Naomba ushauri wa biashara ya malori

Naomba ushauri wa biashara ya malori

Ahsante kwa ushauri wako. Nimeshanunua horse
Umenunua horse aina gani, na vipi perfomance yake?tupe feedback ya changamoto au new lessons yeyote uliyopata.

Mimi pia nataka kununua horse, nawaza kati ya benzi mp3 au daf xf 106 manual gear, au zote kwa pamoja, nichanganye brand mbili
 
Kachumbari kwenye biashara ya magari haishauriwi sana !!
Kuwa na brand moja , ili mambo yakiwa magumu uweze kutumia gari moja kama spare .
Manual gear ?? Sikushauri kabisa!!
 
Umenunua horse aina gani, na vipi perfomance yake?tupe feedback ya changamoto au new lessons yeyote uliyopata.

Mimi pia nataka kununua horse, nawaza kati ya benzi mp3 au daf xf 106 manual gear, au zote kwa pamoja, nichanganye brand mbili
Gari ndio iko bandarini inafanyiwa clearance.
Kutokana na changamoto za meli kutoka ulaya kwa kipindi hiki imenichukua muda sana gari kufika maana nimeagiza in mid June.
 
Mosi , Safety features zipo advanced sana kwenye auyo box kuliko manual box

Driver comfort, auto box inafanya kila kitu na driver anapunguziwa majukumu , maana yake ni kuwa atadrive kwa kurelax
Manua box zinakuwa phased out huko duniani , kabaki mchina tu .
Uliyoyasema ni kweli. Kuna ule udereva wa kizamani wa.kung'ang'ania manual gear trucks, ama kuendesha gari ngumu 113, 114 huu kweli umepitwa na wakati katika dunia ya sasa.
 
Umenunua horse aina gani, na vipi perfomance yake?tupe feedback ya changamoto au new lessons yeyote uliyopata.

Mimi pia nataka kununua horse, nawaza kati ya benzi mp3 au daf xf 106 manual gear, au zote kwa pamoja, nichanganye brand mbili
Soma update kwenye uzi utajua nimenunua gari aina gani.
 
Nimeamua kununua iwe yangu kabisa maana hii ya kukodi ningekuwa nampa mtu kama Milioni kwa mwezi.
Za kukodi naweza pata nifanye route za mikoa?

Inaaeza fika ngapi kukodi horse? Na trailer?

Msaada
 
Mosi , Safety features zipo advanced sana kwenye auyo box kuliko manual box

Driver comfort, auto box inafanya kila kitu na driver anapunguziwa majukumu , maana yake ni kuwa atadrive kwa kurelax
Manua box zinakuwa phased out huko duniani , kabaki mchina tu .
Hivi hadi hizi tipper/dumper ambazo ni auto zipo kweli bongo hii kwa hizi brands pendwa za Mitsubishi?
 
Wakuu nawasalimu kwa Jina la JMT.

Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Nimekuja humu ndani kupata ushauri wa Biashara ya Malori haya ya kubeba mizigo iwe ya Local ama Transit.

Kutokana na Connection nilizonazo nadhani suala zima la kupata Mizigo ya Kusafirisha halitokuwa la kuumiza kichwa.
Changamoto inayonikabili ni funding pamoja na aina ya truck ambayo inapaswa ni nunue.

Kabla ya kuja humu ndani nilishaomba ushauri kwa watu kadhaa ambao wapo kwenye hii industry na wamenijuza truck nzuri ya kununua ni Mtumba SCANIA 124 420 iliyotumika Europe. Hawakunishauri kabisa kununua Truck Mpya ama Refurbished za Mchina, DAF na Volvo wakaniambia zitanitesa maana ndio kwanza naingia kwenye game. Hata nilipouliza SCANIA zilizotumika south Africa wakaniambia ni bora nichukue za europe zinakuwa bado zipo Bora na hazijatembea sana kwenye rough road kwa hizo za SOUTH japo hizo za south walikiri kwa gharama ya manunuzi zipo chini kiasi.

FUNDING
Kama nilivyoeleza awali mimi ni new comer kwenye hii industry hivyo nategemea kujichanga kama 50-60Mil then the rest nichukue mkopo maana nakopesheka vizuri sana. Baada ya kufanya window shopping nimegundua horse scania mtumba inaweza kunicost kati ya 75Mil - 85Mil hapa nitapata gari nzuri tu, Trailer nimeshauri kununua ya Mkononi ambayo imetumika hapa nchini ambapo zina range 25Mil - 30Mil kutokana na hali yake. Nimejaribu kuulizia. Mpya lakini naona bei imechangamka sana USD 28,500.00 flatbed Double tire

TECHNICAL
Nimeshauriwa hapo kwenye trailer kununua super single kwa maana inabeba Mzigo Mkubwa kulinganisha na trailer yenye double tire.
Kwenye Horse kama nilivyoeleza awali nimeshauriwa SCANIA 6x2 124L 420 Mtumba kutoka EUROPE

BUDGET
Ukiangalia makisio ya gharama zote Horse na Trailer budget yake inacheka kati ya 100Mil - 115Mil. 60% Nategemea kuitoa Mfukoni na 40% nichukue Mkopo. Nategemea kulipa Mkopo kwa kutumia Mshahara wangu pamoja na Mapato yatakayokuwa yanapatikana baada ya Truck kuanza kuoperate. Nimekuja kuomba ushauri kwa yeyote mwenye kuielewa biashara hii kwa undani, nimeweka mchanganuo wote hapa ili niweze kupata ushauri mzuri kulingana na information nilizopokea pamoja na uwezo wangu wa kifedha. Nategemea kuna wajuzi wengi humu na nitaambulia ushauri mzuri katika kukamilisha hili. Ahsanteni na niwakaribishe kwa Ushauri. Kejeli na dharau hapa si mahala pake.

