Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Katika aina zote unazofuga ni aina ipi inakupa faida nzuri kuliko zote?
Kuroiler. Mayai yake ni ghali ukilinganisha na layers na pia sio wasumbufu kwenye kufugwa. Chakula chao pia ni rahisi wakishavuka ile hatua ya vifaranga.
Tofauti na layers chakula chao ni special mfuko ule elfu 50 na bado wanakula sana na mayai yao ni bei chee tu.
 
Mkuu nipm basi unipe elimu tafadhali.. Mm siwezi pm mtu.
 
Changamoto ya Banda langu ni hewa ndogo, lkn Hawa niliwafunga ili niwuze sikuku, ya Pasaka na Eid, Hawa walikua 300, lkn wamekufa 24 mpaka Sasa. Nikiwatoa week mbili zijazo ntafanya maboresho ya Banda, na pia niendelea kufanya extension ya Banda Kwa ajili ya ku accommodate kuku wengi Zaid.

Ingawa pia na Banda lingine lenye kuku wengi zaidi, nilianza ufugaji mwakajana, changamoto ninyingi sana, nakiukwel zinakatisha tama, kama ukiwa nakipato kidogo Sana hutoboi.
 
Habari, wataalam na wenye uzoefu wa jambo hili naombeni muongozo katika jambo langu hili.

Ili kujikwamua na ufukara uliokithiri Nilitaman kufanya biashara ya ufagaji.. Nilionelea nifanye ufagaji wa kuku wa mayai. But sijawah kufanya hii kitu uzoefu nilionao ni wa kuhudumia kuku wetu wale tunaofuga nyumbani so kwa kiasi naelewa kuku wanavyotia stress.

Nilitaka ninunue eneo kuanzia 1 hector and above kisha ndio nifanyie hapo shughuli hizo za ufugaji.....
  • So Ningependa kujuzwa vitu vya kuzingatia katika kuchagua eneo la kufanya ufugaji huo.
  • Je biashara hii inalipa au ndio pasua kichwa?
So maelezo yenu ndio yatanipelekea kufanya Viability and feasibility analysis yangu.

Karibu wajuzi wa mambo mnipe mawazo. Yaani naanza from scratch naweza sema sijui lolote kwenye biashara hii.

Nimesoma soma threads humu, kutazama video YouTube na kufuatilia fb swala hili. Natumaini GT wa JF mtanijuza zaid.
Nimeona ni kushauri ki uhalisia mm ni mfugaji pia.
Kuku hao 500 mtaji wake walau uwe na milioni 20 cash otherwise unaweza kuwauza iko hivi
Unawanunua kwa 500@2400=1200000
Chakula kwa mwezi ni wastan wa milion 2 so miez 6 ni milion 12
Banda lets say 4m
Mengineyo
Drinker,feeder,dawa,chanjo,mfanyakaz,randa,na any emergency

Mi binafsi nilianza na kuku 600
Ninatumia cage nilikus na milion 30.
Kuku 1.5m
Cage vifaranga za 1m
Banda 4.5m
Fens 7m
Chakula 6 month 13.5m
Cage 5 ni 4.5m
Mengineyo
.
.
.
.
So roughly ni hivyo

Kumbuka mwanzo gharama ni kubwa sabab ya uwekezaji baada ya hapo ukikamilisha kila kitu ndo utaanza iona pesa.
Miez 6 kuku kishachanganya kutaga wanajihudumia wenyewe faida unaiona.
Kamwe usiweke kuku bandan kama hauna uhakika wa chakula stress itayokupata hautakaa usahau.
Usipendelee kuita ma dr bandan wao ndo chanzo cha kuhamisha magonjwa kutoka banda A to B
Daktar wa kwanza ni wewe mwenyewe.
Uzio wa kuingia bandanuwe closed muda wote
Kuku sio sehem ya maonyesho wape privacy na utulivu
Kama hujui magonjwa ya kuku anza na kienyeji chotara ujifunzie chanjo na magonjwa sabab wanajikaza kufa(niliabza na kroiler) kwa miaka 2 ndo maana sijawah kuita dr bandan kiushaur hua napiga sim farmers centre.
Endelea kuuliza chochote nikipata muda nitakua nakujibu
 
Naomba kuuliza je hela yako hiyo ilirudi??? If yes kwa muda gani???
Kwa maelezo ya wadau nimeona nianze na 100 kuku. Je unanishauri vipi kwa idadi hiyo?
 
