Naomba Ushauri: Nisimame na Baba Mzazi au wa kambo?

Sina haja ya kutoa tena ushauri...Huyu jamaa hapa kashamaliza kilakitu.
1.Muheshimu sana mtu ambaye huna damu naye halafu akakusimamia katika maisha yako bila manyanyaso
2.Hao ndugu wa baba mzazi wanakushirikisha mambo yao kwasababu ushakuwa mkubwa na una kipato chako. Kipindi upo mdogo ulishawahi kuwaona wakikusaidia?
Achana na mambo ya baba mzazi, yeye mpe heshima yake kama mzazi wa damu tu.
Lakini mwenye kujua uchungu wa kulea ni huyo baba wa kambo, na siku ikatokea amepiga goti kumlilia mungu juu yako aisee machozi yake hayataenda bure.
Najua damu ni nzito kuliko maji na mtu kumfahamu na kumjua mzazi wako original ni suala la kujivunia.

Ila za kuambiwa changanya na zako "Mbayuwayu"
 
Kama jaribu kujigawa kwa kidogo walichonacho uwasaidie,wote kama wanahitaji msaada wasaidie kulingana na uwezo wazo,kitendo cha baba wa kambo kujitolea kumchukua mama yako na wewe basi sio kidogo
 
Nilivyo soma maelezo haya nimeumia sana tena sana.
Yaani ningekuwa nimeoa mwanamke mwenye mtoto ningefukuza huyo mtoto pamoja na mama yake na kesho wasingefika.
Samahani ila nina hasira sana na wewe yaani mtu akulee na kukusomesha umwite mshirikiana.
Vipi hao ndugu wa baba yako na baba yako walikuwa wapi kukushirikisha ukiwa upo shule?
Kuhusu kugombana na mama yako unataka kusema ugomvi ilikuwa sababu ni wewe?
Msomi alafu unaamini uchawi ambao huwezi kuthibitisha hopeless kabisa.
Je na wewe ukizaa mtoto mwenye ulemavu itakuwaje, naona wewe saivi umeanza kuenda kwa waganga ndio walio kuambia hata tatizo alilonano mdogo wako ni baba mlezi.
Wewe tuambie kuwa umemtenga maana hata watoto humwambii si hapo umemtenga tayari ila baba yako aliye kukimbia umemwambia wakati yeye hakukumbia kuwa yeye ni baba yako bali mjomba.

NGOJA NIKUULIZE SWALI

Hivi wewe unaweza kukubali hao watoto wako walelewe na baba mwingine ungali upo hai?
Ukijibu swahili hilo jaribu kufikiria kama baba yako anakupenda kweli.

NB mitoto ya kambo mingi ina akili kama za mtoa mada. Kama unailea kuwa tayari kukutana na matusi kama ya mtoa mada ili ujiandae kisaikolojia
 
Baba ni baba tu, damu yako.
Heshima kwa baba wa kambi nayo ni muhimu.
 
uwe na HEKIMA, umeshakuwa mkubwa....wote walikupenda.....heshimu UPENDO wao....wacha FIKRA za KIBAGUZI....
 
Mkuu pole sana ila unapitia kama ninayopitia mimi ila tofauti yetu ni kuwa mimi bimkubwa aliondoka miaka miwili imepita saizi anadai talaka kashafungua kesi me nimepewa kazi kumshawishi mama aachane na hilo jambo japo siwezi hukumu moja kwa moja makosa ni ya nan?
 
hii kitu ni rahisi sana anza kumuita baba mzazi ano kama mwanzo ...piah mjali sana baba wa kambo mlee kama alivokulea ww ....na mara moja kwa mwaka toka na baba mzazi mtoe out umnunulie msosi wa maana kama alivyokuwa anakufanyia ww.... ukiwa mdogo
 
Ukisikia binadamu hana shukrani ndio huku.Baba wa watu kakulea tangu mdogo wakati baba yako yupo anahangaika na familia nyingine huko.Embu muda mwingine tuwe watu wa shukrani.Baba yako ni mshirikina kwa hiyo hakukuloga miaka yote hiyo aje akuloge sasa?
 
Ada za shule alilipa nani?,baba mlezi au baba mzazi?
 
Sasa hao panya buku wanaotafuta malisho kwako ndio waliokulea jamaa
 
Nimegundua mliooa single mama mnamshawishi sana Kijana amtelekeze baba yake mzazi kisa ugali wa baba wa kambo hiyo haikubaliki wahenga wanasema baba ni baba. Kijana kua makini na wapotoshaji
 
Angalia ni nani kati yao ameonyesha kukupenda na kukujali wakati wote, huyo ndiye Baba.
 
sahihi
 
Hii kitu iliwahi Nikuta historia hazipishani Sana,,, wote wana umuhimu sana ila aliekuzaa is the best

Kuna ishu ilinikutaga halafu nikajikuta namuhitaji sana baba mzazi kuliko wa kambo japokua nimelelewa na baba wa kambo na baba mzazi nilimuweka kando kutokana na historia alionipa mother

Oyaaa wewe nilimuhitaji dingi mzazi kinoma halafu ndio alishafariki roho inaniumaga mpka Leo nilikua nakosea kumbagua haya maumivu yake hayajawah kufutika

Wote wana umuhimu ila damu yako is the best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…