Naomba Ushauri: Nimepata Kesi baada ya kumpiga mvuta sigara

Naomba Ushauri: Nimepata Kesi baada ya kumpiga mvuta sigara

Weka sasaiv mkuu. Utakuwa umenisaidia sana
Sheria ya Udhibiti wa Bidhaa za Tumbaku, Sura
121 imekataza uvutaji wa aina yoyote ile wa
bidhaa za tumbaku kwenye maeneo ya umma ili
kulinda afya ya wasiotumia bidhaa hizo. Katazo
hili linahusisha bidhaa za tumbaku
zinazotambulika kisheria ambazo ni sigara, siga,
sigarusi, misokoto, shisha, kiko na tumbaku ya
unga. Bidhaa za tumbaku zisizovutwa
(smokeless tobacco products) haziruhusiwi
kutumika katika maeneo na mazingira yoyote
nchini Tanzania.
Kifungu cha 12 cha Sheria ya Udhibiti wa
Bidhaa za Tumbaku, Sura 121 kimetafsiri
maeneo ya umma kama mahali ambapo
inatolewa huduma ya afya, maktaba, mahali pa
ibada, majengo au maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya mikutano ya kitamaduni na kijamii,
shughuli za michezo au burudani, sehemu za wazi nk.

Usipanic Mkuu huyo bwege asikutishe.
 
wavuta sigara wanaamini kila mtu anapenda sigara. Huwa sipendi kabisaa hiyo harufu.
Nimekaa kwenye benchi kijiweni nashangaa ghafla mtu kawasha kiberiti puuff. Naangalia pembeni pua yangu inanakutana na moshi mzito wa Sigara. Halafu mtu yupo comfortable kabisaa hana habari. Nikamuwasha kofi mdomoni hadi akatema hiyo Sigara.

Sasa hivi nasubiri nije nichukuliwe maana nasikia ameenda Polisi. Ni mzee wa makomo na ameapa atanifunga. Kama Kuna kifungu chochote cha sheria kinachokataza matumizi ya tumbaku hadharani naombeni ili nijiandae kwa lolote

Kalale kwingine kwa amani, kwa huu ujuaji utalala sero bila sababu. Hata kama kuna vifungu, vipo vingine haviruhusu kujichukulia sheria mkononi
 
wavuta sigara wanaamini kila mtu anapenda sigara. Huwa sipendi kabisaa hiyo harufu.
Nimekaa kwenye benchi kijiweni nashangaa ghafla mtu kawasha kiberiti puuff. Naangalia pembeni pua yangu inanakutana na moshi mzito wa Sigara. Halafu mtu yupo comfortable kabisaa hana habari. Nikamuwasha kofi mdomoni hadi akatema hiyo Sigara.

Sasa hivi nasubiri nije nichukuliwe maana nasikia ameenda Polisi. Ni mzee wa makomo na ameapa atanifunga. Kama Kuna kifungu chochote cha sheria kinachokataza matumizi ya tumbaku hadharani naombeni ili nijiandae kwa lolote
Ulipaswa kumpeleka mahakamani na kumdai fidia kwa kuhatarisha afya yako. Umeharibu kumpiga...atakupeleka mahakama na atakudai fidia kwa kumdhuru...kesi ya jinai hiyo!
 
S
Hongera mkuu kwa kuifunza adabu hiyo taka taka. Ipo sheria inayokataza kuvuta sigara kwenye umma Adhabu yake nadhani ni Mil 2 au kifungo miezi sita kesho nitaiweka hapa jamvini.
Shida ya hiyo Sheria ni jinsi ya kuithibitishia mahakama kuwa huyo mtu alivuta sigara kwenye hadhara ipi kwani yapo maeneo mahsusi yqliyoainishwa na Sheria hiyo. Aende tu mahabusu kwa kumshambulia mzee wa watu na kumdhuru mwili. Miezi 6 itamtosha kubadili tabia yake ya kujichukulia Sheria mkononi!
 
Kataa hujampuga kofi bali ulimwambia aache kuvuta sigara hadharani maana anaumiza wengine.

Andika maelezo hayo polisi, umuache athibitishe yeye kwa clear evidence kama ulimpiga.
 
Wewe kaseme kwamba una tatizo la pumu sasa ma moshi moshi kwako ni tatizo kubwa sana ........
 
Muwahi ukamshitaki kwa kuhatarisha afya yako na watu wengine.

Angalizo: mimi mbumbumbu wa Sheria
 
wavuta sigara wanaamini kila mtu anapenda sigara. Huwa sipendi kabisaa hiyo harufu.
Nimekaa kwenye benchi kijiweni nashangaa ghafla mtu kawasha kiberiti puuff. Naangalia pembeni pua yangu inanakutana na moshi mzito wa Sigara. Halafu mtu yupo comfortable kabisaa hana habari. Nikamuwasha kofi mdomoni hadi akatema hiyo Sigara.

Sasa hivi nasubiri nije nichukuliwe maana nasikia ameenda Polisi. Ni mzee wa makomo na ameapa atanifunga. Kama Kuna kifungu chochote cha sheria kinachokataza matumizi ya tumbaku hadharani naombeni ili nijiandae kwa lolote
Unakaa kijiwe cha kahawa siku nzima kubishana simba na yanga pumbav
 
Back
Top Bottom