Biashara ya kuku wa mayai sio mbaya katika uwekezaji, ila ushauri wangu Anza na kuku wachache kwanza hata kama una mtaji mkubwa, Hawa sio kuku wa nyama kuwalisha Hawa viumbe mpaka waanze kutaga inachukua miezi mpaka 6, Hawa wajomba hawalali kazi Yao kubwa iliyowaleta hapa duniani ni kupiga msosi, na gharama za vyakula vyao na vitamin na dawa za kuwachanganyia kwenye maji zimepanda pia.... Kwa io unaweza kukimbilia kuwafuga wengi badae ikawa mtihani katika kuwafuga

Nimeona watu wengi wakiwauza kabla hawajataga baada ya kushindwa kuwahudumia mpaka mwisho

Tahadhari nyingine tafuta sehem au namna umeme uwe wa uhakika Hawa kuku umeme ukikatika ni wajinga sana watatafuta Kona Moja watarundikana na kulaliana kesho unaweza Kuta hata 50 wamekufa kwa kulaliwa na wenzao, sehemu iwe tulivu, kwenye paa lao akitokea hata mtoto mtundu akarusha jiwe watalaliana sehemu Moja kwa hofu na watakufa wengine

Uwe na roho ngumu kidogo, Kuna kaupepo ka ugonjwa kakipita wao kufa hata 30 Kila siku sio jambo la ajabu sana, lakini Mungu akisaidia inalipa maana wakianza kutaga unaongeza na mke wa pili kabisa😃😃

Nimeona nikupe baadhi ya changamoto chache wengine wataleta mengine
Huwa napenda sana ushauri kama huu ambao sio wa kurema maneno. Big up
 
Anza na 100 au 200. Prefarably 100. Mimi nitaandika ushauri vizuri kesho, saivi nipo sehemu siwezi ku type sana, ila i would like to know unafugia mjini sana au sehemu za ndani ndani kidogo..?
Mkuu nakaa mjini nataka niende kijijini ila sio ndani ndani. Nataka ambapo gari lisizidi nusu saa kutembea hadi mjini. In short nataka iwe nje ya mji. Je unaushari gani kwa wazo hili mkuu?
 
Naomba kuuliza je hela yako hiyo ilirudi??? If yes kwa muda gani???
Kwa maelezo ya wadau nimeona nianze na 100 kuku. Je unanishauri vipi kwa idadi hiyo?
Mimi faida napata kuku wangu nilichukua mwaka jana may wakaanz kutaga sept mwishon hadi oct wakawa wameanza kujilisha na kuanza kukusanya faida.
Hela kurudi itarudi tu sabab faida aiona na kuna vitu kama jengo na fensi ni la milele cage life span yake ni hadi miaka kumi so hivi vitu nachukulia tu kama sehem ya kuwekeza siangalii virudishe pesa kwa mizunguko ya mwanzon. faida nai calculste hivi kulisha miez 6 kabla hawajaanza kutaga,dawa na chanjo na any service ambazo kuku alipata like msafisha panda,mlinzi na mishahara wa wafanyakazi tray za mayai nilizouza kipindi chote cha kua na hiyo batch ya kuku so Ki ujumla faida ipo
 
Kuroiler. Mayai yake ni ghali ukilinganisha na layers na pia sio wasumbufu kwenye kufugwa. Chakula chao pia ni rahisi wakishavuka ile hatua ya vifaranga.
Tofauti na layers chakula chao ni special mfuko ule elfu 50 na bado wanakula sana na mayai yao ni bei chee tu.
Kwasasa trei la layers mnauza bei gani
 
Kuna mahali nimeona unataka kuanza na kuku 100. [emoji849][emoji849] Wakifanikiwa kutaga hizo ni tray 3 au 2.5 kwa siku.

Huwezi kusema mradi wa kuku na unakusanya tray 2.5, hata wewe mwenyewe huwezi kua serious na huu mradi unless sio mradi mama hapo shambani.

Ili uweze kupata faida kwenye kuku wa mayai atleast wawe 300/=

Otherwise, unafanya pilot study.
 
Walichochangia wadau hapo juu ndo ushauri wa kubeba kuanza nao sababu ni ukweli pia Kuna dawa za kuzuia typhoid na coccidiosis, pia mafua zisikose unaweza weka Kwa maji au chakula
 
Back
Top Bottom