Naomba Ushauri, nimefilisika baada ya kuoa!

Je, upi uamuzi wako kwenye ndoa?


  • Total voters
    53
Apo kutoboa ni ngumu aisee, mke wa namna gani huyo ulieoa.

Nyie ndo huwa mnaoa matako na sio mtu
Kaka yangu alioa mke kutoka kisini alikuwa na magari mengi lakini baada ya mke kufunga tu ndoa akawa anauza yale magari akidai yeye ni mke wa ndoa hapaswi kuulizwa kwanini anafanya hivyo
 
Ukiona hayo yanakukuta hukujioanga mzee usilaumu watu kwa uzembe wako. Nani alikuambia uoe goli kipa wakati una maisha duni yaani hela ya kula unaipigia hesabu hadi kwa mwaka asee hebu tafuta uhuru wa kifedha dogo alafu kama huwezi kukaa na mwanamke sio lazima ishi kama ulivyozoea ila muda ukishakutupa mkono utafute libibi ulioe muanze maisha
 
Ila hata picha ulioweka kwenye profile yako inanitia mashaka sana inaonekana kuna mengi huyawezi sio kukaa tu na mwanamke
 
Labda hujaoa ukaona jinsi pesa zinavyopotea kwenye mambo ya kifamilia, Bill Gates yupo single kwani kakosa pesa?
 
Labda hujaoa ukaona jinsi pesa zinavyopotea kwenye mambo ya kifamilia, Bill Gates yupo single kwani kakosa pesa?
Na ww kuwa biligeti sasa. Ukijua kwamba maisha ni ww na yanaanza na ww swala la kulalamika hela kutumika kwenye familia Utaacha gate ana familia na anagawa kwa maskini sasa ww familia tu unalia je utaweza kuwapa wenye uhitaji. Muda mwingine tusiendekeze roho mbaya
 
Sio roho mbaya tunapoteza sana hela kwenye familia tena mambo ya kijinga kumbe pesa hizo tungepanua kazi zetu
 
Sio roho mbaya tunapoteza sana hela kwenye familia tena mambo ya kijinga kumbe pesa hizo tungepanua kazi zetu
Kwa nini hukufanya hayo mambo ya maendeleo kabla hujaoa? Au ulilazimishwa kuoa? Kuna watu wameoa na bado wanafanya mambo ya maendeleo. Jitafakari wapi unakosea.
 
Kwa nini hukufanya hayo mambo ya maendeleo kabla hujaoa? Au ulilazimishwa kuoa? Kuna watu wameoa na bado wanafanya mambo ya maendeleo. Jitafakari wapi unakosea.
Niliingia cha kike mkuu
 
Mkeo ana baraka zake, wengine ni misala tu
Seeee...!

1. Love is inversely proportional to distance.

Let love be "L" and distance be "D"

So L ≈ C/D where C is proportionality constant.

But C = a,b,c,d,e,f,t,w,r

Where a = age, b = beauty, c = characteristics, d = diseases, e = education (intelligence), f = family background, t = tribe, w = wealth.

Hence L = C/D

The more the distance the less the love

Ila C "result" ikiwa kubwa huongeza L kuwa kubwa.

Hii ni topic muhimu kwa vijana wanaotaka kuoa ama kuolewa hususani kwenye kuchambua hiyo "C"

2. Kwa waislamu, sisi wanaume tumeusiwa kuoa wanawake wawili, watatu hadi wanne, lakini 'tukishindwa' (kwa sababu mbalimbali' basi tuoe mmoja

Lakini pia tumeusiwa sisi kuwaoa kwa sababu za:-
(i) Uzuri wao
(ii) Ukwasi wao
(iii) Nasaba zao
(iv) Ucha Mungu wao.

Msisitizo ukawekwa kwenye ucha Mungu na kupuuza hayo matatu ya juu maana tutaongezewa...

Lakini atakaye chagua kuoa kwa sababu tatu za juu bila kuzingatia ucha Mungu 'huenda' akaangukia pabaya baada ya sababu hizo zilizomfanya aoe kuondoka.

Hapa napo panahitaji darasa lake.

Credits to JBourne59

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umefafanua vizuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…