Putin alikosa busara,alidhani nchi za Magharibi hazitaungana hasa Ujerumani na Ufaransa kumdhibiti Putin.
Akategemea China huku China yenyewe inajua kuunga Putin ni kuwekewa vikwazo vya kubiashara na nchi za Magharibi.
Vile vile China anataka Russia dhaifu.
Kuungwa mkono na nchi za kiafrika hakuna impact ya kiuchumi wala kijeshi.
Iran nayo fuata mkumbo na drones zake ameishapoteza President Raisi.
Uturuki yeye anakula na kupuliza.
Kiduku wa Korea Kaskazini yeye anataka kufa na mtu siyo ishara nzuri kwake kwani Japan na Korea Kusini,Taiwan,Australia na Marekani wameongeza nguvu ya kivita kumdhibiti Kim.