Mkuu, kwahyo unachoshauri ni kutozibadili kuwa RHS? Je, hazitowasumbua madereva hususani kwenye suala zima la kuovertake?
Kubadilisha mfumo gari hua hiaitulii tena kama ilivyo kuja au kama ilivyotakiwa iwe, pia mafundi wetu ni careless, wanafungatunga ilimradi itoke, steering box lazima ubadili, hapa ndipo unapo anza uharibufu! Unayoifungua na unayo uziwa uifunge hua hali zake hazifanani, kuna gari wameifunga juzi hapa inasumbua vibaya ni mwendo wa kutembea na makopo ya hydraulic fluid, ma pipe ni vululuvululu! Una muuliza mtu sababu ya kuharibu gari hivi ni nini wakati gari imekuja mpya na haina tatizo lolote!? Jibu madereva wanasumbua lazima wabadilike badilike hivyo kuwapata wa left ni ngumu,. Tayari unaona mind set ya tajiri mwenyewe ni kipusa! Tafuta dereva mzuri ishi nae vizuri, hua ni kazi sio adhabu, tengeneza misingi ya kutegemeana sio kutumikishana, madereva cheap ndio wanao ua magari hata liwe RHS
Kuna mdau huko juu alisema ni muhimu dereva wa RHS kupata somo jinsi ya kuendesha LHS. Je, wewe ulipata hilo somo? Je, ni kweli Kuna huo umuhimu?
Udereva ni wito mbali na fani, kuna mtu yupo tu udereva kwasababu hamna kingine cha kufanya ila kuna watu wana dream kua driver kutoka wadogo, watu hawa wawili ni tofauti kabisa, na utawajua padogo sana, kwanza uendeshaji wa gari yenyewe, maamuzi yao barabarani, utunzaji wa gari, na utendaji wa kazi yenyewe!
Elimu kubwa ni mind set tu, kwanza ajitambue na ajue anafanya nini akiwa barabarani, LHS aihitaji dereva wenge au waruwaru kwenye barabara za hapa kwetu, ishu za ku overtake si kwa LHS bali ni kwa gari zote, swala hilo hua linahitaji mahesabu yaliyo kamili haswa kwa gari kubwa pia inakutaka uwe mtu wa subira sana sio kukurupuka
Raha uliyojisikia ni Ipi hasa, unaweza kuelezea japo kidogo?