Naomba ushauri wa biashara ya malori

Hapa naona ushauri wa aina 3. Kwanza ni wa madereva.. wanavutia kwao. Pili. Wakusikia.. hawajawahi kufanya hii biashara ya usafirishaji wa malori na kwa mbaali ... wenye malori wenyewe ambao wengi hawamo humu.
Mimi ni mmiliki wa malori na nimefanya zaidi ya miaka 20. Ushauri wangu... connect na wafanya biashara wenyewe... watafute mji ulipo uongee nao. Ukiwa dar au moshi au mwanza au mbeya kuna utofauti mkubwa sana wa kufanya biashara. Ushauri unategemea unaaanzia mkoa gani. Ipo miundo na mbinu nyingi na aina za magari, madereva, mafundi, Tra nk. Maombo ni mengi ila inalipa ukiipatia.

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Nimedadisi sana kuhusu hili, super single kwa maana ya trailer nimeambiwa inabeba mzigo mwingi kwa sababu trailer inakuwa nyepesi kulinganisha na trailer yenye double tires
Trailer ya mtumba ndio nyepesi lakini ukichukua hizi za kutengeneza ni nzito hata ikiwa single
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
Hesabu zako ziko sahihi kwako ila kwa mifumo ya biashara limekufa kabisa
 
Tuelimishe! ila kwa sasa walahi siwezi kuacha kuchezea Ardhi, Ardhi...[emoji8][emoji122][emoji122][emoji123][emoji106]
Unajua wengi tunawekeza tulicho Fanya utafiti

Mi sijawahi kumiliki roli ila nimeendesha pamoja na kusimamia

Ukiwa umepata gari nzuri Dereva mtunzani Fundi anae jua wajibu wake

Hii biashara utaipenda

Ili uweze kuifanya kwa Uhuru lazima kila Dereva awe na mkataba wa kazi utakao ondoa changamoto zisizo na ulazima kuwepo

Lazima uwe na msimamizi anae jua magari vizr

Hapo lazima utoboe
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
Sasa sote tuwe wakulima tena?
 
Sasa sote tuwe wakulima tena?
Ndivyo nilivyo shauri??!
Nimeshauri kwamba kama una Uwezo wa kuzishinda hizo changamoto Try [emoji106]
Kushindwa mimi sio kushindwa wote kila mtu ana Mbinu yake na Bahati Nzuri na Mbaya Yake!
 
Sawa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu hayo uliyotaja kwa ujumla mara aina ya gari, utofauti wa biashara kati ya eneo na eneo, sijui madereva n.k ndiyo mleta mada anahitaji ufafanuzi wa kina..

Ulivyotaja Kwa ujumla hujamsaidia bado!!!
 
Achana na hiyo biashara!
Kama utaziweza hizi changamoto try!
1-Ale dereva!
2-Ale msaidizi!
3-Ile gari!
4-Ile serekali!
5-Ale dalali!
6-Ale Trafic
Kitakacho fika kwako sound!....

Wekeza kwenye kilimo cha Kitaalamu!
kwa hiyo kwenye kilimo hauliwi?
 
Mkuu nakushukuru sana kwa ushauri wako. Bafo yote nakusanya kama maoni. Ahsanteni sana nyote
 
Mende ya mchanga haiwezi kukaa meza moja na semi kwenye kurudisha pesa .
1. ni gari ya gharama kuanzia manunuzi hadi service kwa sasa mende used ipo kwenye 120 plus , manunuzi tu
2. Ni gari ya msimu, kukinyesha mvua gari ya mchanga inapaki uani just like fuso tipper
3 njia inazopita mende za mchanga si rafiki kwa gari na vitu kama kuvunja diff springs, gearbox , crossmembers , center rubbers , chassis , boggies ni kawaida kwa tipper ya mchanga
Mende ni nzuri kama una project zako binafsi za ujenzi
 
Nimechelewa kuuona huu uzi ila nina imani.kuna mawili matatu naweza kukushauri....
Trailer , kwa kuwa unaanza kaa mbali sana na tela za supper singles, , si kweli kwamba zinabeba sana ila ni kweli nyingi ni nyepesi, swala la kubeba mzigo has a lot to do with axle configurations na sio wepesi wa tela,
Double tyte with steel suspesnion ni chaguo bora kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…