Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 17,499
- 25,295
Mahakama inalitambua hilo.Kama nimeelewa vizuri jamaa hana cha kupoteza,asubiri hiyo tathmini ifanyike then arudi mahakamani kupinga kiwanja chake kuuzwa (kumbuka mahakama inakitambua kiwanja kama mali yake pawe pana nyumba au hapana) huyo mwanamke atamtafuta yeye ampe chochote kitu wamalizane.
Hapo atajipigia anavyotaka yaani atakuwa huru kukataa kila offer anayotaka then yeye atapendekeza ya kwake anayoona inamtosha akiiona ndogo andoe nyumba yake apeleke anakotaka.
Titi fa tati 😂😂😂😂😂😂Najua, sasa wao watathibitishaje kuwa alikuwa anakaa kila siku?.
Mm ntasema nilikuwa silali nae. Anakuja na kuondoka, mahakama sasa au yeye alete mashahidi kuwa alikuwa analala na mm
Amlipe pesa ya nini?Mm siyo mwanasheria kitaaluma
Lakini hapo unatakiwa umlipe pesa yenye thaman na mgao wake il nyumba iwe yako. Mfano kama mnagawana 60 kwa 40% . Thaman ya 40% ya nyumba as per evaluation ni shiling ngapi?? Unampa mnamalizana
Jaribu kutumia akili na siyo hisia. Ulitaka nyumba ijengwe angani??? Unafikiri mahakama haijui nyumba inakaa ardhini?? Mpaka hiyo tathmini inapigwa mahakama haijui nyumba ipo wapi???then arudi mahakamani kupinga kiwanja chake kuuzwa
Hiyo hela sasa anayo?
Funguka kidogo ,angekua amezaa naye ingekuajeKosa lilipoanzia ni kushindwa kumzalisha, pole sana mkuu
Kata rufaa kaka...Mkuu umesema ni mpenzi meaning kwamba hamkufunga ndoa???
ikiwa hukufunga ndoa kata rufaa,mbele huko hawezi kukushinda.Nasisitiza kata rufaa huyo sio mke ni hawara.Wasikutishie kata rufaa halafu tupeane mbinu.Hatukufunga ndoa
Naomba kuuliza nilisikia kukaa na mpenzi miaka miwili na zaidi wanaita ni dhana ya ndoa kisheria ila sio kimaandishi na ushahidi sas hapo si kwenye kugawana mali si wanafidia muda wake. Je ndo anaweza kupewa 1/3 ya mali kwa huo muda waliokaa?Kwan uko wap?
Mpenz unagawana nae Mali?.
Kwan mmezaa?.
Kukaa tu miaka miwili tu ndio wamekushindia.
Aisee kata Rufaa. Kesi isogee mbele.
Mm nikajua ni mke wa ndoa
Sahihi ndugu tafta wakili huyo Mwanamke aende zake akatafte bwana mwingineHana haki ya kuchukua chochote kwako, nenda ofisi yoyote ya wakili atakusaidia.
Sasa mkuu alikushtaki kama mke wako au ?Hatukufunga ndoa
Hatukufunga ndoa
Sasa mkuu mbona unakua Mnyonge mwanamke hamjazaa na hamja funga nae ndoa mlikua mnaishi kiuni tu, kwanini ulikubali kwenda kwenye Mambo ya usuluhishi wa ndoa?Wanakutapeli
Labda huyo Mwanamke atakua Single mother.Naomba kuuliza nilisikia kukaa na mpenzi miaka miwili na zaidi wanaita ni dhana ya ndoa kisheria ila sio kimaandishi na ushahidi sas hapo si kwenye kugawana mali si wanafidia muda wake. Je ndo anaweza kupewa 1/3 ya mali kwa huo muda waliokaa?
Swali la pili kwa jamaa mmekaa miaka mingapi? na mlikua mnatafuta kugundua nini kwenye hayo mahusiano bila kupachikana mimba kaka? Mpka mkajenga pamoja. Ni uzuni kwakweli.
Mahakama inajua ila Kuna vitu ukilala mahakama inasukuma liende, mahakama haitetei mtu Bali hoja zako na kujitambua kwako waweza kuigomea mahakama sababu mahakamainasimamia Sheria na baadhi ya vitu si Sheria ukilala inakula kwako, ulipokosea demi kaleta wakili fasta ilikuwa utafte wakili yaani chuma kwa chuma, Mali kubwa usijaribu kuzitetea wewe kama wewe.Jaribu kutumia akili na siyo hisia. Ulitaka nyumba ijengwe angani??? Unafikiri mahakama haijui nyumba inakaa ardhini?? Mpaka hiyo tathmini inapigwa mahakama haijui nyumba ipo wapi???
Ni stori ya kutunga, ila ngoja tupate ufafanuzi kutoka kwa mawakili, tupate kujifunza.Mimi na mpenzi wangu tuliyeishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tuliachana baada ya mwanamke huyo kuanza visa na akaenda nyumbani kwao. Badae akaibukia mahakamani akiomba talaka na mgawanyo wa mali akiongozwa na wakili mmoja hivi ambae ni ndugu yake.
Moja ya mali ni nyumba ambayo mahakama imeona tumechuma pamoja lakini mahakama hiyohiyo amejiridhisha kuwa kiwanja ni mali yangu peke yangu. Sasa mahakama imeagiza nyumba iuzwe tugawane kwa asilimia ambazo mahakama imeziona. Mimi sitaki kuuza kiwanja changu ambacho mahakama pia imedhibitisha kuwa ni mali yangu pekee yangu ila nyumba ambayo imejengwa ndio imeonekana tumechangia kujenga na huyo mwanamke. Je hii hukumu itatekelezeka vipi kisheria maana ndio tunasubili uthamini?