Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

Kama nimeelewa vizuri jamaa hana cha kupoteza,asubiri hiyo tathmini ifanyike then arudi mahakamani kupinga kiwanja chake kuuzwa (kumbuka mahakama inakitambua kiwanja kama mali yake pawe pana nyumba au hapana) huyo mwanamke atamtafuta yeye ampe chochote kitu wamalizane.

Hapo atajipigia anavyotaka yaani atakuwa huru kukataa kila offer anayotaka then yeye atapendekeza ya kwake anayoona inamtosha akiiona ndogo andoe nyumba yake apeleke anakotaka.
Mahakama inalitambua hilo.
Kasome kesi ya bi HAWA mohamedi
 
Mm siyo mwanasheria kitaaluma
Lakini hapo unatakiwa umlipe pesa yenye thaman na mgao wake il nyumba iwe yako. Mfano kama mnagawana 60 kwa 40% . Thaman ya 40% ya nyumba as per evaluation ni shiling ngapi?? Unampa mnamalizana
Amlipe pesa ya nini?

Mahakama inatambua kiwanja kama mali yake hapo aende akaweke pingamizi la kuuzwa kiwanja chake then mwanamke ataamua nyumba ivunjwe au apewe hela kidogo asogee pembeni.
 
Hiyo hela sasa anayo?

Kama hana hela,
Basi Apeleke kesi mbele,
Nyumba apangishe kwa miaka miwili.
Huku anajipanga pia kujiongeza hela.

Hukumu ikitoka ameshindwa ndio waendelee na tathimin na atakuwa amejipanga kumlipa mwanamke.

Ajaribu kupigana vita ambayo hata akishindwa damage inaweza kuwa recovered .
 
Mkuu umesema ni mpenzi meaning kwamba hamkufunga ndoa???
Kata rufaa kaka...


Omba zuio la utekelezaji wa Hukumu (Stay of Execution) mapema then anza taaratibu za kukata rufaa...

KIfungu cha 160 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinasema wanandoa wakikaa miaka miwili pamoja mfululizo sio kuna siku alikuwa anaenda kwao hapana miaka miwili mfululizo...

Na pia wakiishi kama mke na mume..

Na jamii ikiwatambua hvyo hao watahesabika na mahakama wakati wa taraka kuwa ni wanandoa...

Sasa hata kwao ulienda kujitambulisha, kwenu wana mjua mmekaa miaka miwili kwel mbona matobo mengi hapa mkuu wamekuchezea...


Kataa rufaa tafuta wakili mzuri uokoe nyumba hiyo
 
Kwan uko wap?
Mpenz unagawana nae Mali?.
Kwan mmezaa?.
Kukaa tu miaka miwili tu ndio wamekushindia.

Aisee kata Rufaa. Kesi isogee mbele.

Mm nikajua ni mke wa ndoa
Naomba kuuliza nilisikia kukaa na mpenzi miaka miwili na zaidi wanaita ni dhana ya ndoa kisheria ila sio kimaandishi na ushahidi sas hapo si kwenye kugawana mali si wanafidia muda wake. Je ndo anaweza kupewa 1/3 ya mali kwa huo muda waliokaa?

Swali la pili kwa jamaa mmekaa miaka mingapi? na mlikua mnatafuta kugundua nini kwenye hayo mahusiano bila kupachikana mimba kaka? Mpka mkajenga pamoja. Ni uzuni kwakweli.
 
Wanaume wengine nawashauri ifuatavyo
Ikitokea umekaa na mwanamke miaka 16 ila hamjafunga ndoa na mkakorofishana na akakimbilia mahakamani kudai talaka,jambo la kwanza kulifanya ni kukataa kuwa sio mke wako.
Wkt anatakiwa athibitishe kuwa yeye ni mke wako,tayari utakuwa umepata akili kutoka kwenye vikao vyetu nini cha kufanya.
Kataa kila mahali utakapoitwa kwa shauri lolote kianzia baraza la kata la usuluhishi kuwa huyo sio mke wako.
Utatengeneza njia ya ushindi mbele.
 
Naomba kuuliza nilisikia kukaa na mpenzi miaka miwili na zaidi wanaita ni dhana ya ndoa kisheria ila sio kimaandishi na ushahidi sas hapo si kwenye kugawana mali si wanafidia muda wake. Je ndo anaweza kupewa 1/3 ya mali kwa huo muda waliokaa?

Swali la pili kwa jamaa mmekaa miaka mingapi? na mlikua mnatafuta kugundua nini kwenye hayo mahusiano bila kupachikana mimba kaka? Mpka mkajenga pamoja. Ni uzuni kwakweli.
Labda huyo Mwanamke atakua Single mother.
 
Jaribu kutumia akili na siyo hisia. Ulitaka nyumba ijengwe angani??? Unafikiri mahakama haijui nyumba inakaa ardhini?? Mpaka hiyo tathmini inapigwa mahakama haijui nyumba ipo wapi???
Mahakama inajua ila Kuna vitu ukilala mahakama inasukuma liende, mahakama haitetei mtu Bali hoja zako na kujitambua kwako waweza kuigomea mahakama sababu mahakamainasimamia Sheria na baadhi ya vitu si Sheria ukilala inakula kwako, ulipokosea demi kaleta wakili fasta ilikuwa utafte wakili yaani chuma kwa chuma, Mali kubwa usijaribu kuzitetea wewe kama wewe.
 
Mimi na mpenzi wangu tuliyeishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tuliachana baada ya mwanamke huyo kuanza visa na akaenda nyumbani kwao. Badae akaibukia mahakamani akiomba talaka na mgawanyo wa mali akiongozwa na wakili mmoja hivi ambae ni ndugu yake.

Moja ya mali ni nyumba ambayo mahakama imeona tumechuma pamoja lakini mahakama hiyohiyo amejiridhisha kuwa kiwanja ni mali yangu peke yangu. Sasa mahakama imeagiza nyumba iuzwe tugawane kwa asilimia ambazo mahakama imeziona. Mimi sitaki kuuza kiwanja changu ambacho mahakama pia imedhibitisha kuwa ni mali yangu pekee yangu ila nyumba ambayo imejengwa ndio imeonekana tumechangia kujenga na huyo mwanamke. Je hii hukumu itatekelezeka vipi kisheria maana ndio tunasubili uthamini?
Ni stori ya kutunga, ila ngoja tupate ufafanuzi kutoka kwa mawakili, tupate kujifunza.
 
Back
Top Bottom