Naomba ushauri: Mke wangu aliondoka na mtoto sifahamu anapoishi sasa, hataki kumleta mtoto nimuone

USHAURI DUME!! Kaa nae chini kwa mara ya mwisho mueleze unahitaji jibu moja kua atakupatia muda na mtoto au sio tena fanya hivo huku ukirekodi mazungumzo chochote atakachokwambia kihifadhi! Kwenye frash au popote! Akikataa achana nae na usiulize tena futa mawasiliano kila kitu vaa moyo chuma kbs! Usimtafute hata kwa bahati mbaya! Ishi maisha yako mtoto akikua atakutafuta akikuuliza why ulikua kimya mpe ushahidi wa juhudi ulizofanya! Mwaka 2006 ilinitokea nilijitahidi bibi mtu akazingua hapo mtoto alikua na miaka sita tu nikakata mguu no sim no kamsalimie mtoto alikuja kunitafuta baada ya usumbufu mkubwa nikashika usukani kumsomesha hadi saaa anamaliza form six! Alipokua form two akaniuliza ilikuaje ukaniacha kwa mama nikamweleza bibi yako alileta upuuzi na mie mwanaume sioangiwi cha kufanya kwa mtoto wangu! Akanielewa hadi leo tupo peace!
Asante kwa ushauri mzuri na nitaufanyia kazi mkuu.
 
Duuuuh ngoja nikafuturu kaka, nitarudi kukupa ushauri ila pole sana.
 
Punguza hasira kwanza boss yule mtoto ni damu yako kumzila mtoto sawa na kujikana mwenyewe.

Fanya taratibu za kisheria kutatua swala hilo kama ngazi ya family kwa pande zote mbili ya mwanamke na kwenu mmeshindwa kutatua.
 
Pole sana jamaa yetu... Muombe sana Mungu ili uchukue maamuzi sahihi..
 
Habari za weekend wana JF

Nilioa mwaka 2016, na tukabahatika kupata mtoto 1 wa kiume mwaka 2017 ambae ana miaka 4 kwa sasa na sehemu ya makazi yetu ni hapa Mbeya. Mapema 2020 mke wangu alianza kubadilika sana baada ya yeye kupata biashara nzuri ukilinganisha na ile aliyokuwa anafanya mwanzo.

Katika mabadiliko yake, alihitaji na yeye kwenda kuishi maisha ya peke ake. Nilitafuta suluhu sana za kuweka ndoa sawa ila hakukuwa na mafanikio na hatimae mwezi wa 6 mwaka huo 2020 aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake pamoja na mtoto.

Wakat anaondoka hakusema anapoenda kukaa na mtoto na mpaka sasa sipajui anapokaa na mtoto japo yupo Mbeya hapa hapa. Hayuko tayari kunambia anapokaa mbali na kuhitaji kupajua kwa ajili ya kupata access ya kumuona mtoto wangu. Kila nikiomba aniletee au nifate mtoto nikae nae hata weekend analeta sababu na anaweza kukuahidi kumleta ila ikifika muda analeta sababu na hutomuona tena.

Mtoto akiumwa siambiwi mapema, ila nakuja kuambiwa anapokuwa amelazwa hospital na ndo hapo namuona mwanangu. Tangu aondoke kwangu, mtoto amelazwa hospital mara 3 na mara zote hizo nakuja kuambiwa kashalazwa, naenda kumuona na kumhudumia mpaka anaruhusiwa, akisharuhusiwa tu ndo humuoni tena. Nimeshajaribu kuongea nae juu ya umuhimu wa sisi kumpa malezi ya wazazi wote hata kama hatuishi na mtoto pamoja, kumpa mtoto nafasi ya kuwa ananiona au ananitembelea lakini hakuna matokeo chanya. Cha kusikitisha, mtoto anamruhusu kuwatembelea marafiki zake tena umbali mrefu na hata kwa ndugu zake mtoto anaenda hata kukaa baadhi ya siku ila siyo kumruhusu kuja kwangu au mm kumtembelea mtoto.

Sasa kama mwanaume mwenye hisia na moyo usio wa chuma na mwenye maumivu, nimechoka na haya maisha ya kuishi na mtoto wangu kwa kumuona kila anapolazwa hospital. Nahitaji kufanya maamuzi magumu.

