Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

Najua.

Ila huyu mwanamkr alikuwa anakuja na kuondoka. Hakuwah kulala zaid ya siku 3 na sijazaa nae.
Nani amekwambia hivyo? Mwenzio keshakubali kwamba walikuwa wanaishi pamoja na nyumba wamejenga pamoja!
 
kama mwenye kiwanja alipanga baada ya miaka 10 apauze kwa Tsh 80,000,000/= leo pana thamani pamoja na nyumba vyote 30,000,000/= unategemea mahakama kumpoka haki yake kwa kulazimisha auze hivyo hivyo?
Umeshawahi kufanyiwa land valuation yoyote au kuhudhuria?? Huwa inadili na vitu gani??? Nyumba siyo sehemu ya land valuation???
 
Pia NecZec ukithibitisha pia kuwa Wakili ni ndugu yake, kata rufaa kuwa Wakili ana maslah binafsi na mteja wake.

Kithibitisho unaonyesha Mahakama kuwa wana undugu wa karibu na wakili.
Conflict of interest
Mkuu wakili hata mwanao anaweza kuwa wakili wako nadhani,, Hakimu au jaji ndio changamoto kama akiwa na ukaribu na mmoja walalamikiwa au mlalamikaji .
 
Sheria za wapi hizo
Jamaa ameingizwa mjini tu hapo
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act, 1971), kifungu cha 160(1), ikiwa mwanaume na mwanamke wameishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi, na katika mazingira ambayo jamii inawatambua kama mume na mke, basi kuna dhana ya ndoa inayoweza kutolewa na mahakama.

📜 Kifungu cha 160(1) cha Sheria ya Ndoa, 1971:

✅ Vigezo vya kutambuliwa kwa dhana ya ndoa:
  • Kuishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi.
  • Jamii inayowazunguka kuwatambua kama mume na mke.
  • Kuishi kama wanandoa, ikiwa ni pamoja na kushirikiana majukumu ya kifamilia.

⚠️ Mambo ya kuzingatia:
  • Dhana hii si ndoa halali moja kwa moja, bali ni dhana inayoweza kupingwa mahakamani.
  • Inatumika hasa katika mazingira ya migogoro ya kifamilia, mirathi, au madai ya matunzo.
  • Ikiwa dhana hii itathibitishwa, mmoja hawezi kuoa au kuolewa tena bila kupata hati ya kuvunja ndoa kutoka mahakamani [1] .

📚 Rejea:
  • Sheria ya Ndoa ya Tanzania, 1971, kifungu cha 160(1).
  • Kesi ya Kimba v. Kimba, ambapo mahakama ilitambua dhana ya ndoa baada ya wanandoa kuishi pamoja kwa muda mrefu [2] .

Ikiwa unahitaji msaada zaidi kuhusu haki zako au hatua za kuchukua katika hali kama hii, ni vyema kushauriana na wakili au kituo cha msaada wa kisheria kilicho karibu nawe.
 
Mapenzi/mahusiano huwa yana expire

Ova
 
Ibomoe mgawane matofali halafu ujenge kwenye kiwanja chako. Usikubali iuzwe maana na kiwanja chako kitauzwa.
 
Yawezekana Jamaa kwa sasa uchumi umeyumba na hataweza kumlioa
Mara nyigi hawa hugeuka baada ya sisis uchumi kuyumba
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
 
Mbona hiyo sababu ndogo sana ya ninyi kuachana?, wote hapo mna kosa, ww humuamini, na yeye huenda alikuwa na ajenda zake za siri, ndo maana alikuacha evangelical
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Mkuu siyo ndoa ya Kikristo wala ya Kimila ni Mwanamke alimfata Mwanaume wakaanza kuishi pamoja kama mke na mume, yani ata wewe kama ni Muislam ungefanya hivyo yangekukuta tu yalivyo mkuta huyu Mwenzetu.
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Umesikia wapi kwamba huyo jamaa alikuwa na ndoa ya Kikristo?
 
Kaeni mtumie tu ubinadamu hapo lazima huyo binti aumie,mgawie kilicho chake maisha yaendelee,hata kama ni asilimia thelathini
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Wewe una hasira tu dhidi ya ukristo.
Umesoma vizuri maelezo ya mleta mada?
Amesema hawajafunga ndoa bali walikuwa wanaishi tu kama mume na mke kwa miaka kadhaa wakajenga nyumba wote ktk kiwanja cha mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…