Naombeni ushauri: Kwa hali hii maamuzi ya kuuza nyumba yatakuwa sahihi?

Mimi ni baba wa watoto watatu Na mke mmoja Nina miaka 34.

Mtoto wa Kwanza ni kwa mwanamke wa Kwanza na Hawa wawili ni kwa mke niliyenae sasa ambaye naishi nae hapa nyumbani.

Nimezaliwa Na kukulia mkoa X, nimekuja Dar kutafuta Maisha lakini mji huu unahitaji uwekezaji Na connection Za biashara.

Nina nyumba yenye uwanja mkubwa, nimeijenga baada ya kwenda South Africa lakini Kwa sasa Maisha ni magumu Sana South Africa kwahiyo nikachukuwa jukumu la kurudi nyumbani.

Nilianzisha biashara ya Duka la spear za pikipiki mkoa niliozaliwa lakini Ile biashara ilikuja kufa kabisa nikaamua kuuza ili nipate Kodi ya kuja kuanza Maisha Dar es salaam.

Nimepata rafiki ambaye yeye anauza magari yake kwahiyo Mimi nikaanza Kazi ya udalali WA kuuza magari lakini Sina uzoefu hii Kazi ya udalali WA magari.

Maamuzi yangu Ni kuuza nyumba Na kuondoka mkoa X kabisa na pesa ambayo nitaipata natumia hili tobo la huyu rafiki yangu kwajili ya kununua MAGARI japani Na kuuza hapa nyumbani.

Naombe ushauri wenu wadau maamuzi ya kuuza nyumba Ni mazuri kweli ama hapana.?
Kwanza tafuta UTULIVU una
1. STRESS
2.DEPRESSION
3. FRUSTRATION
 
Nimepata rafiki ambaye yeye anauza magari yake kwahiyo Mimi nikaanza Kazi ya udalali WA kuuza magari lakini Sina uzoefu hii Kazi ya udalali WA magari.

Maamuzi yangu Ni kuuza nyumba Na kuondoka mkoa X kabisa na pesa ambayo nitaipata natumia hili tobo la huyu rafiki yangu kwajili ya kununua MAGARI japani Na kuuza hapa nyumbani.

Naombe ushauri wenu wadau maamuzi ya kuuza nyumba Ni mazuri kweli ama hapana.?
Kama una miaka 34 ina maana watoto wako bado wadogo! Je, ukiuza hiyo nyumba hao watoto wadogo wataishi wapi? Hiyo biashara ya magari inayokushawishi kuuza nyumba una uzoefu nayo?!

USHAURI: Pambana na UDALALI ili uone mwenendo mzima wa biashara nzima ya magari. Baada ya angalau mwaka mmoja ukiuza hiyo nyumba ili uanzishe biashara ya magari angalau tayari itakuwa unafahamu mwenendo wa biashara ulivyo, vichochoro vyake, changamoto na mengine kama hayo! Yaani utauza nyumba at the expense of what you already know!
 
Hii TABIA ya Mwanaume kukwama kidogo, Badala ya Kupambana kutafuta pesa anawaza kuuza vinavyomzunguka TABIA hii inakera sana.

Mwingine anakwama kdg, anauza vyote alivyonavyo ndani Hadi godoro.

Kule pwani, kijana Yuko radhi auze Hadi suruali yake Ili apate pesa ya kwenda mziki.

Uanaume ni kuwa na maono na Kupambana, hiyo Roho ya uza uza ishindwe Kwa Jina la YESU.
 
Unauza nyumba ili iweje, sikia kama una angalau milioni moja hapo na upo dar, tafuta mtaani uliochangamka kodi fremu ya elfu 20 miezi sita kisha watafute wale wa magari ya gesi nunua mitungi ya gesi ya laki tano weka kwenye fremu anza kuuza, biashara hii haina hasara, unaweza kuingiza hata laki kwa wiki kama ukifungua kwenye mtaa mzuri.