Akilini mwangu kwa sasa nna mawazo mawili ambayo nahitaji mojawapo kufanyia kazi, moja ni kumsusia mtoto kabisa abaki nae milele au niende ngazi za sheria ambazo wataweza kunisaidia hili swala kwa kuzingatia sheria ya malezi ya mtoto hasa pale wazazi wanapotengana.

Naomba mawazo yenu ndugu zangu wenye uzoefu na changamoto hizi angalau nijue naamua kwenda mbele na wazo gani hapo.

Nitapitia ushauri wenu kwa ajili ya msaada.
Mwenye uhakika kuwa mtoto ni wako ni huyo mwanamke. Angalia usijekuwa unahangaika na mtoto wa mwenzio.

Kama ulioa kwa taratibu rasmi anzia hapo. Ita waliuhusika na weka nia yako wazi ya kumwachia majukumu ya kulea mtoto kwa sababu hizo ulizozitaja. Siku akiwa tayari kushirikiana malezi utakuwa tayari. Kwa sasa endelea na maisha mengine. Ina maumivu lakini unaweza kuja kuumia zaidi mbeleni ukiambiwa mtoto sio wako wakati kuna ghalama umeingia.

Lakini pia ukiamua kumsaidia mtoto msaidie kama unatoa sadaka hata likitokea lolote usijeumia.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Habari za weekend wana JF

Nilioa mwaka 2016, na tukabahatika kupata mtoto 1 wa kiume mwaka 2017 ambae ana miaka 4 kwa sasa na sehemu ya makazi yetu ni hapa Mbeya. Mapema 2020 mke wangu alianza kubadilika sana baada ya yeye kupata biashara nzuri ukilinganisha na ile aliyokuwa anafanya mwanzo.

Katika mabadiliko yake, alihitaji na yeye kwenda kuishi maisha ya peke ake. Nilitafuta suluhu sana za kuweka ndoa sawa ila hakukuwa na mafanikio na hatimae mwezi wa 6 mwaka huo 2020 aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake pamoja na mtoto.

Wakat anaondoka hakusema anapoenda kukaa na mtoto na mpaka sasa sipajui anapokaa na mtoto japo yupo Mbeya hapa hapa. Hayuko tayari kunambia anapokaa mbali na kuhitaji kupajua kwa ajili ya kupata access ya kumuona mtoto wangu. Kila nikiomba aniletee au nifate mtoto nikae nae hata weekend analeta sababu na anaweza kukuahidi kumleta ila ikifika muda analeta sababu na hutomuona tena.

Mtoto akiumwa siambiwi mapema, ila nakuja kuambiwa anapokuwa amelazwa hospital na ndo hapo namuona mwanangu. Tangu aondoke kwangu, mtoto amelazwa hospital mara 3 na mara zote hizo nakuja kuambiwa kashalazwa, naenda kumuona na kumhudumia mpaka anaruhusiwa, akisharuhusiwa tu ndo humuoni tena. Nimeshajaribu kuongea nae juu ya umuhimu wa sisi kumpa malezi ya wazazi wote hata kama hatuishi na mtoto pamoja, kumpa mtoto nafasi ya kuwa ananiona au ananitembelea lakini hakuna matokeo chanya. Cha kusikitisha, mtoto anamruhusu kuwatembelea marafiki zake tena umbali mrefu na hata kwa ndugu zake mtoto anaenda hata kukaa baadhi ya siku ila siyo kumruhusu kuja kwangu au mm kumtembelea mtoto.

Sasa kama mwanaume mwenye hisia na moyo usio wa chuma na mwenye maumivu, nimechoka na haya maisha ya kuishi na mtoto wangu kwa kumuona kila anapolazwa hospital. Nahitaji kufanya maamuzi magumu.

Akilini mwangu kwa sasa nna mawazo mawili ambayo nahitaji mojawapo kufanyia kazi, moja ni kumsusia mtoto kabisa abaki nae milele au niende ngazi za sheria ambazo wataweza kunisaidia hili swala kwa kuzingatia sheria ya malezi ya mtoto hasa pale wazazi wanapotengana.

