Naombeni ushauri: Kwa hali hii maamuzi ya kuuza nyumba yatakuwa sahihi?

Kwanza tafuta UTULIVU una
1. STRESS
2.DEPRESSION
3. FRUSTRATION
 
Kama una miaka 34 ina maana watoto wako bado wadogo! Je, ukiuza hiyo nyumba hao watoto wadogo wataishi wapi? Hiyo biashara ya magari inayokushawishi kuuza nyumba una uzoefu nayo?!

USHAURI: Pambana na UDALALI ili uone mwenendo mzima wa biashara nzima ya magari. Baada ya angalau mwaka mmoja ukiuza hiyo nyumba ili uanzishe biashara ya magari angalau tayari itakuwa unafahamu mwenendo wa biashara ulivyo, vichochoro vyake, changamoto na mengine kama hayo! Yaani utauza nyumba at the expense of what you already know!
 
Hii TABIA ya Mwanaume kukwama kidogo, Badala ya Kupambana kutafuta pesa anawaza kuuza vinavyomzunguka TABIA hii inakera sana.

Mwingine anakwama kdg, anauza vyote alivyonavyo ndani Hadi godoro.

Kule pwani, kijana Yuko radhi auze Hadi suruali yake Ili apate pesa ya kwenda mziki.

Uanaume ni kuwa na maono na Kupambana, hiyo Roho ya uza uza ishindwe Kwa Jina la YESU.
 
Auuuze kitimoto itamlipa
 
Uza nyumba halafu kanunue uwanja ujenge hata nyumba ya vyumba vitatu tu halafu hera inayobaki ingiza kwenye biashara unayoitaka
 
Muone dalali wa madalali DALALI MKUU akupe maujanja na ndumba za kidalali..

Si ajabu hiyo hela ukatapeliwa na madalali wenzio, dalali msingi domo tu. Kama ngenga imo unaweza anza na mali kauli tu na ukatoboa, ninyi watu wa maneno mengi ni rahisi kumuaminisha mtu.
 
Ni mkosi kuuza kitu ulicho kitafta
 
Usiuze nyumba Ila
Kama unaweza ukajibana ukapangisha nyumba zima wewe na mkeo mkajibana uswahilini vyumba ya bei rahisi wakati unaset mipango mingine Ila nyumba yako ukaitumia Kama chanzo kimoja wapo cha mapato yako, watu wengi nimeshaona wanafanya hivi , mipango Yake ikikaa sawa anarudi kwenye mjengo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…