Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Inaelekea mzee alianza kugonga muda mrefu na pia mafao mnayomtumia maza huwa anapata mgao. Si rahisi uchumba uanze baada ya kifo na wawe na guts za kutangaza ndoa.
 
Mwambie Mama atulie, miaka 68 siyo ya kuolewa, kama ana force akaishi kwa muoaji
 
Kwa umri wa Miaka 68 mama bado anataka Nini lakini sio tabia njema kabisa mie bibi yangu babu alikufa kamuacha kwenye miaka 50 hakutaka kabisa kuolewa coz tayar alikua na watoto wakubwa mpaka Leo yuko kwenye miaka 80 Wala hatukuwahi hata kusikia tetesi bibi anamwanaume mwingine
 
Akisoma hii comment hasa hasa hiyo namba 4 lazima ataomba maji ya kunywa
 
Kuna "silent killers" mkuu, wazee wa zamani walikuwa wataalamu wa kuchepuka na hauwezi hata kuhisi.
 
Ushauri wako ni mzuri wa kukataa kumhudumia akiwa na huyo baba ako wa kambo.
Lakini muulize mama yako kwa nini anataka kuolewa.
Then muulize kama bado anafanya mapenzi, inawezekana huyo baba ako kisha mla sana hadi sasa wanataka kuoana. Usimnyime haki yale ambayo huwezi kumpa. Mkumbuke Graca Machel na Mandela walioana wakiwa watu wazima sana.
Wewe endelea kumhudumia mama yako na huyo baba ako mwache amkaze mama yako, mama yako amepata mkunaji wa vipele, je una dada wa kumhudumia mama yako, kama huna mwache huyo man amhudumie.
Hiyo amount ya pesa usione ni shida kumpa mama yako.
Acha wivu inawezekana huyo baba naye kafiwa na mke lazima wasaidiane mambo ya sirini ambayo watoto hamwezi
 
Wewe ni phaler nini? Baada ya kushauri vitu vya msingi unashauri upuuzi. Au wewe ni mtoto wa huyo mzee? Hajakatazwa kuolewa, aolewe ila huyo mzee amchukue akaishi naye kwake, sio anamuoa anang'ang'ania kubanana naye kwenye nyumba ya marehemu. Hatutaki mazee ganda la ndizi hapa.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Upuuzi nilioshauri ni upi hapo?
Nimeshauri mambo mawili tu.
1. Tunza wazee wako
2. Usiingilie mapenzi ya wazee wako.
Hebu tuambie upuuzi ni upi hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…