Mkuu Kuna watu ni wapumbavu sana.. wanafikiri ile zamani watu walikuwa wanaokota fedha barabarani basi na unaweza okota fedha kwenye akaunti yako..
Hakuna fedha inayoweza potea bure kwenye transaction za kibenki. Wataitrace tu na wataipata.
Ule mwaka serikali imenunua Korosho kuna mkilima aliingiziwa kimakosa million 5, yule mkulima ile hela alijua si yake akaiacha zaidi ya miezi 8 na bado haikutolewa. Kuna wakati akapati shida akaingiwa tamaa akaitoa ile pesa, mwezi May tu hapa alikuwa na access ya 5m kwa account yake wakailamba chaap kuja kufatilia akaambiwa 2018 aliingiziwa hela kimakosa..
Hakuna hela ya bank inapotea hivihivi, na utakuja kuilipa kwa machungu na kudhalilika kama mdau anachokipitia hapa