Oh yeah!!
Umesema umesimamia mashamba mengi ya ufugaji wa kuku wewe ukiwa kama mtaalamu..
okay swali langu kwako ni liko hapa kwenye management of one day chick up to laying time.
Ntajitahidi kufupisha maelezo.
1.Zingatia mazingira ya Joto. Hapa watanzania wengi hutumia vyungu vya joto kulea vifaranga kwa week 2 - 3 kutegeme na msimu wa joto au baridi. Kawaida chungu kimoja kinalea kuku mpaka 100. Lakini pia kuna taa maalumu za joto zinauzwa kwenye maduka ya Mifugo.
2.Zingatia chanjo, Siku ya kuchanja kwa kawaida siku ya 7 tunachanja chanjo ya ugonjwa wa kideri, siku ya 14 tunachanja chanjo ya ugonywa wa Gumboro, siku ya 21 unarudia kideri, na siku ya 28 unarudia gumboro, siku ya 35-42 unapiga ndui/Fowlpox siku ya 60 unawapa dawa ya minyoo. Baada ya hapo utakua unarudia Chanjo ya kideri na Dawa ya Minyoo kila baada ya miezi 2.5 - 3 kutoka kwenye tarehe ya mwisho ya kuchanja
3.Zingatia chakula bora, katika kipindi cha miezi 2 ya kwanza kifaranga anagakiwa apewe chakula bila kupimiwa, angalia kampuni nzuri ya chakula cha kuku wa mayai inayo patikana mahali ulipo. Aina ya chakula wanachokula ni Chick starter kwa miezi 2 ya kwanza, Grower mash mwa miezi 2.5 inayofuata, then Layer mash wakiaanza kutaga kwa asilimia 5
4.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya maji chakula.
5.Zingatia Biosecurity, hapa nimekosa kiswahili kizuri, hakikisha unazui kuingia hovyo kwa watu shambani kwako, hakikisha unabadirisha viatu unapoingia bandani kwako, hakikisha unakua na makoti special ya kuvaa bandani.
Maelezo mengine, unaweza angia pdf nimeshare hapo juu kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai. Kuna no. zangu za simu kama ungependa maelezo zaidi