Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Hahahahaha aendelee tu na Ujomba wake!Alikuwa akija yeye alimtambua kama mjomba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahahaha aendelee tu na Ujomba wake!Alikuwa akija yeye alimtambua kama mjomba
Usimame na yupi kwenye issue gani hasa?Habari Wakuu, nakuja mbele yenu kuomba ushauri, japo nimepata shauri mbalimbali za hapa na pale kwa watu wa karibu na wa mbali niliowahi kukutana nao.
Nianze na historia yangu kwa ufupi. Nilizaliwa mwanzoni mwa miaka ya 90.
Mama alizalia nyumbani kwao wakati bado ni mwanafunzi, haikua rahisi kwa maelezo yake kwa jambo la kubeba mimba ili hali walikua jamii maskini na wapo watoto 7 kwa wakati huo japo wamezaliwa wengi zaidi ya hao.
Ilifika kipindi walimfukuza nyumbani na kuenda kukaa kwa mama mmoja mpaka alipojifungua.
Miaka hiyo ya 90 mwanzoni nikiwa bado mdogo aliolewa kwa ndoa na mwanamume mwingine ambaye sio baba mzazi.
Hakika ndoa ilikua ya kifahari maana sio kwa picha hizo nilizoona kwenye albamu ya picha enzi hizo. Sherehe ilifana sana.
Mwaka 1997 ulitokea ugomvi mkubwa kati ya mama na baba wa kambo, mama aliamua kuondoka na kurudi kijijini ila hakufikia kwa baba na mama yake ila kwa rafiki yake kipenzi wa kusoma nae.
Nakumbuka rafiki yake na mama alikua akiiuza baa maarufu hapo kwenye hiyo wilaya, ambapo alitupa chumba kimoja wapo cha wageni ili tujihifadhi hapo.
Siku moja nikiwa nacheza nje na watoto wenzangu, babu alipita na kuniona maana palikuwa na maarufu na babu alikuwa mtumishi wa serikali hivyo akitoka kupokea mshahara dirisha la halmashauri basi hupita kwenye hiyo baa na kupata kinywaji.
Aliponiona akauliza mama yuko wapi?
Watoto hua hatuna siri, basi nikajibu yupo ndani. Kisha babu akaondoka zake. Jumapili nilimuona bibi ghafla akimsihi mama waondoke nae kurudi nyumbani.
Nakumbuka siku hiyo nilitembea umbali mrefu sana hadi tukafika kwa babu na bibi. Tulikaa hapo kwa muda wa siku 7, na nilikua nasoma darasa la 1, hivyo nilikua naenda shule ya jirani ili nisikose masomo, babu aliomba kwa mkuu wa shule nisome hapo.
Jumapili ya hilo wiki baba wa kambo alikuja kutuchukua na land rover 109.
View attachment 2567033
Tukarudi mjini. Maisha yakaendelea japo nilikua mtoto sio vyote nakumbuka.
Nakumbuka siku moja tulijipata nyumbani kwa msimamizi wa ndoa ya baba wa kambo na mama. Sikumbuki kwanini. Nilikaa pale kwa muda mrefu huku nikiendelea na masomo yangu ya darasa la 2.
Tarehe 31 Desemba 1999 tulihamia kwenye nyumba aliyojenga baba wa kambo nje kidogo ya mji.
Mambo yalizidi kuwa mabaya, ugomvi ulishamiri kwa miaka mingi sana japo mama hakuwa anaondoka tena kurudi kwao, maana yake alipambana na hali yake maana hapo familia iliongezeka na kufikia idadi ya watoto wa 3 ambapo wa 2 walikua ni wa baba wa kambo
Kipindi chote cha utoto baba mzazi alikuwa anakuja kwa mwaka mara moja kuniona shule ya msingi na tulipiga picha na kwenda sehemu za mjini na kula vizuri. Nakumbuka baba mzazi nilikua namuita mjomba. Maana watoto niwaropokaji. Japo alikuwa akinunua zawadi kwa ajili yangu, mama alizificha au kugawa ili kulinda ndoa yake.
Ilifika hatua yale maisha ya ugomvi na amani kukosekana nyumbani, mama aliondoka ghafla bila kujua alipokwenda.
Ikumbukwe kwa miaka yote hiyo, hakuna mtu alitetamka kwamba nina baba mzazi ambaye yupo sehemu fulani, so kwa utoto ule nilijua baba wa kambo ndie baba mzazi. Hata majina ya shule nilitumia ya kwake.
Tusonge mbele zaidi, nilipofika advanced level, form 5 na 6 nilianza kwenda nyumbani kwa baba mzazi na mawasiliano yalipamba moto kwa kipindi hiki. Nilikua namiliki simu so ilikua rahisi kuwasiliana.
