Habari za majukumu ndugu zangu? Straight to the mada.
Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Mzaliwa wa Manyara Mwiraqw.
Niliolewa kwa ndoa takatifu ya kanisani mwaka 2020 lakini bahati mbaya mume wangu alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2023. Since then sijawa sawa kihisia namkumbuka sana naishia kulia tu na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.
Sasa kilichonileta hapa ni kuwaomba ushauri. Kuna kijana mmoja nilisomaga nae chuo kikuu na wote tulikua tunaimba kwaya. But hatukuwahi kuwa kwenye mahusiano. Kuanzia mwaka 2017 akanitongoza kwa lengo la kuanzisha familia but sikua nampenda so sikua tayari kabisa. Ni Msukuma wa Geita.
Baada ya Mr kufariki akarejesha upya majeshi,but bado moyo wangu haukua kwake. Mwaka jana November akapambana mpaka kunihamishia DSM na kunitafutia kazi kampuni X lengo likiwa tuwe karibu. Akaniambia nikaishi kwake na mimi nikasema anyway labda ntajifunza kumpenda na kumsahau marehemu mume wangu. But kiuhalisia bado moyo wangu umegoma kabisa kumuelewa. Kila tukigombana ananiambia eti kwasababu anajua yeye sio chaguo langu. Sasa hapa niko in dilemma natamani kuondoka niendelee na maisha yangu maana naona sasa hata ule urafiki tu tuliokua nao zamani kama siutaki tena.
Naombeni mnishauri. Wale wenye midomo michafu this isn't the right place ya kutukana. Kiukweli nataka kuwasikia mawazo yenu nifanyaje?
Bado ana kaushamba ka kisukuma,ana hasira na mkono wa kupiga alishanipiga mara moja. Akinywa pombe ndo kabisa anakua mkali balaa. I am stucked kwakweli mahari naenda this Year December na ndugu zake washapanga but nawaza nisitishe hata hiyo mipango yake. Kila mkikosana ananiambia mimi nina experience ya ndoa so nitumie hiyo experience kuishi nae 🙆♀️
ni muhimu kufahamu kwamba ndo sio lelemama na ndoa haijaribiwi,
mistake moja tu itakufanya ujute maisha yako yote humu duniani.
but my lady,
kuna red flag arlerts nyingi sana uanziaona kabisa kwa huyo muungwana, kwanza hauko ready nae na kuishi nae, hauko happy awe mumeo, hauna mapenzi ya dhati kwake, huna hisia nae, but pia umeeleza kwamba the gentleman anamkono mwepesi, na alishakushushia kipigo cha mbwa koko, mangumi na makofi, but wewe siju ni kwasababu una hofu na huna hakika na maisha ya kua single, unang'ang'ana tu kumkubalia mambo ambayo kwa maelezo yako mwenyewe ni mazito na kwamba humkubali huyo kijana.
Tafadhali usimpotezee muda kijana wa watu, na kabisa epuka kumuhadaa kwa kujilazimisha kumpenda.
Halafu my lady,
huoni kwamba unajipa mzigo na matatizo makubwa wewe mwenyewe maisha yako yote? utaishije na mtu usiempenda? si unaweza kuingia kwenye records ya ndoa zilizodumu muda mfupi sasa? Maana kwasababu moja hampendi mwingine kwa dhati, baadae maweza hata kuuna sasa kwa chuki kati yenu...
ni muhimu sana kumshirikisha Mungu katika kuamua uelekeo wa maisha yako ya ndoa takatifu.
Jitakase nafsi yako vyema, fungua maskio ya moyo wako ili unapomuomba Mungu akuonyeshe njia kwenye mkwamo huo na jaribu hilo, iwe rahisi kuskia na kutambua sauti ya wito wa Mungu katika utume wa ndoa takatifu ya amani, furaha na upendo unayoitamani baada ya mumeo kuaga dunia kwa ajali mbaya.
Usiingie katika ndoa TAKATIFU usipokua na uhakika wa amani, upendo, furaha na mapenzi ya dhati ya kiMungu. Hayo yatakua ni maigizo tu my lady. Mapenzi na ndoa havilazimishwi na ikiwa ni hivyo itakua ni ubakaji
Mungu akubariiki sana