UPDATE: Baada ya Ushauri wa Kina na kuchuja yote niliyoelezwa. Nimefikia uamuzi wa kuagiza Scania G420 kutoka Uingereza. Nimeachana na gari za kizamani 113, 124 kama wengi walivyoshauri. Wakati nikisubiria Gari ifike napambana na kutafuta trailer. Nimefuatilia Weight Limits za TANROAD naona Super Single na double tire trailers zote zimepewa uzito sawa wa 24MT kwa axle tatu za nyuma. Hii ina maana kuwa kwa kuwa super single ni nyepesi basi itabeba mzigo mwingi. Najua maybe nitakuwa sipo sawa kwenye hili, nipo tayari kurekebishwa kwa mwenye ujuzi zaidi.

Lingine linalonitatiza, trailer ya booster na ya spring ipi ni bora. booster inahitaji service nyingi kuliko spring. lakini pia booster ikiharibika ni lazima itengenezwe hapo hapo ndio safari ianze. Wajuzi naomba nimerudi tena kwenu kuomba ushauri mzuri kwenye trailers. Ahsanteni

UPDATE 2:

Nimefanikiwa kupata Trailer mtumba ya mkononi ambayo imerekebishwa. Najiandaa kupokea Scania Horse ambayo mpaka kufikia mwisho wa mwezi ujao itakuwa imefika na kutoka Bandarini.

Estimated Budget kwa Horse na Trailer hadi hapa ni 120m. Na hapo nimepambana sana. Kumbuka tela nimenunua mkononi ya double tire spring ambayo imekarabatiwa. Horse nimeagiza mtumba UK. Ahsanteni
Umefanya vzr sna mkuu mm nitakiwa manager wako mnk ni.ekuwepo ktk kampuni fln hv so hayo magari nazijua a to z

113,114c,124_420 nazo pia ninazimudu kuanzia spare na kila kitu

Ila nikutonye kama upo dsm basi nenda pale fire mwanza spare karbu na kfc mgahawa kanunue spare zako kwa bei resonable kbsa
 
Cummins ni engine ya kimarekani ,wakati europeans wanaingia tier 3, emissions control , manufacturers pekee aliyekuwa na nozzle simple ku meet euro 3 standard alikuwa ni Peugeot(France) na tech yake ya unit injector , 'pump duce ellementer' (PDE)
Truck manufacturers waliopoona wangekuwa nje ya standards wakaamua kwenda kununua tech hii kwa mfaransa , kwa masharti kwamba neno PDE liwe ni lazima kuwa included kwenye kila engine itakayo tumia tech hiyo kama copyright za france tech
Miongoni wa watengenezaji walolipa kutumia tech ya PDE alikuwa ni cummins , volvo , scania etc na nozzle hii wote walienda kutengeneza kwa Bosch germany. Bosch alichofanya alitengeneza nozzle hii kwa stlye na dimensions moja akaja kutofautisha juu tu kutokana na cam na valve configuration kwa gari husika .

Cummins ilikuwa ya kwanza kuja Tanzania nyingi zilikuja kama gensets , mafundi wakakariri nozzle , ilipokuja 124 420 na unit injector mafundi wakaibatiza scania Cummins.
Kaka nimerejea Tena kuuliza swali.

Kuna hizi scania 114 380 nimekutana na Euro 2 ambayo ni ya mwaka 2001 pamoja na 114 380 Euro 3 ya mwaka 2003. Je, hizi zote ni Cummins engine? Je, nikikutana na neno PDE ndio ishara ya hiyo gari Ina Cummins engine kwenye scania? Je, kinachotofautisha hasa kati ya Cummins engine na engine ya unit injector kwenye performance ni kitu gani hasa. Ahsante Kwa ufafanuzi

Hapo chini nimeweka trucks mbili zote ni 114 380. Yenye maandishi ya PDE ni ya mwaka 2003 na ni Euro 3. Isiyokuwa na maandishi ni Euro 2 ya mwaka 2001. Kati ya hizi Ipi ni nzuri?
Nashindwa kujua Ipi ni Bora na Ipi ni Cummins maana Kuna mdau huko juu alisema tununue ya mwaka 1997 hadi 2001. Lakini hii Miaka sidhani Cummins engine zilikuwa zimeanza.

