Naombeni ushauri ndugu zangu, seriously kabisa. Kuna sauti kila siku haiishi kuniambia kuwa mke niliye nae sio!

Daah basi ningekupa huyu nilienae basi ungekufa mapema,..vumilia ndugu kunamahali unaweza ukamuacha huyo ukapata kituko ambacho utajuta zaidi.hayo mapungufu yakawaida kabisa
 
Kiongozi, hiko kichwa kina ubongo unaofanya kazi? Kuwa mwanaume hakukufanyi uwe kichwa tu kwenye familia....Kuna vichwa vingi vya familia, familia haina chakula, ada za shule zinahitajika; baba pesa yote amemaliza baa.
That's what I think....sijamuelezea mtoa mada kuwa sio kichwa bora cha familia.
 
Dah! wanawake wanavyoona huu uzi wanathibitisha kwamba wao ni wa kuchokwa chokwa tu😁
 
Wewe ndio huvumiliki...
Mhh hiyo no 5 mimi ungenifukuza ndani ya wiki
 
Kwa kifupi unachukia kuwa kwake binadamu. Maana uliyoyaandika kama dosari ni mambo ya kawaida ya kibinadamu.
 
Swala la msingi hapa ni; je hiyo sauti ipoje??, inakujia vipi na katika wakati gani??, ni sauti ya kike au kiume??, inatoa sababu gani za msingi??

Vinginevyo ni sauti ya kichawi/kishetani dhidi ya ndoa yako. LABDA kuna demu, mchepuko kama unaye au adui ya mkeo nk yupo behind the action, kumbuka dunia ina mambo.
 
Huyo ni mkeo, hakuna tena nafasi ya kugeuka na kumuacha. Sauti za kihisia unapaswa uzipuuze.
 
Sio wew tu unaesikia hako kasauti,karibia wanaume wengi tunakasikia ila tunakapinga na kuendelea kuwa na wake zetu
 
Ushauri wangu ni utafute sound recorder iweke irekodi hiyo sauti ukiwa usingizini tena ukiwa unaiuliza hiyo sauti sababu za kukuambia hivyo. Ukiamka sikiliza conversions zenu utapata ukweli
 
labda haumpendi au ulikua naye kwa shinikizo ... changamoto hazikosekani bro na hasa mapungufu ya wenza wetu tukishayatambua inatupasa kutambua namna ya kuyakubali ...
zaidi binadamu hakuna aliyekamilika...
 
Huyo ni mke na mna mtoto mkuu..chochote utachoamua hakilisha unaamua kwa umakini
 
Una jini mahaba. Ombewa
 
Me navyoona huyo ulonae unampotezea muda na utapata mwingine itakua vivohivyo, yani kama uwez kutunza mapungufu ya mwenzio na kuyafurahia mazuri yake ww shimo lako ni wale wadada wa buku buku basi.
 
Utampata wapi asie na mapungufu? Kwa wastani kila binadamu ana angalau tatizo moja sasa hapo wewe mkeo na mtoto jua tayari una matatizo 3 ya kusolve, kuwa kichwa cha familia sio mchezo
Ahsante
 
Mkuu kabla sijatoa ushaur wangu,naomba uwe mkweli juu ya hili ninalotaka kujua,litanidhibitishia kile ambacho naona ni tatizo

Huwa unajisikia kusex nae au kama unajilazimisha?
Ukweli najivuta sana, huo ndo ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…