Naomba ushauri wako juu ya kipi nifanye kwa hiki kilichotukumba kwenye ndoa

Mkuu wewe unaonekana ni mtu unayejali sana familia yako, ni jambo jema na hongera kwa hilo. Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu as long Mungu ameruhusu hiyo mimba jua mlango wa Mafanikio na Baraka zitandamana naye so usiruhusu hofu, mtie moyo wife na play your role as a husband & father.
 
Mkuu haya maisha ni yako, hata siku mmoja usiwaze kuhusu watu wengine watawaonaje, by the way hamna anayejali kuhusu wewe na familia yako. Ni hisia tu ambazo unatakiwa kuzitawala.
 
Yaani umri huo Kaka mkubwa mnadinyana alafu mnaogopa kupata mtoto wa tano ,hapa naona unatamani tukushauri muitoe hiyo mimba Ila Mimi nakushauri msitoe mimba ,lea huyo kiumbe akikuwa fungeni uzazi hiyo ni mistake mshaifanya kubalini uhalisia tu .
Kwa huo umri bado wadogo sana, hata wa sita anawezekana.
 
Ujumbe murua mkuu
 
Ushauri maana yake unapata mawazo yatakayokusaidia (enlighten you) kufanya uamuzi sahihi na siyo mawazo utakayotumia kwenye uamuzi wako. Kwa upande, wangu badala ya ushauri nashangaa kwamba "hukuwa tayari kumpokea mtoto ambaye mmejaliwa kumpata". Ujue hata kama utamficha atakuja tu kujua reaction yako na itamuumiza sana. Unaweza kuwa na reaction kama hiyo kama unajua kama mtoto si wako, lakini kama ni wako, nasikitika sana na najiuliza kwa nini ulikuwa na hiyo reaction. Kuna familia moja walizaliwa watoto 17, kwa sasa wameshabaki 3 tu. Kama wazazi au mzazi mmojawapo angekuwa na mawazo kama yako, angefurahi au angehuzunika? Nakuachia hilo swali.
 
Mimba Ina muda gani?

Kama mko tayari, leeni mimba, mtoto azaliwe.

Kama hamko tayari na kamimba ndo kako mwezi wa kwanza, bado sana hiyo, ni vinyamanyama tu. Katoeni muendelee na maisha.

Wengi tu humu wametoa mimba/wamelazimisha wenza wao kutoa mimba ila hapa watajifanya hawaijui hiyo option.
 
We chizi nini, sasa una ushauri gani unataka, ulipiga pipe, basi pokea hiyo mimba kwa mikono miwili, mengine pambana kiume, iwe ni bajeti ama gharama za maisha pambana kiume.. Ya mungu mengi ya kuku mayai we unajiwekea hao wa4 unahakika ndio hao hao watakuwa moaka uzeeni mwako kama utafanikiwa kuwa na umri mrwfu, usishangae keshokutwa wa4 wako wanapata ajali wanakufa(siombei likukute, mungu akuepushie mbali) unabaki kuiombea dua mimba usiyoita

Mimba ishakuja we lea akizaliwa mtoti hewala, mimba ikiharibika yenyewe hewala lakini usiwe kwenye majuto kw avitu vya baraka kama hivyo.
 
Nimekuelewa mzee japo umenifokea sana na vitisho juu, ila nimekupata 😅
 
Mkuu haya maisha ni yako, hata siku mmoja usiwaze kuhusu watu wengine watawaonaje, by the way hamna anayejali kuhusu wewe na familia yako. Ni hisia tu ambazo unatakiwa kuzitawala.
Sawa mkuu. Hil nalo ni la kwel, inawezekana najishtukia tu bila sababu za msingi
 
Ahsante sana mkuu. Nashukuru
 
Usiwe na bias na children gender mtoto ni mtoto
Ni sahihi kaka. Kwa hili sina shida nalo. Maana kwa dunia ya sasa malezi ya watoto changamoto yake haibaguibwa kike wala wa kiume. Tofaut na zamani. Hili sina tatizo nalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…