Mama ya vifaa nimeumia, nimemuuliza sana kagoma kabisa kunikubalia, na michezo yote waliyocheza na wale mabinti, na kiwanja, bado hakubali,
Sasa toka kipindi tumepokea pesa ya kwanza, kulikuwa na ubishani mkubwa sana kuhusu tununue wapi kiwanja,
Mimi ushauri kiwanja kinunuliwe upande wa njia ya kwenda kwangu au mbele ya kwangu, na kuna eneo ambalo nilililenga, lina potential kwa siku za baadaye, na pili mwendo wa kwenda kwake kusema kweli ulikuwa ni mrefu, wakati nimempata nilikuwa maeneo ya mjini kati, na kwenda kwake ilikuwa kama km 20,
Baada ya mimi kuhamia makazi mapya
Mwendo ukaongezeka ikawa km 37,
Nikitoka kwake saa moja usiku nafika kwangu sio chini ya 4.5 au saa tano foleni ikikaza,
Lakini yeye aligoma kabisa,
Kumbuka pesa ameshika yeye!
Eneo nililiopendkeza huku upande wangu ni kama km 10 kumi, nikichukua boda na dala dala ni nusu saa tu nipo ndani mwangu,
Yeye alikuwa akipendekeza eneo lake ni km 20 zaidi kwenda opposite direction!
Yaani alipo hapo kwenda ndani zaidi huko,
Kutoka huko sasa mpaka kwangu ni km 52,
Sasa jamani hii ni kitu gani tena?
Kusema kweli sasa hapo, nilisema liwalo na liwe, nilishika nikataka kupiga, baadaye nikaacha, nikamwambia naomba nipe pesa zangu, na kuachana tuachane, nitakugawia pesa ukajenge huko kwenu,
Watoto wakalia sana wakisema baba usituache,
Nilivyosikia sauti hizo nilimwachia baadaye nikaona nalia mwenyewe tu, huku natetrmeka mbaya sana,
Baadaye nikamsikia mtoto mmoja anamuuliza Kwani mama wewe we ukoje,
Siku nyingine tutamwacha baba akupige,