Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Washitaki ofisini kwako, hawatakiwi kukata mshahara wako wote, kisheria lazima 1/3 ibaki, hao NMB wasubilie au waongeze muda wa mkopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nenda ongea nao sana sana, na waambie kama Hawa kati kidogo kidogo una Acha kazi unatafuta ingine maana huwezi survive, watanyoka tu!
 
Washitaki ofisini kwako, hawatakiwi kukata mshahara wako wote, kisheria lazima 1/3 ibaki, hao NMB wasubilie au waongeze muda wa mkopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huyo alichofanya ni uwizi.. Alishaambiwa halali yake ni 5m yeye kakuta 9m kachukua yote bila hata kuuliza..

Mkopo atakatwa kama kawaida lakini pia ile ya uwizi anatakiwa kuilipa. Hapa ushauri wowote unaotolewa bank hawatausikiliza, jamaa akomae kulipa tu hiyo 4m na si vinginevyo..

Njia nzuri ni yeye kama ana biashara achukue hati yake then akopee bank kwa hiyo biashara yake au hata kama yeye hana biashara basi atafute mtu mwenye biashara amkopee na yeye akubali kuweka hiyo hati yake kama dhamana..

Tofauti na hili tusidanganyane jamani, eti mtu anamwambia akaongee na meneja, zile fedha si za meneja ni za taasisi. Maneno hayatafanya asamehewe au mkataba ubadilishwe, bali alipe tu as long as anakubali kwamba aliitumia..
 
Hivi hizi akili za kujenga kwa kukurupuka huwa mnazitoa wapi?!

Unakwenda kujenga huko nje ya mji ambapo hata ukikosa nauli kuja mjini ni shughuli....

Kwann usisave then upate kiasi cha kuanzia kujenga baada ya muda....
 
Nawaza hivi lakini Je kama mkopo wa NMB alishatumia hati ya nyumba kama dhaman??
Mkopo wa NMB dhamana ni mkataba wake wa ajira, huoni kwamba pesa inakatwa yote juu kwa juu na ndio maana analia?
 
Nilishasema, sipati pesa nikaiwekeza kwenye nyumba ili hali haina mrejesho wa uchumi. Ungekuwa na akili ya biashara ungeitumbukiza huko ukaja kujenga kwa madaha.
 
😆😆😆 Ilo jumba bovu lime mwangukia loan officer aliye issue claims yako ...we mwachie liporomokeee kabisaaa yaan we waambie pesa umewekeza shambani
Kuna mdau aliuza deni la CRDB kwa bank X. Kosa walilofanya bank X walimpa mdau milioni 6 cash akalipe deni CRDB. Hakurudi tena na CRDB hakulipa. Walipoenda kuingiza makato kwa mwajiri wakakuta bado deni la CRDB bado lipo. Walimbembeleza arudishe ila wapi
 
Hii habari mleta mada umeiandika sijui huku unakimbizwa na maofisa mikopo wa NMB wanataka kukunyang'anya na simu kabisa ili wapunguze deni.


Hebu ainisha bila kificho mambo yafuatayo bila kutuchanganyia madawa...

1. Deni la bodi ya mikopo (HELSB) ni kiasi gani?!
2. Ulikuwa unadaiwa na NMB kabla ya kupelekea deni la helsb ama ulimaanishaje?!
3. Hiyo amount ya milioni 5,600,000 inahusiana na nini na hii 17,400,000 ni nini?!
4. Kwa mujibu wa NMB na utaratibu wao wa kukopesha na makato, inakuwaje wanakulamba mshahara wote?!
5. Mshahara wako ni kiasi gani ili tuweze kukusaidia kucalculate makato sahihi?!

Hebu tunyooshee habari maana umeandika kwa kuruka ruka sana...
 
Nawaza hivi lakini Je kama mkopo wa NMB alishatumia hati ya nyumba kama dhaman??
Halafu nasikia SASA hivi japo sina uhakika Sana Wana mtandao mmoja na ukishajulikikana wewe si mwaminifu hutakopesheka Kwa Benki yote nchini.
 
Hukuwa na kosa lolote kwani sheria inasema kama umekuta pesa kwenye akaunti ukaamini ni ya kwako hutakiwi kudaiwa. Wewe uliamini hiyo pesa ni yakwako kwa sababu ulichukua mkopo.
 
Wàtu hawajui kuwa mkopo maana yake ni "kipato chako cha baadaye umeamua kukitumia leo" . When you decide to use all your future income today then make sure you have strategies to survive in the future. Jamaa alitumia pato lake la leo tangu juzi, tena alitumia kujengea nyumba, ale hiyo nyumba sasa kama inalika.
 
Katika nchi za watu wanaojitambua, nchi ambazo watu wanaenda shule ili kila mtu apate ujanja kichwani ili asitokee mmoja au taasisi ya kumwonea mwingine, benki haiwezi kumlazimisha mwajiri wako eti mshahara wako upitishiwe kwao benki.

Ingekuwa ni kiasi cha wewe kwenda kumwambia dada wa human resources, ee bana eehh, kuanzia leo mshahara wangu nautaka mkononi! Cheki au cash money. Shenz type.

Halafu hao benki mngeendelea kudaiana pembeni mtaani huko.
 
Nilishasema, sipati pesa nikaiwekeza kwenye nyumba ili hali haina mrejesho wa uchumi. Ungekuwa na akili ya biashara ungeitumbukiza huko ukaja kujenga kwa madaha.
Mkuu kwa hiyo unapata hela unaenda kupangisha nyumba unalipa kodi!?? Well and good
 
Hakuna cha nchi inayojitambua mkuu.. mdhamini wa mkopo wako ni mwajiri, Sasa mkibadilisha akaunti ya mshahara kwa njama basi marejesho yasipoonekana anafuatwa mwajiri. Bado haujasolve tatizo hapo
 
Hakuna cha nchi inayojitambua mkuu.. mdhamini wa mkopo wako ni mwajiri, Sasa mkibadilisha akaunti ya mshahara kwa njama basi marejesho yasipoonekana anafuatwa mwajiri. Bado haujasolve tatizo hapo
Mwajiri anapokudhamini, ukifukuzwa kazi inakuaje?

Au tuseme bongo hamna suala la kufukuzana kazi, okay, ukifa inakuaje? Mwajiri analipa deni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…