Naomba ushauri wa namna ya kupata haki kuhusu hii simu ya wizi iliyopo polisi

Naomba ushauri wa namna ya kupata haki kuhusu hii simu ya wizi iliyopo polisi

chagga_daddy

Member
Joined
Dec 14, 2019
Posts
16
Reaction score
9
Habari Wana jukwaa...

Kuna rafiki yangu kauziwa simu ya wizi yeye alinunua huko Makumbusho polisi wameitrack wakamkamata ila akawapeleka aliponunua wakamkamata pia aliyemuuzia wakaenda kumweka ndani ili aseme kaipata wapi ndipo akawapa number za aliyemuuzia.

Wakamfatilia wakajua yupo Mtwara ila shida inakuja kwa huyu rafiki yangu Polisi wameshamtoza tena hela za kwenda kumfatilia huyo mtuhumiwa number moja wakati yule aliyemuuzia wamemkamata ndio angetakiwa kuwajibika sio huyu rafiki yangu tena

Maana yeye kanunua tu na kingine WANATAKA tena laki Tano eti naye alipe ili kulipa vitu vilivyopotea na hiyo simu wakati huo kashawapa laki 3 za kumfuata huyo mtuhumiwa huko Mtwara na simu alinunua milioni 2

Je, wadau afanyaje kuipata haki yake maana mimi naona wanamlia hela wakati kesi ahusiki tena.

MAONI YENU PLEASE.
 
Kuna rafiki yangu kanunua simu ya wizi police wamemkamata akawapeleka alipouziwa wakamkamata aliyemuuzia wakamuweka ndani awaoneshe aliyemuuzia simu.

Kumbe aliyemuuzia uyo dalali simu yuko Mtwara Cha kushangaza police wamemwambia rafiki yangu achange HELA Tena laki 3 eti wakamkamate uyo aliopo Mtwara akawapa.

Wamemtaka Tena aliepe laki Tano eti kufidia vitu vilivyopotea na simu wakati mtuhumiwa aliyemuuzia yupo wanaye

Naombeni ushauri wadau apate aki yake simu alinunua million 2 iphone.
 
Back
Top Bottom