Ahsante Kwa ushauri wako.
View attachment 2560958View attachment 2560959
Cc
t blj
cannulla
mlima wa mizeituni
 
Neno Pde ni trademark ya ufaransa, ikiwa ni abbreviation ya neno "pompe duce ellemente" au unit injector kwa English. Wakati euro three inakuwa mandatory europe , Peugeot france ndo walikuwa na pde tech na ni moja ya tech ambayo ilionesha kufaulu euro 3 emissions regulations. Kwa gharama nafuu. Scania na Cummins walinunua hii tech kutoka france , na wote wakaenda kutengenewa nozzle ( unit injector) kwa bosh diesel( USA, branch) Cummins imekuwa popula kwa sababu bosch walitengeneza nozzle hizi USA ndo akawa wa kwanza kuzipata , scania yeye alipata baadaye..
114 kabla ya 2001 zilikuwa ni mechanical pump, kuna ambazo zilitengenezwa na kampuni ya zexel, zipo za bosch pia , to the best of my knowledge gari zenye mechanical pump hazijawahi kuwa na maisha marefu kama gari ya unit injector, ni mafundi walikuwa wanogopa gari za umeme ,ila siku hizi wameshazizoea, nakushauri nunua gari ya pde ,
 
You have said it all. Ahsante sana mkuu
 
Gari za EU au Scandinavia huwa ziko well spec'd na zinakuwa hazijatembea sana, tatizo ni LHD.
Mind set tu ya dereva! Nimesha endesha LHS shacman H3000 nilijisikia raha sana! Wabongo waaribifu kuzibadili mfumo
 
Mind set tu ya dereva! Nimesha endesha LHS shacman H3000 nilijisikia raha sana! Wabongo waaribifu kuzibadili mfumo
Mkuu, kwahyo unachoshauri ni kutozibadili kuwa RHS? Je, hazitowasumbua madereva hususani kwenye suala zima la kuovertake?

Kuna mdau huko juu alisema ni muhimu dereva wa RHS kupata somo jinsi ya kuendesha LHS. Je, wewe ulipata hilo somo? Je, ni kweli Kuna huo umuhimu?

Raha uliyojisikia ni Ipi hasa, unaweza kuelezea japo kidogo?
 
Mkuu, kwahyo unachoshauri ni kutozibadili kuwa RHS? Je, hazitowasumbua madereva hususani kwenye suala zima la kuovertake?

Kubadilisha mfumo gari hua hiaitulii tena kama ilivyo kuja au kama ilivyotakiwa iwe, pia mafundi wetu ni careless, wanafungatunga ilimradi itoke, steering box lazima ubadili, hapa ndipo unapo anza uharibufu! Unayoifungua na unayo uziwa uifunge hua hali zake hazifanani, kuna gari wameifunga juzi hapa inasumbua vibaya ni mwendo wa kutembea na makopo ya hydraulic fluid, ma pipe ni vululuvululu! Una muuliza mtu sababu ya kuharibu gari hivi ni nini wakati gari imekuja mpya na haina tatizo lolote!? Jibu madereva wanasumbua lazima wabadilike badilike hivyo kuwapata wa left ni ngumu,. Tayari unaona mind set ya tajiri mwenyewe ni kipusa! Tafuta dereva mzuri ishi nae vizuri, hua ni kazi sio adhabu, tengeneza misingi ya kutegemeana sio kutumikishana, madereva cheap ndio wanao ua magari hata liwe RHS

Kuna mdau huko juu alisema ni muhimu dereva wa RHS kupata somo jinsi ya kuendesha LHS. Je, wewe ulipata hilo somo? Je, ni kweli Kuna huo umuhimu?

Udereva ni wito mbali na fani, kuna mtu yupo tu udereva kwasababu hamna kingine cha kufanya ila kuna watu wana dream kua driver kutoka wadogo, watu hawa wawili ni tofauti kabisa, na utawajua padogo sana, kwanza uendeshaji wa gari yenyewe, maamuzi yao barabarani, utunzaji wa gari, na utendaji wa kazi yenyewe!

Elimu kubwa ni mind set tu, kwanza ajitambue na ajue anafanya nini akiwa barabarani, LHS aihitaji dereva wenge au waruwaru kwenye barabara za hapa kwetu, ishu za ku overtake si kwa LHS bali ni kwa gari zote, swala hilo hua linahitaji mahesabu yaliyo kamili haswa kwa gari kubwa pia inakutaka uwe mtu wa subira sana sio kukurupuka

Raha uliyojisikia ni Ipi hasa, unaweza kuelezea japo kidogo?

Raha sana nilikua najisikia tofauti sana! Wewe unamuonaje dereva anaeshuka kwenye gari ya LHS
 
Raha sana nilikua najisikia tofauti sana! Wewe unamuonaje dereva anaeshuka kwenye gari ya LHS
Ahsante sana Kwa mchango wako kaka.
Kuhusu Mafundi wa Kibongo ni kweli aiseeee. Yaani gari ikienda garage Kwa ajili ya Corrective maintenance ni ngumu kurudi kwenye Hali yake ya mwanzo. Nimeshaexperience hili jambo.
 
Back
Top Bottom