Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri mzuri, most of the time biashara zina changamoto hasa as a supplier company kwa gvnt ni shida, tatizo hizi taasisi za serikali unakuta wamepata pesa ya kumlipa supplier lakin vipao mbele vyao vinasababisha reallocation of fund na supplier anaacha kulipwa kwa wakati and they don't care, wanakujibu pesa haijaingia subiri kumbe wewe ulikopa na ukatarajia quick payment. So inabidi jamaa amvumilie kama jamaa hakuwa na lengo baya, na experience inaonekana amewahi kumkopesha mara kadhaa kwa style hiyo hiyo, biashara ni suala ambalo wakati mwingine ni undetermined.Mi ningekushauri usimdai,hesabu kama hasara alafu akipata atakupa,huwezi jua amekwama kwa namna gani.Mambo ya biashara yana changamoto ndugu.
Kopesha mtu kiasi ambacho unaweza kumsamehe, Binadamu hatuna dhamana,unaweza mkopesha mil 10 ukashangaa mtu huyo amepata kesi mara amepata maradhi,dakika ya mwisho kumdai huwezi mtu akikuomba umkopeshe kiasi fulani basi kigawe mara kisha mpatie hiyo nusu.Salaam,
Katika harakati zangu za kusaka tonge, yupo jamaa ambae nilifahamiana Naye katika biashara, tukawa tumezoeana hadi ikafikia kipindi akiwa na shida na hela namuazima ila anaacha gari yake kama bond, akienda akasupply mizigo yake akilipwa ananirejeshea pesa zangu na yeye anachukua gari yake.
Sasa zamu hii nilimpatia pesa milioni 8 akaniachia gari yake Range Rover namba B akiahidi atarejesha baada ya mwezi mmoja akishalipwa na hiyo halmashauri anakosupply mzigo.
Sasa yapita miezi karibia 6 toka achukue hela na gari lake lipo hapa limelala kila Nikimdai pesa yangu ananambia hajalipwa bado, na hili gari hatujaandikishana kwamba akishindwa kulipa gari iwe mali yangu, binafsi sijawahi kumiliki gari na gari lenyewe nikisema niwe nalitumia kupooza machungu siwezi sababu gari inakula mafuta sana hii.
Imefikia hatua namdai ananambia anatafuta mteja akaliuze hili gari aweze kunilipa hata hvo naona kama sound tu. Nimefikia hatua kumwambia walau anilipe tu nusu ya pesa yangu nilompatia na nusu itakayobaki nihesabu hasara tu ili niweze na mm kulipa madeni yanayoniandama ila bado anadai hela hana coz hajalipwa bado.
Wakuu nafanyaje hapa?
Braza hili ni jambo la msingi sana na la kuzingatiaKopesha mtu kiasi ambacho unaweza kumsamehe, Binadamu hatuna dhamana,unaweza mkopesha mil 10 ukashangaa mtu huyo amepata kesi mara amepata maradhi,dakika ya mwisho kumdai huwezi mtu akikuomba umkopeshe kiasi fulani basi kigawe mara kisha mpatie hiyo nusu.