Chukua hiyo laki tano iliyobaki fungua butcher la nyama, tafuta frem mtaani hata ya elfu 20 miezi sita, nunua panga, shoka, gogo, mzani na machuma ya kuanikia nyama anza kazi kuhusu friji sijui vioo utaweka siku nyengine hapo nunua tu nyama ya ng'ombe machinjoni anza kazi, ukiuza kilo moja ya nyama unapata elfu kumi hivyo watu kumi hapo una laki yak, hivyo kwa wiki huwezi kukosa wateja wanyama ya ng'ombe mtaani biashara hii haina hasara kwa dar es salaam

Kila la kheri biashara hizo mbili naamini zitakutoa mkuu, kama huna hiyo million moja kama nyumba inakiwanja kikubwa sana kata enso uza upate mtaji
Auuuze kitimoto itamlipa
 
Mimi ni baba wa watoto watatu Na mke mmoja Nina miaka 34.

Mtoto wa Kwanza ni kwa mwanamke wa Kwanza na Hawa wawili ni kwa mke niliyenae sasa ambaye naishi nae hapa nyumbani.

Nimezaliwa Na kukulia mkoa X, nimekuja Dar kutafuta Maisha lakini mji huu unahitaji uwekezaji Na connection Za biashara.

Nina nyumba yenye uwanja mkubwa, nimeijenga baada ya kwenda South Africa lakini Kwa sasa Maisha ni magumu Sana South Africa kwahiyo nikachukuwa jukumu la kurudi nyumbani.

Nilianzisha biashara ya Duka la spear za pikipiki mkoa niliozaliwa lakini Ile biashara ilikuja kufa kabisa nikaamua kuuza ili nipate Kodi ya kuja kuanza Maisha Dar es salaam.

Nimepata rafiki ambaye yeye anauza magari yake kwahiyo Mimi nikaanza Kazi ya udalali WA kuuza magari lakini Sina uzoefu hii Kazi ya udalali WA magari.

Maamuzi yangu Ni kuuza nyumba Na kuondoka mkoa X kabisa na pesa ambayo nitaipata natumia hili tobo la huyu rafiki yangu kwajili ya kununua MAGARI japani Na kuuza hapa nyumbani.

Naombe ushauri wenu wadau maamuzi ya kuuza nyumba Ni mazuri kweli ama hapana.?
Uza nyumba halafu kanunue uwanja ujenge hata nyumba ya vyumba vitatu tu halafu hera inayobaki ingiza kwenye biashara unayoitaka
 
Muone dalali wa madalali DALALI MKUU akupe maujanja na ndumba za kidalali..

Si ajabu hiyo hela ukatapeliwa na madalali wenzio, dalali msingi domo tu. Kama ngenga imo unaweza anza na mali kauli tu na ukatoboa, ninyi watu wa maneno mengi ni rahisi kumuaminisha mtu.
 
Hii TABIA ya Mwanaume kukwama kidogo, Badala ya Kupambana kutafuta pesa anawaza kuuza vinavyomzunguka TABIA hii inakera sana.

Mwingine anakwama kdg, anauza vyote alivyonavyo ndani Hadi godoro.

Kule pwani, kijana Yuko radhi auze Hadi suruali yake Ili apate pesa ya kwenda mziki.

Uanaume ni kuwa na maono na Kupambana, hiyo Roho ya uza uza ishindwe Kwa Jina la YESU.
Ni mkosi kuuza kitu ulicho kitafta
 
Usiuze nyumba Ila
Kama unaweza ukajibana ukapangisha nyumba zima wewe na mkeo mkajibana uswahilini vyumba ya bei rahisi wakati unaset mipango mingine Ila nyumba yako ukaitumia Kama chanzo kimoja wapo cha mapato yako, watu wengi nimeshaona wanafanya hivi , mipango Yake ikikaa sawa anarudi kwenye mjengo wake.
 
Back
Top Bottom