Naona Syria inaenda kuwa uwanja wa vita kati ya Iran na Israel; sijui Assad amekubalije nchi yake kila mtu kujikatia kipande chake

Hivi ukisikia adui yako aliyeapa kukufuta kaweka ghala la silaha kwa jirani yako ,
Ina maanisha nini
 
Vita ya Ukraine na Urusi ni tofauti kabisa na mgogoro wa Mashariki ya Kati.

Tangu kuanzishwa kwa Russian Federation, Ufaransa na Ujerumani zimekuwa kwenye mahusiano ya kidiplomasia na Urusi na zinawasiliana kupitia balozi zao. Unapotokea mvutano, mabalozi wa pande zote huwa wanaitwa na nchi walizopo kutoa maelezo, baada ya muda hali inatulia. Urusi inatambua huo uhusiano uliopo na umuhimu wake hivyo sio karata nzuri kwao kijeshi/kivita kushambulia balozi za hizo nchi na hatimaye kuanzisha vita na mataifa hayo ama na NATO kwa ujumla. Hiyo haina maana kwamba Urusi huwa haishambulii maeneo mengine ya kiraia.

Huo uhusiano niliousema ni tofauti na Israel na Iran ama Israel na Syria ambazo hazijawahi kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na hata sasa hazina uhusiano wa kidiplomasia. Hizo nchi zilishatangaziana vita zamani na tayari ziko kwenye vita hivi sasa.

Kitendo cha Israel kushambulia pale ubalozini Syria ni muendelezo wa vita ambayo ilishaanza muda mrefu. Ukitaka kufahamu hilo, fuatilia itikadi, mafundisho (doctrines), matamko ama pro-war rhetoric pamoja na operesheni za kijeshi zinazofanywa na Iran na washirika wake dhidi ya Israel.

Mfano halisi wa pro-war rhetoric ni ile kauli ya rais wa zamani wa Iran kwamba "Israel inapaswa kufutwa kwenye ramani ya dunia". Hiyo ni kauli inayoashiria vita iliyopo. Iran na washirika wake katika hiyo "Axis of Resistance" wanaitazama Israel kama "mvamizi" wa ardhi ya ile iliyokuwa "Palestine" na kwamba haipaswi kuwepo mahali hapo. Hilo ni tishio kamili la kiusalama kwa Israel ndio maana wakati mwingine Israel huwa inafanya preemptive strikes kabla haijashambuliwa.
 
Mchambuzi wa masuala ya vita ukiwa Gongo la Mboto.
 
Wameumbwa Ila Wana maarifa na uwezo wa mkubwa Sana kuliko mataifa mengi
Ndo maana aliweza kuwatandika mataifa mengi kwa wakati mmoja NDANI ya siku sita tu
Lakini Wana Agano la milele na Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo
Kama ni Mungu wa Waisraeli sawa nikajua Mungu wa kweli wa ulimwengu wote.
 
Basi tusubiri kitakachotokea.
Ila Israel ni nchi iliyojikokea moto yenyewe kupitia matukio yake ya nyuma.
 
Hivi ukisikia adui yako aliyeapa kukufuta kaweka ghala la silaha kwa jirani yako ,
Ina maanisha nini
Tujiulize haya maghala yalianza kuwekwa 2011.
Kwanini yakawekwa??
Hizo kauli hazina miaka mingi toka zitamkwe,kwanini zilitamkwa??
Israel kama angekubali kuipokea Palestina kam taifa huru na kama USA ingeridhia kuitambua Palestina kimataifa,kama Israel isingeanza expansion 1948,kama Israel isingeanzisha migogoro mengine 1956 Egypt,1957 Syria unadhani haya yote yangetokea??
Embu tutizame kabla ya 1948 middle east ilikuaje??
Israel ni sababu ya haya yote.
Na sasa hivi middle east nzima ishakua inajiona haiko salama kwa uwepo wa Israel.
Na ndio maana mie nikashikilia kuwa Israel inafanya mambo kwa kutizama utashi wake.


Hata tukitizama hii vita inayoendelea sasa hivi july,august wayahudi walikua wakivamia mashamba ya mabedui West bank na kuyachoma moto,Jenin nyumba zilianza kuvunjwa za wapalestina ili kutanua makazi ya wazayuni,watoto zaidi ya 100+wamekamatwa chini ya umri miaka 14 kwa kisingizio ni tishio kwa IDF kwasababu wanarusha mawe,toka lini mtoto akawa tishio kwa kurusha jiwe kwa mwanajeshi??
Hamas alipo react Octoba 7 wakawachukulia Hamas magaidi,sasa tujiulize kipindi Yair Lapid alivyokua kiongozi wa mpito Israel na Palestina waliishi vizuri kiasi kuna mpaka waisrael wamejenga na kuanzisha biashara Gaza,ila aliporudi Netanyahu kwa nini haya yote yakatokea??
Je aliyofanya IDF na wayahudi kushambulia mashamba ya mabedui,kuvunja nyumba Jenin je huo sio ugaidi??
Ukitizama kiuhalisia Israel inafanya mambo kiutashi.
Hii ndio hoja yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…