Naomba mawazo yenu ndugu zangu wenye uzoefu na changamoto hizi angalau nijue naamua kwenda mbele na wazo gani hapo.

Nitapitia ushauri wenu kwa ajili ya msaada.
Kwani huyo mzaz mwenzako hana wazaz na ndugu zake?
 
Hapa tumesikia ya upande mmoja, kwa niwajuavyo wanaume na jinsi wanawake wengi wanavyopitia mateso kwenye ndoa sikuhizi nashindwa kushawishika na maelezo yako i wish ningemsikia pia mkeo ana yapi ya kutuambia kwasababu hicho kinachoendelea sio cha kawaida.

Wanawake wengi hata ambao hawajaolewa ila wamezaa tu their dream and wish ni kuona watoto wanakuwa na mahusiano ya karibu na baba zao na hilo likikosekana huwa wanasononeka sana na huwa wanahangaika kutafuta namna ya kutengeneza ukaribu wa watoto wao na baba zao hata kama wao wazazi hawapatani. Umemtenda nini huyu dada?
 
Mimi naona ushirikishe wazazi au ndugu ikishindikana uende kwenye vyombo vya sheria, akikana mtoto sio wako fuata taratibu za kujua mtoto ni wako au la

(Maana wengi wakiambiwa mtoto sio wako wanasusa mazima) pambana ujue km mtoto ni wako au siyo, ikifahamika mtoto ni wako utamdai naww upatiwe haki yako ya kukaa nae, ikiwa umefahamu mtoto sio wako mfungulie mashtaka huyo mwanamke kwa kukuaminisha wewe huyo ni mtoto wako na gharama zote ulizotumia katika malezi ya huyo mtoto utayadai
 
Pole sana brother! I am at more/less same situation, nilichofanya mm nmeamua kupotezea kila k2,siulizi habar za mtoto wala mamake. It hurts,inahitaj moyo wa chuma. Binafsi,naamin kama mtoto n wangu kweli kuna siku atakuja nitafuta.

NB:ingefaa sana tungeskia upande wa pili wa habar kabla ya kujaji kuhusu uyo mwanamke
 
Katika mabadiliko yake, alihitaji na yeye kwenda kuishi maisha ya peke ake. Nilitafuta suluhu sana za kuweka ndoa sawa ila hakukuwa na mafanikio na hatimae mwezi wa 6 mwaka huo 2020 aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake pamoja na mtoto.
Hii ni dalili ya kukuchoka

Wakat anaondoka hakusema anapoenda kukaa na mtoto na mpaka sasa sipajui anapokaa na mtoto japo yupo Mbeya hapa hapa. Hayuko tayari kunambia anapokaa mbali na kuhitaji kupajua kwa ajili ya kupata access ya kumuona mtoto wangu. Kila nikiomba aniletee au nifate mtoto nikae nae hata weekend analeta sababu na anaweza kukuahidi kumleta ila ikifika muda analeta sababu na hutomuona tena.
Hii inaonesha kuna uwezekano anaishi na mtu mwingne(mwanaume) sasa anaogopa usije gundua wenda kamdanganya huyo mtu kuwa yeye ni single mother(aliisha achana na baba wa mtoto au uliisha kufa) ama huyu mtoto sio wako.

Huyo sio mwanamke kabsa chunguza mwisho wa siku utapata ukwel
 
Walishashirikishwa ila hawakusema chchote juu ya hilo la kuondoka na kuhsu mtoto pia. Inshort walitupilia mbali.
Bas wao wanajua ukwel sasa wanakuona ww bwege. Hapo ni ww pia kuwaona wapumbavu achana kujiumiza kuwafikiria wala kupoteza mda wa kumtafta anza upya ikibidi oa kama utapata alietulia
 
Damu haipotei... Acha karma ifanye kazi yake, tafuta mke upate mtoto mwingine.. We ng'ang'ana tu ipo siku utajua mwanamke mpumbavu huua ili amfurahishe hawara.
Fuata ushauri huo, mke mwelezi usimfiche, pia jiandae rudishiwa mtoto ukisha oa eti unakomolowe
 
Si ajabu mtoto si wako Mkuu. DNA muhimu kama utaweza.
Habari za weekend wana JF

Nilioa mwaka 2016, na tukabahatika kupata mtoto 1 wa kiume mwaka 2017 ambae ana miaka 4 kwa sasa na sehemu ya makazi yetu ni hapa Mbeya. Mapema 2020 mke wangu alianza kubadilika sana baada ya yeye kupata biashara nzuri ukilinganisha na ile aliyokuwa anafanya mwanzo.

