Naomba ushauri wako juu ya kipi nifanye kwa hiki kilichotukumba kwenye ndoa

Tamthilia zinatuharibu,watoto watano tu mnalia na kununiana,mwenzio nina watoto saba,kwetu tulizaliwa kumi na maisha yanasonga,relax
Ahahahahah...sio tamthiria kaka mkubwa. Ni mshtuko tu kinyume na mategemeo.
 
Japo hujasema ila inaoneka kuna kitu zaidi ya uliyoyasema kwenye uzazi wenu kwasababu sioni sababu ya nyie kuwa frustrated na suala la mimba wakati mmeshapitia hiyo stage mara nne kwahiyo mna uzoefu wa kutosha.
Tafuta siku nzuri mkae na mkeo mzungumze mkishawekana sawa ombeni toba kwa Mungu kwasababu mmekosea kunun'gunika kwa kiwango hicho. Then jiandaeni kumpokea mtoto wenu mzuri mtakaempata na tafuteni jina litalokuwa na ushuhuda kumhusu.
Kila la heri
 
Ilinitokea mm pia, miaka kadhaa iliyopita, kidogo tuitoe ile Mimba ila baada ya kuwaza tena na wife tukaona hii zambi itatutafuna miaka yote ya maisha yetu hapa duniani, hakuna namna ilibidi kukubaliana na hali tu, mtoto kuzaliwa kafanana na mm kuliko wote waliopita, dogo now yuko shule afu kana akili sana, M/Mungu amjalie sana, Leo namtazama nafsi inanisuta kiaina.
Nikupe moyo, ni mipango ya Mungu, huwezi jua,
Nb: njia za uzazi wa mpango ni muhimu ile ya kalenda ni bahati nasibu.
 
Ongera sana kwa kuongeza familia mkuu, usiwaze mtalaamu suala la kupata ujauzito wife wako ni jambo la heri kabisa labda kama ana changamoto ya uzazi ambayo ndio inawafanya muwe na msongo wa mawazo, ila mtoto ni baraka mpokeeni kwa mikono miwili
 
Nashkuru chief, ni kwel sikutaka kuandika kilankitu kuepusha kuwachosha watu na mambo mengi ila nitazingatia ushauri wako
 
Kikubwa kubaliana na hali mpokee mtoto anayekuja.shangaa huyo akawafaa uzeeni make hakuna ajuaye ya mbeleni
 
Haya mambo haya mimi kalenda ilinisaliti mpaka mr akaanza kusema au umenibambikizia,kwanza mtoto alikuwa bado mdogo sana jamaa alipanic akasema tuitoe,mi nikamwambia sina mpango huo hata sir God hawezi kunielewa,badae akarudi kwenye mstari mambo yakawa sawa tu.
 
Nakazia hapa.

Nyie hamkupanga lakini Mungu alipanga kua huyo mtoto lazima azaliwe wakati huo.

Nakumbuka mimi na wife tulipitia stress kidogo baada ya mimba ya mtoto wa pili kuingia wakati wa kwanza bado hajakua vizuri.

Tuliamua kutomwaga damu, isitoshe watoto ni zawadi, tukakubaliana nalo, na Mungu mwema safari ya miezi tisa tumeimaliza.

Hakikisha unakua karibu na mke wako, muonyeshe upendo mkubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…