Naomba Ushauri: Nisimame na Baba Mzazi au wa kambo?

Usimame na yupi kwenye issue gani hasa?
Kwani wanakugombea?
Au kuna mazingira gani yanakufanya uchague upande?
Ukiendelea kuishi nao kama unavyoishi nao Sasa itakuaje?
Wao Kwa wao wenyewe ni maadui?
Mama yako yuko wapi?
Na anasemaje juu ya hili?
 
I go for baba Mlezi. Anaweza tamka laana na ikakupata. Baba mzazi muheshimu lakin fanya maisha yako. Tengeneza your future. Kama ni percentage baba mzazi apate 10%, baba mlezi 20%. Maisha yako na wanao 70%. Imeisha iyo.
 
Heshima kwa walezi wote, hapo ulipofika umekula vya baba mlezi vingi sana na hata ufanyaje huwezi vilipa hivyo atleast show him some respect... at mshirikina? Unajuaje kama bamzazi sio mshirikina? Kila mmoja nenda nae sawa jitoe kadri uwezavyo. Afadhali wewe unao baba wawili wapo ambao hawana hata huyo mmoja
 
Hujielewi.
Ni vyema ungeshauri kwa namna ambayo sijielewi.
Sijaona sehemu "Baba wa kambo" alikunyanyasa.

Ni mshirikina unaogopa atadhuru wanao, mbona hakukudhuru wewe?


Na uache kumtusi kumuita mshirikina.
Mkuu, kuna kunyanyaswa kisaikolojia. Mfano kuna kupindi alikuwa akimpiga mama waziwazi au kugombana waziwazi. Tulishawahi kulala kwa watu mara kadha wa kadha. Sikupata ule upendo wa karibu kama mtoto na hivyo kunijengea hofu na kutojiamini kwa kuwa mara nyingi alikua akigomba na kufoka kwa nguvu.
Pia mama alivyoondoka nilikua chuo mwaka wa kwanza, nakumbuka alishawahi kuniandikisha ada.
Hakuwa na upendo ule wa kutoka moyoni huenda alifanya kwa kuwa nilikua nae.

Swali nililojiuliza ni kwamba kwa kipindi hicho ni kweli alikosa mwanamke wa kumwoa asiye kuwa na mtoto??
Hii ilikua nia maana hata mdogo wangu kwa mama ulemavu wake ni wa kutupiwa yani aligeuzwa kama chuma ulete (sijui niliwekeje hili.)

Kingine ni yeye kunitaka kufanya biashara zake ambapo misingi yake ni ya kishirikina.
Nimeona mengi na sipendi kuyaandika hapa maana naweza tambulika. Kwa sasa biashara zimedorora, na hivi karibuni nilienda likizo nyumbani, niliyosimuliwa na dogo na niliyoyaona, haina budi kumuita mshirikina, Mungu anisamehenkama nakosea.
Asante
Mshirikina ni mshirikina, mshirikina hajawahi kuwa MTU Mzuri.
Hata awe NI mama yako.

Ukishagundua mtu ni mshirikina kaa naye Kwa machale. Ikiwezekana muepuke
.
 
Mimi navyochukia watia mimba na kukimbia basi hapo baba yako ni huyo WA kambo .kama angetaka asikuleee angeweza kumwambia mama yako akurudishwe kwenu waanze upya.
Ilikua sababu ya kumuoa mama ili nije nirithi biashara zake, maana nilijiuliza miaka hiyo ni kweli alikosa binti asiyekuwa na mtoto?
 
Usimame na yupi kwenye issue gani hasa?
Kwani wanakugombea?
Au kuna mazingira gani yanakufanya uchague upande?
Ukiendelea kuishi nao kama unavyoishi nao Sasa itakuaje?
Wao Kwa wao wenyewe ni maadui?
Mama yako yuko wapi?
Na anasemaje juu ya hili?
Wote kwa sasa ni 60+, hapa kuna mambo mengi yanatukia mkuu.
 
Ilo liliro mkojolea mama Yako na kusepa na kuishia kukupa zawadi sio jitu ni tapeli tu hata baba wa kambo s alimkojolea mama yako ukapata ndugu wawili hachana na ilo tapeli likulekeza
 
Ushirikina ni hadithi sababu ukiambiwa uthibitishe huwezi thibitisha.
Na hata akiwa mshirikina wewe haikuhusu, huwezi mkataa mtu aliyekulea eti kisa tu mshirikina.
Kisaikolojia enheee?
Kumpiga mama ako ni manyanyaso pekee uliyopitia?
Najua haipendezi, najua sio vizuri. Ila uliwahi jiuliza kwanini wanapigana? Una uhakika mama ako sio mkorofi?
Una uhakika huyo unayemuita "baba mzazi" sio chanzo cha ugomvi wao?

Wangapi wanaishi na baba zao wa damu lakini bado baba na mama wanapigana waziwazi? Vipi na hao wakatafute baba wengine kwa kuwa baba anampiga mama?
Hii sio sababu ya kutosha.

Alikuandikisha ada?
Yes, alikuwa sahihi hata mimi ningekuandikisha. Maana aliona husomeki umeanza kiburi kwa kuwa Umekutana na huyo mzee unayemuita baba mzazi.
Na kwa kuleta huu uzi hapa inathibitisha alikuwa sahihi, alichokihisi kinaenda kutokea.
Unataka kumkacha kisa " kula vizuri" mara moja kwa mwaka.

Unamuona huyo dingi ana upendo, kwa kuwa hujakaa naye. Ungekaa naye Ungemjua vizuri.
Hakumchukua mama ako wakati amefukuzwa kwao, alipomdanganya na kumpa Mimba.
Yote ya yote, maamuzi ni yako. Na nahisi ushayafanya hapa unataka kujustify tu.
 
Mkuu najaribu kueleza uhalisia, wala sipo hapa kumtetea baba mzazi na kumkandia baba wa kambo. Nashukuru kwa ushauri.
 
Baba yako wa kambo ndio jembe, alimchukua mama yako nakumstiri huku akijua wewe sio mwanae, akakulea mpaka ukahitimu chuo, pamoja na mama yako kuondoka nyumbani na kwenda kusikojulikana bado alikulea kama mwanae tena ukiwa wa kike...

Lipa fadhira acha ujuaji..
 
Mkuu najaribu kueleza uhalisia, wala sipo hapa kumtetea baba mzazi na kumkandia baba wa kambo. Nashukuru kwa ushauri.
Huelezei uhalisia.
Unajustify unachokifanya, na mimi nakueleza ukweli ambao unaujua ila huupendi.
Vaa viatu vya huyo dingi "wa kambo".
Uone anajiskiaje.
Nna uhakika watu walimwambia asioe Single mother, asikusomeshe, na maneno kibao.
Yet, hakujali alifanya anacho ona yeye ni sahihi.
Sa ivi nna uhakika ana kumbuka ushauri aliopewa kitambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…