Naomba ushauri wa namna ya kupata haki kuhusu hii simu ya wizi iliyopo polisi

Nikituo gani nione namna ya kukusaidia?
AAss
Asante mkuu
 
Serikali inakosa pesa ya kuripa per diem zao?
 
dunia ya sasa ni hatari sana kununua vitu mkononi.
 
Hiyo yote michongo,na police wamo kwenye hiyo michongo.
 
Mwambie rafiki yako na wewe muache ujinga. Ukitaka simu nenda dukani, nunua simu upewe na risiti. Jf haishauri wezi.
 
mmmh jaman maduka ya simu tele bado watu mnanunua za magendo
 
Ndo mjifunze sasa yeye dukani apajui hio laki nane aliyowapa police still bado zitamtoka si angepata iphone
 
Aliyemuuzia wanae sa kwann bado WANATAKA alipe Hela za vitu vilivyopotea na ajajua atma ya Hela yake mkuu
Atalipa kwa zamu yake Acha wamfilisi kwanza huyo rafiki yako.
Hakuna msaada wa kisheria hapo mwambie akubali tu kulala na chupi.
Muuzaji na mnunuzi wote kesi moja ya umiliki wa mali ya wizi.
 
Wewe na rafiki yako wote wapuuzi

Mnanunuaje simu yenye thamani Kama hyo kwa mtu Tena bila risiti

Mpigwe TU labda mtabadirika kiakili

Mil 2 n nyingi Sana kununulia simu Tena mkononi hamkujar usalama wenu kabisa
Na tena kama ni simu ya bei police wanajua pesa ipo
 
Wanakulaga kotekote, kwa aliyeibiwa simu, kwa aliyeiba na kwa aliyenunua. Wataendelea na kamchezo hako wala hawamwambii aliyeibiwa kuwa imepatikana
Pia ipo michezo unauziwa simu kisha muuzaji anaenda ripoti police unapatikana unaliwa kotekote kwa kupigwa kesi ya wizi au mauaji kupitia simu uliyonunua.
So ukifikiria miaka 30 au maisha jela lazima uuze nyumba Ili washinde bar.
Hadi wakufilisi
 
Uwezo wa kulipa simu 2M upo cha ajabu mnashindwa kupata wakili wa 500,000 tafuteni mwanasheria aende kuongea na mkuu wa kituo.
Wabongo tunapenda sana sifa, yaani mtu anataka kumiliki simu ya million 2 kilazima hata kama uwezo wake ni wa chini.
 
Police wa kitengo cha syber ni wezi sana
 
Wanakulaga kotekote, kwa aliyeibiwa simu, kwa aliyeiba na kwa aliyenunua. Wataendelea na kamchezo hako wala hawamwambii aliyeibiwa kuwa imepatikana
Hahahaaa..na alieibiwa watamuuzia na sio kumrudishia!
 
Pia ipo michezo unauziwa simu kisha muuzaji anaenda ripoti police unapatikana unaliwa kotekote kwa kupigwa kesi ya wizi au mauaji kupitia simu uliyonunua.
So ukifikiria miaka 30 au maisha jela lazima uuze nyumba Ili washinde bar.
Hadi wakufilisi
Sipendi kbs ukaribu na urafiki wa polisi mimi. Wajinga mno maisha yao ni kudhulumu tu wenzao.
 
Watanzania wengi ni wapumbavu sana.


Una milioni 2 unaenda kununua simu ya mkononi??????



ACHA ALIWE ILI APATE AKILI TIMAMU.
 
Ohooo,hapo huyo aliyepeleka malalamiko,aliyemuuzia jamaa na polish wote lao moja amini nakuambia wanajuana hao kama vipi we angalia mlango mwingine tu
Ni kweli, Kwa simu za iPhone mlalamikaji, muuzaji na hao Polisi ni kitu kimoja kwenye huo mchezo, hao wote ni matapeli.
 
Haya ndio madhara ya kutaka kumalizana polisi.
Huyo ndugu yako awatake wapeleke kesi mahakamani vinginevyo ataliwa pesa sana na kesi iko pale pale.
Na pia aache tamaa. Amenunua IPhone ila mpaka mwisho atatoa pesa ya simu ingine nawisho atakuwa hana simu bado.
 
Angeachana nayo tu, polisi watamla mpaka wamle yeye mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…