Umenena Kaka,,Huwezi Kumchampa Mtoto Kisa Kakataa Kula,,Hapo Ndio Anamvuruga Kabisa,Mtoto anahitaji Akili Kubwa Mnoo ili uwezekung'amua Shida Zake
Mimi wangu hapendi kula ila sio fimbo mzee unaenda mbali sana.
1. Nilichokuja kugungua ni kuepuka kuwaonyesha watoto wenu kwa watu. Watu ni wachawi mno. Wapeleke watoto wakacheze mbali na home, home binaadam wabaya sana.
2. Epuka kumpa mtoto vyakula vya viwandani, epuka biscuits japo mara moja moja mpe, pipi, vitu vyenye sukari humpotezea mtoto hamu.
3. Epuka ugali, wali, ndizi kila mara. Changanya radha mbalimbali, mpe mayai, maboga, viazi batata, changanya na mchuzi wa samaki, wkt mwingine nyama ngommbe kuku nk.
4. Epuka vyakula vyenye harufu. Kwa mfano viungo, epuka, mfano jaribu hii mrenda na kaugali. Hapa hakuna harufu atakula, mpimie kipimo cha umri wake, usimpe ari mradi.
5. Uji. Epuka hii wanaita lishe. Kama ni uji wa mahindi mpe wa mahindi tuu, kama ni mama mpe huo tu, kama ninwa muhogo mpe huo tu. Na isiwe kila siku badili badili radha tofauti. Ubwabwa weka na kipande cha samaki, weka jani la maboga changanya.
6. Matunda siku 7 za wiki ale matumda sita au saba mfano. Embe J3, Chungwa J4, Parachichi Jumatano, Papai Alhamisi, Nanasi Ijumaa, Apple Jumamosi na Topetope Jumapili. Topetope liwe mwisho wa wiki maana kulipata ni kwa shida. Juisi wazoeshe za kutengeneza kwa usafi.
Mwisho mpe mtoto mayai ya kukaanga na kuchemsha, mpe nyama maana IQ inapatikana kwenye nyama, mayai, maziwa, ndizi, wanga kwa mbaaali nk nk
Hii ni kwa experience yangu.
I am done here