Naombeni ushauri ndugu zangu, seriously kabisa. Kuna sauti kila siku haiishi kuniambia kuwa mke niliye nae sio!

Naombeni ushauri ndugu zangu, seriously kabisa. Kuna sauti kila siku haiishi kuniambia kuwa mke niliye nae sio!

Hiyo na 2,3&4 ni red flag za kutosha kabisa, bila shaka amelelewa na mama peke yake au kama baba yake yupo basi hana nguvu katika familia. Kumruhusu
mkeo kumsikiliza mama yake ni kosa kubwa coz unaruhusu ndoa yako iendeshwe kwa rimoti kutoka ukweni(kama sirikali inavyoendeshwa toka pwani) na ukiendelea kuruhusu hilo na mwanao kama ni wa kike ataenda kumjibu mumewe kama wewe unavyojibiwa na mkeo coz anakua na kujifunza na kama unavyojua maskio ya watoto ni macho.. Akiwa wa kiume ataendeshwa na mkewe
 
Hii thread inachekesha kwakweli!!!

-Wewe ndie mwenye Matatizo sababu unataka uingilie Uhuru wake umpangie hadi Mavazi eti avae according na wewe unavopenda while mwili ni wake yy Eboh😏

-Asizoeane na Mzazi wake ili iweje? Wewe utajiskiaje watoto wako wakija kukutenga sababu Wapenzi wao Wametaka hivo?

-Hilo Suala la kulima bora hata huyo kakubali kushika jembe😏

-Eti Ucheshi nayo ni kasoro!! Unataka ajitenge na Dunia nzima aambiwe anaringa.. ucheshi ni Karama si kila mtu kapewa..
 
Mhimu ni kuzungumza nae mkuu. Wengine huona ya kawaida lakini ni vema kuyaweka wazi na mkajadili kwa pamoja ili yaishe au kupungua. Mama wakwe wengine wanakera si kidogo na ndugu wengine wa mke. Wakati mwingine huweza hata kuchangia ndoa kuvunjika. Utoaji wa taarifa zisizo rasmi kutoka ukweni kupitia kwa mkeo kuja kwako. Zungumzeni ili muweze kubalance mambo vizuri. Ucheshi na aina ya mavazi ni mambo yanayozungumzika sana. Labda kakulia uswahilini,,ahahaha
Dawa ni kumpenda na afahamu kuwa unampenda kisha angalia mrejesho kutoka kwake,Mkeo akiwa mzuri mawazo kama hayo unaweza kupata hasa kama Muda mrefu unatumia kazini
 
UMETUTAJIA KASORO PEKEE... HAIWEZEKANI AKAWA KASORO PEKEE... KUNA ULICHOMPENDEA MWANZO... NA TUPE NA UPANDE WA UZURI WAKE KIUMBO NA KITABIA ZINGINE...

ALAFU TUTAKUSAIDIA KUKUPIMIA ANAKUFAA AU HAKUFAI!
 
hiyo ni sauti ya shetani mzee achana nayo. Ukiikubali tu imekula kwako na maisha yako yataaribika moja kwa moja.
 
Kusema za kweli haki we unamtafutia sababu tu huyu Dada umuache. Na hapa Kuna mawili, eiza una limchepuko linakuharibu akili au umerogwa. Au vyote fullstop
 
nd
Ni mwaka wa 3 nipo na huyu mke na mtoto mmoja tayari; sijawahi kukamata sms ya ajabu wala kumkamata au kupata taarifa za kuchepuka kwake (labda watu wananiheshimu na hivyo hunistahi kwa kutoniambia), lakini pamoja na hayo nafsi yangu, katika kipindi chote, haiachi kuniambia kuwa hapa siyo sehemu sahihi.....nimepotea.

Kila nikijaribu kuipotezea sauti hii huwa inajiongeza hadi kufikia kuniamsha usingizini wakati mwingine.

Tuna viutofauti kadhaa, ndiyo, lakini mimi mwenyewe sijawahi kuvifanya kuwa hoja sana (kuvifikiria kupitiliza kiasi cha kupata hisia hizi hasi.....naona ni vitu vya kurekebishika vikidanyiwa kazi ipasavyo). Baadhi ya viutofauti gtetu ni hv hapa;

1. Kupenda kuvaa madera (mi si mfuasi wa madera),

2. Kulalamika lalamika ( sipendi makelele makelele miki),

3. Kuzoeana sana na mama yake,

4. Majibu ya jazba yanayopelekea ugomvi kati yetu,

5. Uchapakazi hafifu (si mwenye kuweza kulima ipasavyo),

6. Ucheshi unaompelekea kuzoeleka kirahisi (hii changamoto nayo wakati mwingine).

Uamuzi bora ni upi hapa wa kuchukua wadau?!!!

Sauti inaongezeka siku baada ya siku na hali ndo kama hivyo.
ulikurupuka broh kwaiy ulitaka amzoee nani au unatka kula kuku na mayai
 
Mama yake ndio binadamu wa kwanza kumuona alipoanza kupata ufahamu,huwezi kuzuia hilo.....sema tu humtaki
 
itakuwa ni mchawi labda
inawezekana kuna vitu anafanya kwenye ulimwengu wa giza,ndoto za hivyo sana sana ni ukiwa unaishi na mshirikina unaweza kutahadharishwa kupitia ndoto ni muhimu kumchunguza na kuchunguza familia yake kwa umakini
si jambo la kupuuzia
 
Hapa kwenye [emoji116]

5. Uchapakazi hafifu (si mwenye kuweza kulima ipasavyo),

Nakushauri:
Nunua powertiller, inalima speed mno.
Ni million 10 TU unaepuka hii kero mkuu[emoji41]
 
On serious note,
Yote uliyoelezea nmegundua
Mkeo ana tatizo la ujuaji mwingi.

Yaan she's is too much know,

Na hili Ni janga sana pale baba unapotaka kusimama fully Kama Kichwa Cha familia.

Cha kufanya,
Tumia "martial law" atarudi mstarini[emoji41]
 
Sasa kuvaaa deraa ni tatizoo..sasa ingekuwaa Kama sisi wavaa vimin..suluari na vipensiii...[emoji28][emoji28][emoji28]sijaonaa tatizoo
Ha ha ha....
Madam hicho kipensi unakibaliaga wapi?[emoji4]
 
Wanasemaga kuna watu hawajuagi kudumu muda mrefu kwenye mahusiano huenda na wewe ni mmoja wapo.
 
Back
Top Bottom