Katika mabadiliko yake, alihitaji na yeye kwenda kuishi maisha ya peke ake. Nilitafuta suluhu sana za kuweka ndoa sawa ila hakukuwa na mafanikio na hatimae mwezi wa 6 mwaka huo 2020 aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake pamoja na mtoto.

Wakat anaondoka hakusema anapoenda kukaa na mtoto na mpaka sasa sipajui anapokaa na mtoto japo yupo Mbeya hapa hapa. Hayuko tayari kunambia anapokaa mbali na kuhitaji kupajua kwa ajili ya kupata access ya kumuona mtoto wangu. Kila nikiomba aniletee au nifate mtoto nikae nae hata weekend analeta sababu na anaweza kukuahidi kumleta ila ikifika muda analeta sababu na hutomuona tena.

Mtoto akiumwa siambiwi mapema, ila nakuja kuambiwa anapokuwa amelazwa hospital na ndo hapo namuona mwanangu. Tangu aondoke kwangu, mtoto amelazwa hospital mara 3 na mara zote hizo nakuja kuambiwa kashalazwa, naenda kumuona na kumhudumia mpaka anaruhusiwa, akisharuhusiwa tu ndo humuoni tena. Nimeshajaribu kuongea nae juu ya umuhimu wa sisi kumpa malezi ya wazazi wote hata kama hatuishi na mtoto pamoja, kumpa mtoto nafasi ya kuwa ananiona au ananitembelea lakini hakuna matokeo chanya. Cha kusikitisha, mtoto anamruhusu kuwatembelea marafiki zake tena umbali mrefu na hata kwa ndugu zake mtoto anaenda hata kukaa baadhi ya siku ila siyo kumruhusu kuja kwangu au mm kumtembelea mtoto.

Sasa kama mwanaume mwenye hisia na moyo usio wa chuma na mwenye maumivu, nimechoka na haya maisha ya kuishi na mtoto wangu kwa kumuona kila anapolazwa hospital. Nahitaji kufanya maamuzi magumu.

Akilini mwangu kwa sasa nna mawazo mawili ambayo nahitaji mojawapo kufanyia kazi, moja ni kumsusia mtoto kabisa abaki nae milele au niende ngazi za sheria ambazo wataweza kunisaidia hili swala kwa kuzingatia sheria ya malezi ya mtoto hasa pale wazazi wanapotengana.

Naomba mawazo yenu ndugu zangu wenye uzoefu na changamoto hizi angalau nijue naamua kwenda mbele na wazo gani hapo.

Nitapitia ushauri wenu kwa ajili ya msaada.
 
Daah mama yangu pia alikuwa na msimamo kama wa mkeo kumzuia Baba asinichukue matokeo yake akaharibu maisha yangu.

Baba mpaka leo inamuuma sana na hataki hata kunisaidia.
 
Aisee pole sana mkuu........hapo kwanza kabisa mke umeshamkosa na sikushauri kum'bembeleza arudi nyumbani tena ila ukitaka ni sawa pia kwa maamuzi yako binafsi

Ila swala la mtoto ndio la msingi na pia inawezekana mtoto sio wako au inawezekana ni wako ila tayari mtoto ana baba wawili hvyo kitendo cha kuruhusu kuja kwako baba mwenzio huko atajua Kua Kuna mwenzake kitu ambacho mkeo hataki

Kikubwa usifanye fujo sogea ngazi ya sheria kama unataka mtoto watajua namna ya kukusaidia, ila pia ukijiweza kimfuko pima DNA ili usijipachike ubaba kwa kulazimisha na ukute mtoto sio wako
 
Kachek DNA kuna uwezekano 97% mtoto sio wako hizo 3% zilizobaki tunampa mwanamke wako benefit of the doubt...
 
Back
Top Bottom