Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Mkuu niumepanga katika hili zoezi nishiriki mwenyewe pia kwa asilimia 120% sitaki ufugaji wa kupiga simu. Pia nilitaka nipate japo heka 2-5 ambapo humo naweza kufanya shughuli zingine za kilimo.

Japo sijui kulima ila nitajulia huko huko. Huko nilitamani niwekw mbuzi na mifugo mingine kama. Oink oink

Hapo sasa unataka kuharibu.
Kuku na 'hayo madude' sehemu moja?
Hapana sikushauri.
 
mkuu soma kwa makini comment no 09 amepiga mle mle

cha kuongezea hapo usitegemee chakula cha kununua pekee vyakula vingine tengeneza wewe mwenyewe maana katika ufugaji wa kuku chakula ndo mziki ulipo kwa eneo hilo ukiwa nalo hakikisha mchicha unao,chinise nk vilevile kama upatikanaji wa maji utakuwa mzuri fanya kuozesha kinyesi chao kwa ajiri ya funza wadudu hao wana protein za kutosha

hakikisha kiangazi unatengeneza hydroponic folder zitakupunguzia sana gharama.

usisahau kutupa mrejesho
Naomba mtuelekeze namna ya kuandaa chakula cha kuku tafadhari
 
Habari!

How much are u willingly to invest in this business.

Kama uko na hela ya kutosha hakuna sababu ya Kuanza na kuku 100 sijui 200, Unaweza anza na kuku hata 3000+ kwa ushauri wa Wataalamu n ww kuingia kitabuni.

Binafsi nina uzoefu mkubwa wa kusimamia mashamba ya kuku wa mayai/Broiller kama mtaalamu, so kua free kuuliza chochote.

Nimekuekea hapa budget ya kuku 260, Kwa kipindi cha day 1 - wanaanza kutaka unaweza ipitia kama muongozo
View attachment 2942972

Oh yeah!!
Umesema umesimamia mashamba mengi ya ufugaji wa kuku wewe ukiwa kama mtaalamu..

okay swali langu kwako ni liko hapa kwenye management of one day chick up to laying time.
 
Kama ni eneo kubwa unafuga bila shida weka tu uzio tafuta na vijana wa kukusaidia wenye uzoefu hata ng'ombe wa maziwa kama ni sehemu yenye uhitaji wanalipa sana muhimu upate elimu ya kutosha ya ufugaji na ujitoe
📌📌📌📌.
Hasa kwenye ng'ombe hapo...
 
mkuu soma kwa makini comment no 09 amepiga mle mle

cha kuongezea hapo usitegemee chakula cha kununua pekee vyakula vingine tengeneza wewe mwenyewe maana katika ufugaji wa kuku chakula ndo mziki ulipo kwa eneo hilo ukiwa nalo hakikisha mchicha unao,chinise nk vilevile kama upatikanaji wa maji utakuwa mzuri fanya kuozesha kinyesi chao kwa ajiri ya funza wadudu hao wana protein za kutosha

hakikisha kiangazi unatengeneza hydroponic folder zitakupunguzia sana gharama.

usisahau kutupa mrejesho
hydroponic fodder ni project inayohitaji fedha kwanzia green house, seeds ,wheat.... nk ,nutrients,trey za kupandia,maji,usimamizi so mi ningemshauri afocus kwanza na ufugaji wa kuku kwa kutumia home made ration...

baadaye akiexpand mradi ndio awaze kuhusu hydroponic fodder.

Maggots pia ni wazuri kwa kulishia kuku so nakubaliana na wewe.
 
Oh yeah!!
Umesema umesimamia mashamba mengi ya ufugaji wa kuku wewe ukiwa kama mtaalamu..

okay swali langu kwako ni liko hapa kwenye management of one day chick up to laying time.
Ntajitahidi kufupisha maelezo.

1.Zingatia mazingira ya Joto. Hapa watanzania wengi hutumia vyungu vya joto kulea vifaranga kwa week 2 - 3 kutegeme na msimu wa joto au baridi. Kawaida chungu kimoja kinalea kuku mpaka 100. Lakini pia kuna taa maalumu za joto zinauzwa kwenye maduka ya Mifugo.

2.Zingatia chanjo, Siku ya kuchanja kwa kawaida siku ya 7 tunachanja chanjo ya ugonjwa wa kideri, siku ya 14 tunachanja chanjo ya ugonywa wa Gumboro, siku ya 21 unarudia kideri, na siku ya 28 unarudia gumboro, siku ya 35-42 unapiga ndui/Fowlpox siku ya 60 unawapa dawa ya minyoo. Baada ya hapo utakua unarudia Chanjo ya kideri na Dawa ya Minyoo kila baada ya miezi 2.5 - 3 kutoka kwenye tarehe ya mwisho ya kuchanja

3.Zingatia chakula bora, katika kipindi cha miezi 2 ya kwanza kifaranga anagakiwa apewe chakula bila kupimiwa, angalia kampuni nzuri ya chakula cha kuku wa mayai inayo patikana mahali ulipo. Aina ya chakula wanachokula ni Chick starter kwa miezi 2 ya kwanza, Grower mash mwa miezi 2.5 inayofuata, then Layer mash wakiaanza kutaga kwa asilimia 5

4.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya maji chakula.

5.Zingatia Biosecurity, hapa nimekosa kiswahili kizuri, hakikisha unazui kuingia hovyo kwa watu shambani kwako, hakikisha unabadirisha viatu unapoingia bandani kwako, hakikisha unakua na makoti special ya kuvaa bandani.

Maelezo mengine, unaweza angia pdf nimeshare hapo juu kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai. Kuna no. zangu za simu kama ungependa maelezo zaidi
 
Back
Top Bottom