Kaudunde Kautwange
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 1,644
- 1,648
Mkuu, ebu msome tenaa.." NMB wakanipigia mahesabu ya jumla kuwa pamoja na kununua hilo deni na kutoa deni lao watanipa jumla ya Tsh 5,660,000 nikasema poa tu"
1.Hii hela (5,660,000) waliyokupigia hesabu kwamba utabaki nayo baada ya wao kukata madeni yao yote ikowapi?
2.Na kama walikupigia hesabu wao,kwenye fomu ya mkataba ni lazima iandikwe hivyo,Je IPO hivyo? Kama imeandikwa kwenye mkataba kosa ni lao hivyo hawapaswi kushikilia hela yako kabisa.
3. Makao makuu uliongea na nani?kama ni wale wa huduma kwa wateja wengi hawana uelewa wale,kwa ishu tata kama hizi utaishia kupewa majibu rahisi tu kama waliyokupa.
4."Nikawapigia makao makuu, (audio clip ninazo) wakadai kuna makosa pande zote"
Hapa kosa lako wewe ni nini?si uliambiwa utabaki na 5,660,000?
5."lakini pia wakasema nilifanya kosa la kutoa pesa ambayo ilizidi (kitu ambacho nilikubali)" hapa ulikubali nini mbona unajichanganya wewe mwenyewe?
Hitimisho:
Ukijibu hayo maswali tuyajua tatizo liko wapi,maana kuna vitu naona umejichangaya hatuelewi lakini nikushauri tu,
Andika barua kwa mwajiri(ambaye ndiye mdhamini wako) wako kuelezea tatizo lako ukiweka na uthibitisho wa bank statement,mkataba wa mkopo nk ili yeye aiandike bank rasmi.
Kingine piga huduma kwa wateja(ila usiwaeleze tatizo tena) waombe contact za Idara ya mikopo ya wafanyakazi,ongea na mkuu wa Idara kisha tuma malalamiko yako kwa email(yakiwa na ushahidi,pamoja na barua uliyopeleka kwa wajiri na benki) kopi iende kwa MD au CFO,maana naamini hio barua unayosema umendika umepeleka tawini,ambapo kama kosa ni lao hio inaishia kwa Meneja tu ili nao wawe salama,kwa hatua hizi utapata majibu ya Uhakika.
Kila la Heri.
1. Hiyo 5.6M ndio ipo ndani ya ile 9. something Milion ambayo aliitoa bank.
5. Alikubali kuwa hiyo pesa iliyozidi, yaani 4.something Milion ni kweli ameitoa toka kwenye account yake.