Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

Nilisikia vipindi vitaongezwa kwa kila darasa, kwa namna moja ama nyingine nguvu ya ziada(kwa walimu na watumishi wengine) itatumika kwa hivyo wazazi na wenye shule mkae mjadiliane kuhusu ada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa ambazo zililipwa na wazazi kwa ajili ya chakula na malazi zitumike kulipia hiyo nguvu ya ziada itakayotumika.
Hata sisi wenye watoto tumetumia nguvu ya ziada kukaa nao home, miezi mitatu siyo mchezo, watoto wamenenepa sare zao shule zinawabana tunaanza upya kununua sare nyingine mpya[emoji23]
 
Kiongozi umekula ada? [emoji23]


Hicho chakula watakila katika siku zilizoongezwa. Alafu wataongezewa share watarudi wakiwa wamenenepa[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyu mtoto ambaye kwa kumuongezea masaa mawili kila siku ya masomo hamuoni kama mtauchosha ubongo wake badala ya kumsaidia? Pili yale mapumziko yaliyowekwa katkati ya term ya masomo yana maana kubwa kwa mtoto kuweza kujenga ubongo wake ili uweze kuelewa masomo yake vyema kwa hiyo nafikiri kuna kitu hakijafikiriwa vizuri kabla ya kutoa huu muongozo wa masomo
 
Private schools wanataka kulifanya madhara ya janga la Korona mzgo waubebe wazazi..
Hili halitakubalika biashara ya shule binafsi ni sawa na biashara zngne ambazo wateja wao ambao ni wazazi ama walezi wanazo..hapa wamiliki wa shule wajue kuwa hakuna biashara isiyo na changamoto ..kwny biashara lazma wote tujue kuna hasara na Faida..Korona imeua secta nyingi za wateja wa private schools huu ni ukweli usiopingika. Haiwezekani wazazi ambao wengi wao wamepoteza ajira na vipato walazmishwe kulipa huduma ambazo hawakupewa watoto wao haiwezekani asilani.
Kuna rafiki yangu anashule amewatangazia wazazi kuwa hawatalipa huduma ambayo hakutoa kwa watoto wao. Hyu amefikilia mbali sana kuwa busara ni msingi wa kuendesha mradi wowote wa kijamii...
Na washauri wamiliki wa shule kuwa huduma yao ni biashara hivo wasiwatwishe wazazi madhara ya Korona kweny biashara zao..
Bali wawe imara kuvumilia changamoto hii vingnevo kuna shule ztakufa badae mana jinsi mradi wako unavyotreat wateja ndvo unastawi ama unakufa...
Huu ni wakati wa kuwavumilia wateja sio wakati wa kuumiza wateja!!kumbukeni" Wema wako wa leo ndyoo mtaji wako wa kesho"
 
Huu ni wizi outright.Huwezi kutoa punguzo la100,000 tu wakati mtoto hakulala,hakutumia maji,hakutumia umeme nk.Kwanza mwaka huu ideally ada ya mwaka inatakiwa ipunguzwe kwa at least robo,au ideally kuwe na dialogue kati ya wazazi na wamiliki wa shule wapate muafaka wa pamoja.Shule haziweze kutoa matamko tu,kwani wao ni akina nani,miungu?That is wrong.Hapa ni lazima serikali itumie mamlaka yake.Mmiliki asiyetaka kufuata haki anyang'anywe leseni.
 
Wazazi wengi wanaibiwa kwenye BIMA ya AFYA mashule mengi hayapeleki NHIF na Watoto hawapewi kadi
 
hakuna kitu kama hicho, ada utalipa pale mtoto alipo anzia kwenda shule, yani kuanzia mwezi julai 2020, na kwa wale amabao walilipa ada ya mwaka mzima lazima itatolewa miezi 3 ambayo hawajangia darasini, yani kuanzia mwezi 4 mpaka wa 6 ambapo wanafumzi hawajaingia darasani.


nadhani kunahaja wizara itoe tena ufafanuzi kwenye jambo la ada kwa shule binafsi kabla hazijafunguliwa kuliko kusubiria purukushani zianze halafu ndio waziri azu gumze hapana,
kwa sasa kuna kila dalila baada ya kufungua shule hiyo trh 29 kutatokea mtafaruku kati ya wazazi na wamiliki wa shule,
 
Ukitaka kujua uchumi halisi was maisha ya mtanzania pitia huu Uzi.

Watu wanashindwa kulipa laki 1 au milion 1 kwa nchi inayojivunia kuwa tajiri na donor country. Haya ndio maisha halisi sisi watanzania sio hayo ya wanasiasa eti tuko vizuri.


Vizuri ya nyoko [emoji1]
 
Na Sisi ambao tushalipia mwaka mzima kuna chenji?
Acha tu, siku zote mfanya biashara anataka mgawane hasara ila faida anaimudu yeye mwenyewe.

Elimu ni biashara kama biashara zingine ndio maana Kuna St. Katumba, English medium, International school nk,hapo utachagua elimu kuendana na pesa yako.

Swala la chenchi tena.........
 
Issue sio hali ngumu ni kuzingatia mikataba iliyokubaliwa kati ya mzazi na shule
Mwenye hela hawez kubargain kutoa laki 1 kwa shule ukizingatia shule nyingi zimeyumba kwa covid. Kwanini usitoe Kama sehemu ya kusaidia ?!!


Huna hela kapuku wewe. [emoji1]
 
Mtoto bado Yuko chekechea unamlipia kwa mwaka milion 2.5 bado hajafika shule ya msingi , secondary na chuo halafu anakuja kulipwa mshahara wa laki 9 ...


Wazazi fikirini nje ya box
Wazazi wanatofautiana mwingine anataka mwanawe a enjoy kadri anavyokua kuanzia akiwa mtoto kusoma Best schools nk mzazi mwingine anataka mwanae aje a enjoy mali za mzazi, mzazi akifa!!!

Hayo mambo ni family choice ya mzazi unataka mwanao afaidi chako lini ukifa au ukiwa hai? Na si kila mzazi yuko interested na return kuwa mwisho wa siku hizo pesa zitarudi au la Mtoto atamtunza mzazi baadaye au LA. Mzazi anachofanya ni kumpa raha mwanawe akulie, asome kwa raha nk mbeleni asije lalamika Kuwa hajawahi ishi maisha mazuri
 
Mwenye hela hawez kubargain kutoa laki 1 kwa shule ukizingatia shule nyingi zimeyumba kwa covid. Kwanini usitoe Kama sehemu ya kusaidia ?!!


Huna hela kapuku wewe. [emoji1]
Msaada haulazimishwi huombwa
 
Ujinga ni huu kulipisha wanafunzi ada ili zipatikane pesa za kulipa walimu, kodi wakati hakuna ufundishaji wowote uliofanyika. Kwa logic hii hata waliofunga biashara zao wanapaswa kuwalipisha wale wateja wao (wale wanaofahamika) ili zipatikane pesa za kodi, kulipa wahudumu etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…