Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

Naona shule zimeanza ukorofi, wanatoza ada ya muhula ambao wanafunzi wamekuwa nyumbani

Hivi huyu mtoto ambaye kwa kumuongezea masaa mawili kila siku ya masomo hamuoni kama mtauchosha ubongo wake badala ya kumsaidia? Pili yale mapumziko yaliyowekwa katkati ya term ya masomo yana maana kubwa kwa mtoto kuweza kujenga ubongo wake ili uweze kuelewa masomo yake vyema kwa hiyo nafikiri kuna kitu hakijafikiriwa vizuri kabla ya kutoa huu muongozo wa masomo
Ndugu unashauri kipi ambacho kingekuwa ni vizuri zaidi?


Au mwaka wa masomo ungefutwa na kuwataka wanafunzi warudi January?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue sio hali ngumu ni kuzingatia mikataba iliyokubaliwa kati ya mzazi na shule
Mkataba mtoto wako alitakiwa kusoma kwa masaa 8 kwa siku, alitakiwa kupumzika wiki mbili September na alitakiwa kufunga tarehe 4 December.


Fanya kutii mkataba mbona hamtagombana na shule utagombana na Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii itakuwa ni crushing program.
Wazazi tupunguze jazba.

Nilipata nafasi ya kuutazama waraka unaoelekeza kufunguliwa kwa shule zote.

Unawataka walimu/shule kufidia muda ambao wanafunzi hawakuwapo.

Shule zimetakiwa kuongeza muda wa masomo kila siku kwa saa mbili.

Muhula wa kwanza uliokuwa uishe mwezi June mwanzoni, kwa sasa utakamilika mwezi August mwanzoni.


Muhula wa pili hautakuwa na Likizo na wanafunzi watasoma mpka 18 December.

Sasa hapo ni jitahada za kumtendea haki mwanafunzi. Shule pia zitendewe haki.

Ada yako itasaidia kuinua hali za walimu ambao kila siku wamekuwa wakisemwa wanafanya kazi katika mazingira duni. Wazazi kwa pamoja tutimize wajibu wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga ni huu kulipisha wanafunzi ada ili zipatikane pesa za kulipa walimu, kodi wakati hakuna ufundishaji wowote uliofanyika. Kwa logic hii hata waliofunga biashara zao wanapaswa kuwalipisha wale wateja wao (wale wanaofahamika) ili zipatikane pesa za kodi, kulipa wahudumu etc
Mwenye hela hawez kubargain kutoa laki 1 kwa shule ukizingatia shule nyingi zimeyumba kwa covid. Kwanini usitoe Kama sehemu ya kusaidia ?!!


Huna hela kapuku wewe. [emoji1]
Kwani CoVD iliathiri shule tu ? biashara za wazazi wenye watoto shule hazikuathirika? Kwa nini waamini ni wao tu shule kuwa wao tu ndio biashara ya shule iliathirika lakini Mzazi vyanzo vyake vya mapato havikuathirika hivyo alipie miezi shule iliyoathirika na corona na kufungwa kwa kuwa yeye mzazi kipindi cha Corona yeye mapato yake yalikuwa stable kama kawaida hivyo alipe !!!!
 
Ndugu Mzazi/Mlezi;

*Kuelekea kufungua Shule(Toka likizo ya Janga la corona), ADA YETU ITAKUWA KAMA IFUATAVYO:-

1. Ili kuwapa wepesi wazazi katika kufanya Malipo ya Ada kutokana na Janga hili la korona, Uongozi umeamua kupunguza ada kwa kiasi cha Sh. 100,000/= (Shilingi laki moja). Hivyo bas:-

● Kiwango cha Ada ya awamu ya Pili(Mwezi March) ni Sh.500,000/= badala ya Sh.600,000/= hapo mwanzo.
●Awamu ya Tatu(Mwezi June) ni Sh.500,000/=
●Awamu ya Nne(Mwezi septemba) ni Sh. 500,000/=
● *Baada ya punguzo hilo, Jumla ya Ada kwa Mwaka huu itakuwa 2,500,000/= Badala ya 2,600,000/= hapo kabla.*

2. Mara tu Mwanafunzi atakaporipoti atatakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 1,000,000/= (ambayo ni mjumuisho wa awamu ya Pili na ya Tatu kama ilivyoainishwa hapo juu)[emoji115]

●Ili uendeshaji wa Shule uende ipasavyo, mwanafunzi anatakiwa alipe kiasi chote cha Sh. 1,000,000/= (milioni moja) kabla ya siku ya kuripoti shuleni.

