Naomba ushauri, ninunue pikipiki au nifungue library ya kuingiza movie katika flash? (nina Tsh. milioni 1. 2)

Mtu kaomba kujua kati ya pikpik au library we unaleta biashara nyingine ya machuma chuma ebu kua serious acha ujuaji
Nunua welding machine angle grinder na drill ufungue goli uwe unachomelea riziki utapata mkuu
 
Watu kama nyie mnakera ..alf mnajidai wajuaji kumbe hakuna kitu ,,biashara unazomshauri na library anayotaka kufungua unaona vinaendana ?
1.mtu anafanya kitu anachopenda ndio ataeza kukisimamia vizur alaf vitu anavotka haviitaji usimamizi mkubwa Wala havichukui mda wake mwingi kuvifatilia hii inamfanya afanye hata kazi zingine
Pili library hupat hasara movie hata uwarushie watu 100 haiaribiki na unaweza uza hata movie za mwaka 1990 ila kitumbua Cha juzi huezi muuzie mteja
 
Nina uzoefu juu Hilo mkuu, nilimpa kijana boda yangu akaendesha wiki 2 tu akaipiga chini,hizo gharama siyo poa kaka..taa kubwa, dashboard,foot rest, na hapo Hela aliyoleta Kwa wiki 2 haitoshi kununua hivyo vyote
Hawa vijana wa siku hizi wanachukulia maisha poa sana
 
Nawe kua muelewa kilimo kinaitaji mtaji wa kutosha na muda mwingi uwepo kusimamia .vinginevo utalia na kusaga meno
Kwani kabla hajaipata hiyo hela alikuwa anaishije mkuu? Ni uhakika huo ni mtaji wake siyo hana hela ya kujikimu kama ni hivyo hata kwenye boda aombee mema asipate changamoto yoyote......
 
Chukua pikipiki na ukomae nayo wewe mwenyewe.

Ukiwa na nidhamu na kazi yako pamoja na nidhamu ya pesa utafanya la maana zaidi.

Kufungua library ni kutengeneza kijiwe cha kupigia soga tu.
Umemaliza kila kitu.
 
Ushauri mzuri huu.
 
Kama yupo Mbeya atapiga hela,Isanga,Mama John,Karibia sehemu nyingi niliona hiki kitu na kina watu kwa jioni.
Kuna watu wachache sana wanajua habari za netflx,Torrents..
 
Acha kumuingiza Chaka mwenzio, library ya muziki inalipa sana uswahilini
Nimetoa reference,nilikuwa Mbeya nimeona sana hiki kitu.
Kuna ofsi nilienda kubwa tu,wafanyakazi wanasimulia Squid game na mpaka wanapoenda kuichukua😀😀
Nikasema nisiwe mmbeya kusema kuna netflx nitakata ugali wa mtu.
Mdada amekusanya flash huyo kaenda kwa Library😀😀😀
 
ikitokea umenunua pikipiki jiepushe na wake za watu, matumizi ya madawa ya kulevya na kusafirisha magendo
 
Kwa maktaba hela haitatosha kwa sababu itakubidi ununue kompyuta na fremu ya biashara vitagharimu zaidi ya hiyo 1.2m
 
Wengi mnashaurinlakinibhamjawwhi kufanya hizo kazi NI kwa kuangalia nnje tu...Kama umri unaruhusu fungua movie libray...unamda wa kuziangalia na kujua wahusika watoto watoto ndio wanajua Kama Kuna biashara Kama hio mi nilikuwa sijui naonaga tu vyumba vimejaa cd...mpaka mmoja wao alipokuja kuomba ushauri na kujifunza Adobe ndio nikamdodosa na kwenda kwenye ofisi yake anapoga kazi...na haiztaki location ya usoni sana kwenye makazi ya wamama wanaoshinda nyumbani Kuna movie kibao wanazifuatilia naingizo yake NI Kama kupiga photocopy tu..movie moja Mia mbili Hadi Mia tana unategemea imetoka lini na inahitajika kivip...wanauza soft copy...hii biashara nilishawahi kufanya enzi hizo tunaburn CD music na kurusha kwenye simu...we ni kuwa na umeme tu...kazi imeisha kitoto Toto unaweza maana MTU anakuja anakuimbia au kuniambia kipande inabidi ujue anataka Nini...boda sijawahio kufanya kwa kweli na naziogopa
 
Pikipiki inalipa ila usimamizi wa karibu muhimu sana. Mimi nilinunua nikampa mtu kwa mkataba.
Alikuwa analipa vizuri tu mpaka nikashawishika kununua ya pili.
Dahh! Miezi miwili Nyuma dogo akaanza sarakasi za kijinga nikamfuatilia nikagundua alishaanza kunywa pombe Hadi akawa anashindwa kulipa pesa.

Niliamua kuchukua Pikipiki na kuuza kabisa maana Mimi situmii.

Ukitaka ule loss nunua Pikipiki mpya halafu tukutane na dereva mpuuzi utajuta.
Maisha ni uangalifu na kupanga mikakati thabiti.

Mimi nakushauri hivi;
Kama dereva ni "wewe mwenyewe" basi nunua Pikipiki kama sivyo utapoteza pesa.
 
Kwani kabla hajaipata hiyo hela alikuwa anaishije mkuu? Ni uhakika huo ni mtaji wake siyo hana hela ya kujikimu kama ni hivyo hata kwenye boda aombee mema asipate changamoto yoyote......
Ni mkazi wa mjini daslam, ina maana hapo kabla alikua anapiga mishe zake hapo mjini, kumpeleka huko ndichi hizo mishe atapigaje na inabidi asimamie shamba ambalo kwa miezi kadhaa hana hakika kama atapata kitu
 
Saloon ya kiume tayari boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…