WA MAPENZI, WALA HAFATI SOLUTION YA TATIZO LAKE ILA ANAKUJA KUTAFUTA FARAJA.

SASA KWA WW NAVYOKUONA UNASHINDWS KUMPENDA KIKAMILIFU HUYO MTU ILA UPO INSECURE KAMA UKIMUACHA SASA hii SITUATION YAKE HADI INAKUUMIZA AKILI KUPELEKEA KUJA HUMU KUTAKA FARAJA TU.

ANYWAY, FANYA HIVI... MAAMUZI YA MAPENZI NI YAKO maana moyo ulipoo katika mapenzi unakuwa kipofu hadi pale macho yatakapo ona ndio utaweza fanya uamuzi binafsi ambao ndio huwa the best of the best.
 
Ondoka tu,utamuumiza huyo ...
Ana busara ila Hana bahati nawe...mwambie aoe anayemlilia maana najua naye yupo anayeteseka juu yake....but why moyo umegoma bado ukakubali akutendee mema yote hayo?
Anyways,kama itawezekana tuliza kichwa tafakari majibu sahihi unayo mwenyewe
 
SIKU ZOTE MTU AKIJA KUOMBA USHAURI WA MAPENZI, WALA HAFATI SOLUTION YA TATIZO LAKE ILA ANAKUJA KUTAFUTA FARAJA.

SASA KWA WW NAVYOKUONA UNAMPENDA HUYO MTU ILA UPO INSECURE Kutokana NA SITUATION YAKE HADI INAKUUMIZA AKILI KUPELEKEA KUJA HUMU KUTAKA FARAJA TU.

ANYWAY, FANYA HIVI... MAAMUZI YA MAPENZI NI YAKO maana moyo ulipoo katika mapenzi unakuwa kipofu hadi pale macho yatakapo ona ndio utaweza fanya uamuzi binafsi ambao ndio huwa the best of the best.
mkuu naona umefunga uzi hapa umemaliza kila kitu kiufupi kama yeye hamtaki basi aondoke amuache tu, kama hataki basi abaki aishi nae huu ndio ushauri wa kufanya maana naona kuna kitu hakipo sawa kwa mtoa uzi
 
Can't date na a married man.
Kwa ninavyofahamu jibu unalozuri tu ila unataka namna ya kulihalalisha
Mi nashauri muache ila chonde chonde usianze kusumbua ndoa za watu just be calm nunua dildo halitakusumbua
 
mkuu naona umefunga uzi hapa umemaliza kila kitu kiufupi kama yeye hamtaki basi aondoke amuache tu, kama hataki basi abaki aishi nae huu ndio ushauri wa kufanya maana naona kuna kitu hakipo sawa kwa mtoa uzi
Hakika mkuu

Hakunaga ushauri wa mapenzi

Kwa maana mapenzi yalianzia moyoni mwako basi yataishia moyoni mwako

Basi tu kama ameamua kuishi nae kisela huyu msukuma ila naungana na wewe kuwa huyu mtoa mada ndio mwenye shida
 
Kuanzia mwaka 2017 akanitongoza kwa lengo la kuanzisha familia but sikua nampenda so sikua tayari kabisa. Ni Msukuma wa Geita.
Baada ya Mr kufariki akarejesha upya majeshi,but bado moyo wangu haukua kwake. Mwaka jana November akapambana mpaka kunihamishia DSM na kunitafutia kazi kampuni X lengo likiwa tuwe karibu. Akaniambia nikaishi kwake na mimi nikasema anyway labda ntajifunza kumpenda na kumsahau marehemu mume wangu. But kiuhalisia bado moyo wangu umegoma
kwanza, Pole

pili, wasukuma dah ndugu zangu mna tatizo gani

tatu, humpendi

nne, humpendi tena

tano, kakufanyia yote hayo bado humpendi

sita, humpendi moyo umegoma

saba, humpendi unataka tukushauri umpende mtu hashauriwi kupenda

nane, humpendi unamchora

tisa, dah bado tu humpendi

kumi, nasikitika humpendi na hutompenda hata kama mtakuwa wapenzi
 
hii ndo shida ya wanawake, mtu kakuangaikia kote uko wewe unapokea tu ila moyoni haupo naye, kwa hyo ulidhani yy ni malaika kwa hyo maangaiko yote aliyokuangaikia katumwa na mungu au? mkuu achanaga na kupokea vya watu, hakuna cha bure hapa duniani, utakuja kufa bure, kama humpendi mtu just mwambie ukwel, haya mambo ya ngoja nimtumie ili yangu yanyooke ndo yanawatokeaga puani.
 
Sijui kwanini hatupendi kusikiliza mioyo yetu...

Moyo wako umeshaongea haumpendi...

Fuata moyo wako...
mtoa mada naona anashida sehemu nyuma ya pazia haja twambia fact, haps anatafuta sijui nini yani kama haeleweki
 
Back
Top Bottom