Naomba ushauri nifanye nini katika hali kama hii, nataka kucheza fair

Naomba ushauri nifanye nini katika hali kama hii, nataka kucheza fair

Kwa wanaume tu.
Sio lazima kila jambo la kulianika (kuliweka wazi kwa kila mtu) jifunzeni kuwa na SIRI ZA MAISHA.
Tuna ndoa na tuna watoto nje ya ndoa na wife hajui na maisha yanasonga kwa amani na familia zinaishi vizuri.
Zingatia tu mtoto aishi, avae, asome pia uhakika wa maisha nunua viwanja viwili vitatu andika majina yake, anzisha duka kwa jina lake pia.

Kwa ambao bado mnajitafuta kimaisha jitahidi sana usiwape mimba wanawake wengi na huna Hela na ukiwa nazo mkeo wa ndoa hawezi kukuacha sababu una mtoto nje ya ndoa.
 
Habari yenu ndugu zangu.

Niende kwenye mada.

Mimi nina mchumba wangu toka mwaka juzi tupo kwenye uchumba na mwakani tumepanga kufunga ndoa.

Sasa mwaka jana mwezi wa 6 nilipata transfer nikahamia mkoa mwingine (Kaskazini hukuhuku).

Sikuweza kuhama na mchumba wangu kwasababu hatukuwa tunaishi pamoja hata hapo awali na alikuwa na mishe zake anafanya kwahyo nikamuacha huko mkoani (nilipohamia ni mkoa jirani tu na alipo yeye).

Sasa mwezi wa 9 nikakutana na binti mmoja katika mazingira ambayo yalifanya tubadilishane namba na hatimaye tukaanza kuwasiliana na kujikita tupo kwenye mahusiano ya rasharasha.
Kadri siku zilivokuwa zinaenda mapenzi yakaanza kukolea.

Wiki iliyopita alianza kunambia anajisikia vibaya mara kichwa mara kichefu chefu mara tumbo.

Majuzi kaenda kupima kaambiwa ana mimba ya wiki mbili kasoro na highly probably ni mimba yangu kwahesabu nilizopiga na hata hivo binti hana mambo mengi.

Nipo nawaza mchumba wangu itakuwaje, ananipenda nampenda hajanikosea anajua kabisa ni lazima nitamuoa na tayari huku binti naye nishampa ujauzito na yeye ananipenda sana tu sielewi cha kufanya.

Binti kashaanza kusema mimba hatoi na ofcourse na mimi sitaki aitoe kibaya zaidi anasema anahitaji kupajua kwetu na kujua ndugu zangu in case ikitokea lolote basi ajue anaanzia wapi.

Huyu mchumba wangu simu kila mara sijui kanusa nini yani simu na meseji ni almost kila muda na huyu Binti nilichokosea sikumwambia kwamba nina mchumba na tuna mpango wa kuja kufunga ndoa.

Plz naomba ushauri nifanye nini katika hali kama hii, nataka kucheza fair.

View attachment 3194170
Mpka anakubebea mimba we oa huyo na uleee mtoto wako maisha yaende hapo
 
Baki na unaempenda, mwingine mwambie hali halisi.
Demu nae anapataje mimba kindezi tu bila mipango bila shaka aliitaka hiyo na kaipata na ww utakiona cha moto. Kwa jinsi ulivyoandika wewe no kijana rojorojo lazima hizo pisi zikuendee kwa sangoma ww, utajuta.
 
Chief jaribu hivi.

Mwambie ukweli huyo mwanamke kuwa una mchumba wako wa siku nyingi, na ulipanga kuoana nae ila sababu ya umbali ukajikuta unaanza mahusiano mengine yaliyopelekea yeye kubeba mimba.

Ukimaliza huko, kama mchepuko kaelewa somo, fanya chapu muoe mchumba wako wa mwanzo( ila tu kama unampenda ,usioe kwa kumuonea huruma muda uliompotezea).

Mkishaoana ndio badae uje kumwambia ukweli wote kua una mtoto ila mchepuko ulikuficha kuhusu hiyo mimba, so now mchepuko kaniambia kuhusu mtoto wangu nmeona sio mbya nikakuomba msamaha.



Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Nashukuru sana
 
Back
Top Bottom