Naomba ushauri kuhusu biashara Spare za Pikipiki

Hongera kwa UTHUBUTU... Nadhani mpaka sasa utakua na uzoefu walau wa yule mtu anaetaka kuanza biashara hiyo, naomba ushare kwenye haya:

1: Ulianza kudeal na Uuzaji wa vipuri vya Kampuni zipi za pikipiki?(zitaje kwa majina)

2: Je, Ulianza kuuza spea na oil kwa pamoja hapo mwanzo? Ni spare zipi na/au oil zipi ulianza nazo?(zitaje kwa majina)

3: Chimbo ulilokuaunatoa/unalotoa spea na/au oil? Ni lipi

4: Gharama TRA zimekaaje?
AHSANTE...
Naomba kuwasilisha.
 
Personal nilianza na duka kubwa la urembo wa magari kwa mtaji wa 15M.

Mungu akisaidia by feb-march 2023, ntaongeza duka la spare na urembo wa Bodaboda/bajaji.

Mungu ni mwema business hizi hazimtupi mtu.
Nitaomba mawasiliano ya mahali unapochukua urembo wa pikipiki
 
Kiongozi samahani kwani spare kwa kuanzia huwezi kuanza bila kuweka fundi?

Bila fundi uongo kama unauza rejareja, mana boda hawez nunua spea akapeleka kwa fundi ambaye yuko kijiwe kingine ambako nako kunauza spare
Muhim kwa reja kuwa na fundi ili kurahisisha mzunguko,
 

Natumai biashara yako imetimiza mwaka mmoja sasa hongera sana.

Vipi maendeleo kiongozi...?
 

Mkishakatana kwenye Kodi kidogo kidogo baada ya hapo frame inakuwa yake ama...?
 
Bila fundi uongo kama unauza rejareja, mana boda hawez nunua spea akapeleka kwa fundi ambaye yuko kijiwe kingine ambako nako kunauza spare
Muhim kwa reja kuwa na fundi ili kurahisisha mzunguko,
But mm nataka niwe na ofisi kwanza nione inakuaje natumai sitochelewa kumpata fundi
 
Utajichelewesha hivyo ndugu! Jitahid uwe na fundi ili matatizo na hamu zao wateja wamalize hapo hapo!...
Nikitaka fundi nampataje maana wengi ni wapigaji akiona tena unashida nae sana anakua na kibri
 
Nikitaka fundi nampataje maana wengi ni wapigaji akiona tena unashida nae sana anakua na kibri
Unapotaka cha uvunguni sharti uiname!.. kwa maana wakat mwingine unaweza hata kumpa kiasi flani cha fedha kumtoa sehemu moja fundi kwenda nyingine. Na sio kuwa wanaringa ila eneo utakalomkuta kumbuka anakuwa na wateja wake hivyo basi unavyomuamisha atakuwa anakwenda kuanza maisha mapya kwahyo ndiyo maana wengi wao hiko wanakikwepa! Mfano mim fundi wangu kumtoa sehemu aliyokuwepo na kumleta mazingira yangu ilinibid nimpangie hadi chumba kwa miez 3 na posho kidogo nilimpa yote hiyo kujitengenezea mazingira!... Nadhan nimekujibu!...
 
Mkishakatana kwenye Kodi kidogo kidogo baada ya hapo frame inakuwa yake ama...?
Ndiyo kwa maana kiwanja ni chake . Kinachofanyika tu ni kwamba gharama ya kujenga frame inatoka kwangu kwa kuwa yeye kwa sasa hana pesa ya kujenga . Hivyo basi gharama inayotumika kujenga ni sawa na gharama ambayo nimelipia kodi kwa muda flan au miaka kadhaa lkn tumetengeneza mkataba wa makubaliano hayo kwa wanasheria maana huwezi jua Kwa badae mmoja wetu akaingia tamaa au mmoja wetu akatangulia mbele za haki basi familia zetu zibaki zikitambua hilo kupitia mkataba. Pia kwa kuwa itachukua muda mrefu pasipo kupokea yeye kodi basi tulikubaliana kodi ya frame nusu itakuwa inapunguza deni la kujenga alafu nusu anapokea.

Baada ya muda wa makubaliano ukishaisha nitaanza kulipa kodi kama kawaida na yawezekana pia ikapanda kulingana na thaman ya muda huo.
 

Tuchukulie umejenga kwa milioni moja hiko chumba kimoja, unatoa laki tano unampa yeye it means si ni milioni moja na nusu au sijakuelewa vizuri kiongozi...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…