Baba mzazi alinieleza sababu kwanini hakumuoa mama, na akaoa mwanamke mwingine. Sikua huru sana wakati nipo kwa baba mzazi na ukizingatia maam wa kambo yupo maana ni mazingira mageni kwangu.. Uzuri ni kwamba nilikaa kwa baba mzazi kipindi cha likizo fupi tu.
Tuendelee mbele zaidi.
Kwa sasa ni mwajiriwa wa serikali, baba mzazi amekwisha staafu na baba wa kambo alikua mfanyabiashara lakini kwa sasa kasi na uwezo umepungua na hana msaidizi kwakua mwanae wa kwanza kwa mama ni mlemavu na wa pili bado anasoma chuo.
Kwa sasa nipo kwenye kipindi cha kuhitajika na wote, baba mzazi na wa kambo kwenye mambo mbalimbali.
Mfano nimeshindwa kufunga ndoa kisa baba wa kambo kutaka mama arudi kwanza nyumbani baada ya kuachana miaka 13 iliyopita.
Ndugu wa baba mzazi wamekua wakinitambua na kunishirikisha kwenye mambo mbalimbali ya kifamilia sasa, na kuna baadhi ya vitu baba wa kambo anavijua na vingine havijui na hii ni kutokana na ukaribu na urafiki wangu na baba yeyote nitakavyoona.
Mfano; baba wa kambo ni mshirikina kwenye biashara zake, hivyo sijawahi mueleza kuhusu watoto niliyozaa, japo baba mzazi anawajua wote.
Niwaombe ushauri wana jamvi, nisimame na yupi kwa sasa?
Pili, mimi sio mwandishi mzuri hivyo muniwie radhi.
Tatu, nipo tayari kutoa ufafanuzi mzuri endapo kuna mahali hapajaelewekaa vizuri.
Nia nikupata ushauri.
Asanteni na karibuni
Ni vyema ungeshauri kwa namna ambayo sijielewi.Hujielewi.
Mkuu, kuna kunyanyaswa kisaikolojia. Mfano kuna kupindi alikuwa akimpiga mama waziwazi au kugombana waziwazi. Tulishawahi kulala kwa watu mara kadha wa kadha. Sikupata ule upendo wa karibu kama mtoto na hivyo kunijengea hofu na kutojiamini kwa kuwa mara nyingi alikua akigomba na kufoka kwa nguvu.Sijaona sehemu "Baba wa kambo" alikunyanyasa.
Ni mshirikina unaogopa atadhuru wanao, mbona hakukudhuru wewe?
Na uache kumtusi kumuita mshirikina.
AsanteWote hao wanayo nafasi katika maisha yako, Baba wa kambo ndiye anaonekana kuchukua nafasi kubwa ya malezi yako hivyo huna budi nawe kulipa fadhila juu ya hilo yaani usimtupe kwani masikitiko yake dhidi yako Mungu anaweza kupokea na ukashikwa na shida nk, basi usimtupe, kumbuka alivyokulea isitoshe hata ubini wako ni jina lake ulipokuwa ukisoma shule.
Baba mzazi naye anayo nafasi pekee kwani huyo ndiye damu yako imeanzia hapo, bila ya yeye usingeweza kuja duniani na wala usingepata nafasi ya kwenda kuishi huko kwa baba wa kambo, kwa.jinsi ulivyoeleza baba mzazi naye alikuwa akija kukutembelea na kukuletea zawadi alipopata nafasi hiyo ilikuwa.ni ishara ya upendo kwako na tayari unao watoto na huyo Baba mzazi anawajua na kuwatambua watoto wako isitoshe ndugu wa upande wa Baba mzazi wanakutambua kama.mmoja ya wanafamilia wao basi huwezi kuwakiuka kwani hao ndio damu yako.
Hitimisho ni kwamba; Baba wa kambo anayo nafasi yake kwako kutokana na jinsi alivyokulea halikadhalika Baba mzazi ndiye aliyekuleta duniani na ndiye damu yako na damu ni nzito kuliko maji, basi kila mmoja mpe haki yake inayostahili kulingana na uwezo wako kwani kuhudumia watu wawili kwa wakati mmoja inabidi mtu ujipange lakini utafanyaje na hali ndio imekuwa hivyo, basi Omba Mungu akusaidie.
Hayo ni maoni yangu kulingana na hadithi yako, labda kuwepo na jambo kubwa lililojificha ambalo linakuogopesha na hukulisema, mfano Ushirikina wa baba wa kambo, kwani wewe unahofia nini juu ya huo ushirikina wake??, je unaogopa anaweza kukutoa wewe kafara au?, ushirikina wake upoje?, kumbuka pia kwa huyo baba wa kambo kuna wadogo zako wa damu mnaochangia mama hivyo tayari kumeshakuwepo na udugu kati ya wewe na huyo baba wa kambo kupitia hao wadogo zako.