3. Kwa wanafunzi wanaodaiwa ada ya awamu ya kwanza wanatakiwa kukamilisha kiasi chote cha deni hilo pamoja na Malipo ya Awamu ya Pili na ya Tatu Sh.1,000,000/=

6. Wanafunzi wote wasiolipia BIMA YA AFYA TSH. 50,400/= wanakumbushwa kulipia katika akaunti za Shule na kukabidhi risiti hiyo kwa Muhasibu ili asajiliwe na kuweza kupata huduma ipasavyo.

Tunawaomba wazazi/walezi kukamilisha Malipo kama yalivyoelekezwa na Uongozi wa Shule ili kufikia Malengo yetu kwa pamoja.

N:B. Malipo yote yafanyike kupitia Akaunti za shule:-
AMANA BANK
Acc Name: IBN JAZAR ENGLISH MEDIUM SCHOOL
Acc No: 001120310750001

KCB BANK
Acc Name: IBUN JAZAR ISLAMIC ENGLISH MEDIUM NURSERY AND PRIMARY SCHOOL
Acc No: 3300618819

NBC BANK
Acc Name: IBUN JAZAR ISLAMIC ENGLISH MEDIUM NURSERY AND PRIMARY SCHOOL
Acc No: 048132000088

Kwa maelekezo zaidi:
0658514451 Mkuu wa Shule
0659907513 Muhasibu.

Shukran
Duuh 1M ulipe kwa pamoja kazi ipo, Bora ukampeleke mwanao Kayumba kuunga mkono jitihada za mkuu za maendeleo[emoji23][emoji23]
 
Mzazi hajaingia mkataba na serikali ni na shule
Naanza kupata mashaka na wewe.

Kwa namna nyingine unataka kuzishinikiza shule binafsi zipingane na Serikali.

Unapogoma kulipa hiyo ada inamaana wamiliki wa shule wakaigomee serikali ule muda walioongeza. Wakaiambie serikali kwamba wazazi wamegoma kulipa ada, kwa hiyo watoto hawatasoma masaa mawili ya ziada, watafunga likizo ya siku 14 September na shule zitafungwa tarehe 4 December.


Nimejisikia vibaya. Ni vile unataka kuihujumu serikali indirect.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina mkataba na kodi ya majengo ya shule, sina mkataba na mwalimu kuhusu mshahara wake.

Kama ni hivyo mwenye shule nae awe na mkataba na biashara zangu, siku zikienda sawa nisimlipie ada mtoto kwakuwa nina kodi za kulipa.

Bahati tu watoto wangu wako shule ya Tambuka Reli Pr School, vinginevyo pangechimbika.
Nafundisha hapo mkuu. Nipe jina lake ili nimlee kama mwanangu.
 
Naanza kupata mashaka na wewe.

Kwa namna nyingine unataka kuzishinikiza shule binafsi zipingane na Serikali.

Unapogoma kulipa hiyo ada inamaana wamiliki wa shule wakaigomee serikali ule muda walioongeza. Wakaiambie serikali kwamba wazazi wamegoma kulipa ada, kwa hiyo watoto hawatasoma masaa mawili ya ziada, watafunga likizo ya siku 14 September na shule zitafungwa tarehe 4 December.


Nimejisikia vibaya. Ni vile unataka kuihujumu serikali indirect.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hana hela huyo kazi kupiga fujo mitandaoni shilingi laki 1 inamtoa mapovu hahahaha
 
Mzazi hajaingia mkataba na serikali ni na shule
Huna hela wewe vuvuzela unatokwa mapovu kwa laki moja hela ya bia hata hulewi. Nilijua mnavyopiga kelele humu kuwa awamu hii imeleta Maendeleo nikajua wenzetu watoto wenu wanasoma international schools ...


Mna ukwasi wa milion 500+ kwenye bank account zenu ... Kumbe ada za shule za milion 1 kimbembe.


Hahahaha nasema tena tajiri hawez kubargain hiyo milion 1 wewe una njaa tu na kapuku Kama sisi mnaotutukana kila siku
 
Hiyo iko wazi maana Kuna mda wa ziada kufidia mda uliopotea hivyo watoto watpewa Haki yao Kama kawaida. Na wewe mzazi mpatie haki yake mwanoa.

Elimu buru Nani kakwambie mwanoa umpeleke huko na elimu Ni ilele[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom