Naomba Ushauri: Nisimame na Baba Mzazi au wa kambo?


Pole na misukosuko.

Navyoiona.

Baba yako mzazi anakuja kuvuna tu, japo alijitokeza mara moja moja ila tambua kwamba msingi wa mtoto ni muhimu sana na huo msingi unajengwa udogoni. Baba wa kambo alikuchukua kama mwanaye anasimama kwenye nafasi ambayo baba yako mzazi alishindwa.

Mpe heshima yake huyo Mzee hata kama ni mshirikina. Angekuwa na nia mbaya na wewe, angekuulia mbali ukiwa mdogo. Ushirikina ni mambo yetu ya kiafrika na ni mambo yake binafsi maadamu hajakushirikisha, tambua anakuheshimu.

Baba yako mzazi pia pamoja na kutokusimamia majukumu yake, alionesha kukutambua na mapenzi yake kwako, lakini hakulipia gharama za wewe kufika hapo. Fikiria asingetokea baba wa kambo kumuoa mama yako na akakubali kukulea wewe ungekuwa na maisha gani? Hapo ndo utaelewa kwamba baba mzazi alifufail.

Ningekuwa wewe, kwa sasa ningemshauri mama arejee mezani waongee, wapange namna ya kuwaruhusu nyie kuendelea na maisha yenu. Baba wa kambo mfanye msimamizi katika mchakato wa kuoa, huyo ndo amekupa maisha.

Baba yako pia umshirikishe akubali na kumheshimu huyo baba wakambo na maamuzi yako ya kumpa jukumu la kukusimamia kwenye ndoa. Yeye utamshirikisha na kushirikiana naye kama baba.

Yote haya unafanya kulinda heshima yako, ya mama yako, baba zako wawil. Lakini zaidi ya yote, unajenga future yako.


I hope nimeongea angalau point moja.
 
Simama na wote kwa sababu:-
Baba mlezi - kulipa fadhila maana alikutunza
Baba mzazi - ana baraka zako
 
Hongera kwa kuwa na baba wawili. Ni kama Rich dad na Poor Dad. Nenda nao wote kwani hujaonyesha ugumu uko wapi.

Wewe songa na maisha wakati ukiwajulia hali.
Kuhusu ndoa, mwambie huyo dingi kuwa wewe huwezi kumlazimisha mama kurudi...na unahitaji kuoa. Hivyo endelea na mipango ya ndoa.
 
Hiyo miaka 13 mama ambayo hakuwepo nani alikulea? Na ww sio mtoto wake?

Laana nyingine tunazitafuta wenyewe na tunazipata kirahisi sana....! Au umeungana ma mama Yako?

Stick na Baba wa Kambo...huyo Baba mzazi kama kawaida avute noti kistyle...mpulizie mara kwa mara kukwepa laana yake!

Ila maisha mpe baba wa Kambo...
 
Kaka nakushauri usimame na wote kila mmoja kwa nafasi yake,haki yake na ushiriki wake katika malezi yako. Zingatia kusimamia haki hata kama hisia zako zinakinzana nayo.
 
Baba mzazi na baba mlezi wote ni wazazi wako. Baba mzazi una bloodline nae alitamani kuishi nawe utotoni sema mama yako changamoto, thus hakukutupa alikukumbuka kwa zawadi. Baba mlezi ni mtu muhimu Sana aliyetengeneza future yako.
Mama ni mama haijalishi mapungufu yake. Huo ni ugomvi wao wazazi hayakuhusu.
USHAURI MKUU
1.Simama neutral usiegemee upande wowote waheshimu wazazi wako watatu.
2.Watambue wote ni Baba zako ya huku ni ya huku na ya kule ni ya kule yabakie siri yako, hata mama YAKO usimwambie, maana upo ugomvi wa asili Kati ya mwanamke na mwanaume usioisha hasa kwa waliohitilafiana, wanawake ni watu wanaoishi na bifu, mioyo yao ni migumu kusamehe.
3.Toa matumizi potepote sio lazima uwape wote kwa pamoja. SAsa ndio kipindi Mlezi wako anahitaji Sana fadhila zako
4.Sioni kama pana haja ya kuwaficha watoto wako kutowatambulisha kwa baba zao, sema wanatokea ukoo mmoja.
 
Ushauri mzuri. wajali wote tu. Kama baba yako mzazi pia ameoenesha upendo kwenye maisha yako ww huna budi kumpenda na kumjali pia. Mda mwengine huwezi jua yeye alishindwana nn na mama ako wakaachana. Vitu vyengine huwezi mwambia mtoto. Utaleta uchonganishi usio na maana kwa mzazi mwenza. Ushauri wangu nenda nao sawa tu utabarikiwa. Usimtenge mtu au kuhukumu kisa hajakulea.
 
Thread closed.
 
Anatumia majina ya baba mlezi kwenye vyeti vipi hili kuna namna ya kuweza kubadili au aachane nalo
 
Eti baba mlezi ni Mshirikina, tena maneno hayo unayapata kutoka upande wa ndugu wa baba.

Huo ni upuuzi. Kama anafanya ushirikina kwenye biashara yake, basi afanye. Si kwa nia ya kulinda mambo yake? Kakudhuru? Jibu ni Hapana. Mama yako aliondoka miaka 13 imepita sasa, angekuwa na nia ungekuwa msukule wake muda huu.

Hao ndugu wa baba ni washenzi sana. Wanataka kukuvuta uegemee upande wako zaidi. Achana nao.

Bila kusita sita, enenda na baba yako mlezi. Huyo ndiye mzee wako. Kakulea na kukukuza mpaka umekuwa jitu. Gharama zake unazijua!? Kama ni hivyo vichips vya mara moja moja kutoka kwa sperm donor, hata mtu yeyote angeweza kukutendea hayo. Muheshimu tu kama mbegu iliyokutengeneza.

Nakushauri, kuwa makini sana na watu wanaopenda kuwaongelea wengine kwa mabaya tu.
 
Simama na wote pale wanapokuhitaji, sijaona sehemu ukisema kuna aliekubagua kipindi unakua…so ni vyema kutokuwabagua pia. Fanya kwa kila mmoja kadri uwezo wako utakapoishia
 

Simama na atakayesimama na wewe.
Hayo mengine waachie Waume wa Baba yako.

Atakayekukorofisha piga Chini, akijirudi mnaendelea mlipoishia
 

Mshirikina ni mshirikina, mshirikina hajawahi kuwa MTU Mzuri.
Hata awe NI mama yako.

Ukishagundua mtu ni mshirikina kaa naye Kwa machale. Ikiwezekana muepuke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…