.Mshirikina ni mshirikina, mshirikina hajawahi kuwa MTU Mzuri.
Hata awe NI mama yako.
Ukishagundua mtu ni mshirikina kaa naye Kwa machale. Ikiwezekana muepuke
Ilikua sababu ya kumuoa mama ili nije nirithi biashara zake, maana nilijiuliza miaka hiyo ni kweli alikosa binti asiyekuwa na mtoto?Mimi navyochukia watia mimba na kukimbia basi hapo baba yako ni huyo WA kambo .kama angetaka asikuleee angeweza kumwambia mama yako akurudishwe kwenu waanze upya.
Wote kwa sasa ni 60+, hapa kuna mambo mengi yanatukia mkuu.Usimame na yupi kwenye issue gani hasa?
Kwani wanakugombea?
Au kuna mazingira gani yanakufanya uchague upande?
Ukiendelea kuishi nao kama unavyoishi nao Sasa itakuaje?
Wao Kwa wao wenyewe ni maadui?
Mama yako yuko wapi?
Na anasemaje juu ya hili?
Ushirikina ni hadithi sababu ukiambiwa uthibitishe huwezi thibitisha.Ni vyema ungeshauri kwa namna ambayo sijielewi.
Mkuu, kuna kunyanyaswa kisaikolojia. Mfano kuna kupindi alikuwa akimpiga mama waziwazi au kugombana waziwazi. Tulishawahi kulala kwa watu mara kadha wa kadha. Sikupata ule upendo wa karibu kama mtoto na hivyo kunijengea hofu na kutojiamini kwa kuwa mara nyingi alikua akigomba na kufoka kwa nguvu.
Pia mama alivyoondoka nilikua chuo mwaka wa kwanza, nakumbuka alishawahi kuniandikisha ada.
Hakuwa na upendo ule wa kutoka moyoni huenda alifanya kwa kuwa nilikua nae.
Swali nililojiuliza ni kwamba kwa kipindi hicho ni kweli alikosa mwanamke wa kumwoa asiye kuwa na mtoto??
Hii ilikua nia maana hata mdogo wangu kwa mama ulemavu wake ni wa kutupiwa yani aligeuzwa kama chuma ulete (sijui niliwekeje hili.)
Kingine ni yeye kunitaka kufanya biashara zake ambapo misingi yake ni ya kishirikina.
Nimeona mengi na sipendi kuyaandika hapa maana naweza tambulika. Kwa sasa biashara zimedorora, na hivi karibuni nilienda likizo nyumbani, niliyosimuliwa na dogo na niliyoyaona, haina budi kumuita mshirikina, Mungu anisamehenkama nakosea.
Asante
.
Mkuu najaribu kueleza uhalisia, wala sipo hapa kumtetea baba mzazi na kumkandia baba wa kambo. Nashukuru kwa ushauri.Ushirikina ni hadithi sababu ukiambiwa uthibitishe huwezi thibitisha.
Na hata akiwa mshirikina wewe haikuhusu, huwezi mkataa mtu aliyekulea eti kisa tu mshirikina.
Kisaikolojia enheee?
Kumpiga mama ako ni manyanyaso pekee uliyopitia?
Najua haipendezi, najua sio vizuri. Ila uliwahi jiuliza kwanini wanapigana? Una uhakika mama ako sio mkorofi?
Una uhakika huyo unayemuita baba wa kambo sio chanzo cha ugomvi wao?
Wangapi wanaishi na baba zao wa damu lakini bado baba na mama wanapigana waziwazi? Vipi na hao wakatafute baba wengine kwa kuwa baba anampiga mama?
Hii sio sababu ya kutosha.
Alikuandikisha ada?
Yes, alikuwa sahihi hata mimi ningekuandikisha. Maana aliona husomeki umeanza kiburi kwa kuwa Umekutana na huyo mzee unayemuita baba mzazi.
Na kwa kuleta huu uzi hapa inathibitisha alikuwa sahihi, alichokihisi kinaenda kutokea.
Unataka kumkacha kisa " kula vizuri" mara moja kwa mwaka.
Unamuona huyo dingi ana upendo, kwa kuwa hujakaa naye. Ungekaa naye Ungemjua vizuri.
Hakumchukua mama ako wakati amefukuzwa kwao, alipomdanganya na kumpa Mimba.
Yote ya yote, maamuzi ni yako. Na nahisi ushayafanya hapa unataka kujustify tu.
Huelezei uhalisia.Mkuu najaribu kueleza uhalisia, wala sipo hapa kumtetea baba mzazi na kumkandia baba wa kambo. Nashukuru kwa ushauri.