Naombeni ushauri kuhusu nyumba yangu niliyoijenga Maramba Mawili

Naombeni ushauri kuhusu nyumba yangu niliyoijenga Maramba Mawili

Kuna mtu pia alinishauri hiyp.ya room selfcontained ila naona uzito kudeal na watu wengi

Nilivyo mwehu eti namuombaga yeye ushauri na anavyonikatisha tamaa sasa.
Kuna wkt alinishauri nimuuzie ila hiyo bei alitajia nilichoka
Usipokua makini utapoteza nyumba yako.
Nyie mmeunganishwa na biashara bila shaka humjui na wala yeye hakujui, unamuingiza kwenye mipango yako kitu ambacho ni hatari sana.

Atapima uelewa wako na kuona akupige vipi na ushindwe kuchomoa.
 
😂😂😂 fanya unikutanishe naye tu mzee wa bucci
Poa.
Leo nimemuona yuko kwenye ford ranger ya boss wake wanamjengea gorofa alivyoweka hicho kipepsi nilikukumbuka nikacheka 😄😄
 
Karibia na Kwa Osama,ingekua kipindi kile cha kikwete kabla Mambo hayajaharibika,Kodi ungekula Ata laki tano Kwa mwenzi,
Ila Kwa Sasa pandisha Kodi kidogo apo kwenye laki tatu sio mbaya
Poa mkuu?
 
Usipokua makini utapoteza nyumba yako.
Nyie mmeunganishwa na biashara bila shaka humjui na wala yeye hakujui, unamuingiza kwenye mipango yako kitu ambacho ni hatari sana.

Atapima uelewa wako na kuona akupige vipi na ushindwe kuchomoa.
Nakubali mkuu kuwa hapo sikutumia akili
 
Hi JF.

Ndugu zangu naomba mawazo yenu.

Ni hivi, kuna nyumba iko hapo Mbezi Maramba mawili naona kama nilipoteza muda na hela zangu bure coz haina faida yeyote kwangu tokea nimeijenga.

Ilipokamilika nilimpa uncle wangu na wife wake wakae. Baada ya miaka 3 ndugu akajiongoza akaenda panga 2 rooms then akaleta mpangaji kwa 200K kwa mwezi. Ikawa ile kodi anatumia kulipia zile 2 rooms inayobaki anatumia.

Ikaenda hivyo for two years nikiwa sijui kitu coz baada ya kuwakabidhi sikuwahi tena kwenda huko hadi siku jirani mmoja kunipigia akilalamika kuhusu wapangaji wangu.Nikashangaa ikabidi niende kwa lengo lakuwatimua hao waliopangishwa bila idhini yangu.

Kufika Maramba, nilijicheka kumebadilika, kumejengwa hata njia ya kufika kwangu nimeisahau😁😁 ila nilifika nikakuta nyumba imechoka baadhi ya vioo vimevunjwa, vitasa hakuna, rangi ndo usiseme ila wapangaji walinipokea vizuri na walikua watu wastaarabu sana.

Nikajitambulisha na wakashangaa coz kwa 2 yrs wanajua ndugu yangu ndo mama mwenye nyumba wao wakaanza kulalamika kutapeliwa.

Nikawaambia hakijaharibika kitu endeleeni kukaa ila nikawaomba wanipe 300k kwa mwezi sababu nyumba imechoka coz 200K ni ndogo sana.

Hiyo 300K kwa mwezi walilipa miezi 6 tu then Covid 19 ikaja wakaomba 200k coz Covid imempozea baba kazi, nikakubali nikiwa naplan nikaikarabati then niweke mpangaji atakayenipa hela yakuridhika.

Cha ajabu nina hiyo plan tokea enzi za Covid ila kila nikifikiria kwenda Maramba kufanya huo mchakato naona uvivu na mind you marekebisho makubwa hapo ni rangi tu na toka nilipoenda kujitambulisha sijarudi tena Maramba so mpaka leo wananipa 200K kwa mwezi ila nahisi ni ndogo sana.

Ninawaza niiuze hiyo nyumba then nikajenge kwenye moja ya plots zangu zilizoko Mtoni Kijichi.Kijichi kuna kodi nzuri.

Au niikarabati then niongeze kodi ila hapa nashindwa kuamua coz sijui soko la nyumba za kupanga likoje hapo Maramba Mawili.

So majirani zangu wa Maramba Mawili hebu niambieni eti kajumba ka 3 bedrooms,big living room,dinning,jiko,choo cha master na public,alluminium window,tiles,umeme ikiwa kwenye hali nzuri halali yake kwa mwezi ni bei gani kupangisha kwa sasa?Enzi hizo kabla wakati nampatia uncle wangu alipatikana mpangaji wa 350K kwa mwezi kwa kila miezi 4.

Na je nikisema niuze nitapata kiasi gani eti majirani zangu wapendwa(Kwa kukadiria)

Natanguliza shukrani zangu Majirani zangu wapendwa.Sisi ni ndugu tusaidiane🙏🙏
Kiufupi HUNA NYUMBA UNAJIFURAHISHA KUANDIKA UZI
 
Poa.
Leo nimemuona yuko kwenye ford ranger ya boss wake wanamjengea gorofa alivyoweka hicho kipepsi nilikukumbuka nikacheka 😄😄
Mi kucheka sitaki bana 😂😂😂
Hiyo ford alikaa mbele?
Mr bucci basi ana ujinga mwingi, ungempiga picha bana nimuone mzee wa bongo bahati mbaya.!
 
Mi kucheka sitaki bana 😂😂😂
Hiyo ford alikaa mbele?
Mr bucci basi ana ujinga mwingi, ungempiga picha bana nimuone mzee wa bongo bahati mbaya.!
😁😁😁
Akae nyuma ana wwzimu😄
Kajitanua pale mbele uzasema ye ndo bosi anaendeshwa😄😁
Picha singeweza huyo boss angenimind.
 
😁😁😁
Akae nyuma ana wwzimu😄
Kajitanua pale mbele uzasema ye ndo bosi anaendeshwa😄😁
Picha singeweza huyo boss angenimind.
😂😂😂 kaupiga mwingi
Km ana simu hapo kajifotoa za kutosha.!
Mzee wa bongo bahati mbaya natamani sana nimuone
 
Wabongo tupunguze wivu, unachokiona kigumu kwako sio kwa wote.!
Kuna sehemu niliona anatia huruma kuomba connection ys ya ajira nikatamani ningekua na uwezo nimfanyie wepesi.Imagine ningekua na huo uwezo hlf unaingia cha kike kumsaidia mtu kama huyu.
 
Back
Top Bottom